SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 22 Mei 2016

T media news

Van Gaal akiri Imefika Mwisho – Neville Asema Mourinho Ataleta Makombe Lakini Hatodumu

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal aliondoka katika hoteli waliyofikia na tiku yake huku akizungumza maneno kwamba ‘it’s over’ baada ya jana kuripotiwa rasmikwamba Jos Mourinho angechukua nafasi yake.

 
 Kocha huyo wa kidachi aliulizwa na ripota wa Sky Sports kama angekuwa na muda wa kuongea, van Gaal akajibu:  ‘It’s over.’ Akitoa ishara kwamba labda tayari ameshafukuzwa kazi. 

Kauli hiyo fupi imezidisha kusambaa kwa kwa taarifa za kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 yupo njiani kuondoka Old Trafford. 

Jana, muda mfupi baada ya kushinda ubingwa wa FA Cup – taarifa zilizosemekana kutoka kwa wakala wa Jose Mourinho zilizema kwamba mteja wake Jose Mourinho angembadili Van Gaal katika uongozi wa benchi la ufundi la Manchester United. 

 
 Mourinho aliondoka Chelsea baada ya kufukuzwa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya kwa mabingwa watetezi wa EPL kwa wakati huo.  

Kocha huyo mreno pamoja na kwamba amefanikiwa kushinda makombe kwenye nchintofauti baraji ulaya lakini hajawahi kukaa kwenye klabu moja kwa zaidi ya miaka mitatu na miezi 3 aliyokaa wakati akiwa Chelsea katika awamu ya kwanza.

Jambo hilo limepelekea kocha msaidizi na nahodha wa zamani wa Man United, Phil Neville kuzungumza kwamba Mourinho hatokaa muda mrefu OT lakini ataipa makombe. 

‘Sioni kama atakaa muda mrefu pale Man Utd, labda miaka miwili au mitatu,’ Neville aliiambia BBC Radio jana.

‘Wakati Jose anapoondoka katika klabu huondoka huku akiwa amekosana na baadhi ya wachezaji wake.

‘Jambo hili lilitokea akiwa Chelsea, pia wakati anaondoka Real Madrid – kulikuwa na taarifa aligombana na baadhi ya wachezaji wake. 

‘Hii ndio system ya Jose, anakuja kwenye klabu, anapata mafanikio lakini hakai kwa muda mrefu.’ 

United mpaka leo wameshindwa kumaliza juu zaidi ya nafasi ya 4 katika Premier League tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu.