SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 20 Mei 2016

T media news

Lungi amtumia Snura kuwabipu Waislam



Msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
Na Hamida Hassan
Wakati Waislam wakipiga vita kitu kinachoitwa Vunja Jungu, msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga ameandaa shoo hiyo huku akimtumia Mwanamuziki Snura Mushi.

Snura Mushi
Lungi aliitonya safu hii kuwa, anajua Waislam hawapendi sherehe hizo lakini yeye ameamua kufanya ili kuwatafutia watoto yatima pesa ya futari.
“Najua Waislam watanimaindi na kuna ambao wameshaanza kuniambia nawachokonoa Waislam lakini sina nia mbaya, lengo ni kuwasaidia watoto yatima na nitafanya hivyo mwisho wa mwezi ndani ya Ukumbi wa Travertine Magomeni Dar,” alisema Lungi.