SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 23 Mei 2016

T media news

LULU DIVA AFUNGUKA KUHUSU KUMWOGOPA BARAKA


 

Lulu Abassi ‘Lulu Diva.
Stori: Hamida Hassan, Wikienda
Dar es Salaam: Muuza nyago (video queen) maarufu Bongo, Lulu Abassi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kudai kuwa akikutana na mkali wa Bongo Fleva, Baraka Andrew Odiero ‘Baraka Da Prince’ hawawezi kusalimiana kwani anamuogopa kama ukoma kwa madai kwamba alimchonganisha na mpenzi wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

Baraka Andrew Odiero ‘Baraka Da Prince’
Akizungumza na Wikienda, Lulu Diva alisema kuwa Baraka alimpelekea Nay umbeya na kumtangazia ubaya kwa sababu waliwahi kuingia kwenye uhusiano lakini yeye aliamua kuachana naye kwa sababu aliona hawatafika mbali.
“Baada ya kuachana na Baraka, alianza kunitangazia ubaya kwa Nay kuwa sifai, kisa kikiwa ni kumpiga chini hivyo namuogopa kama ukoma,” alisema Lulu Diva.
Baraka alipotafutwa alimkana Lulu Diva kuwa hajawahi kuwa naye na wala hapendi kumzungumzia.