Hivi ndivyo Liverpool inavyoweza kuifanyia roho mbaya Man Utd isiweze kushiriki hata Europa

Kufuatia matokeo ya jana usiku ya Jumanne katika uwanja wa Upton Park, matumaini ya Manchester United kucheza kwenye michuano ya ulaya msimu ujao kuwa kwenye mashaka makubwa.

 
 Kikosi cha Louis van Gaal kilisafiri mpaka West Ham wakiwa wanafahamu gika kwamba ushindi katika mechi ya jana na ya mwisho ya ligi dhidi ya Bournemouth ungewahakikishia nafasi ya kushiriki Champions League.

Lakini Wagonga Nyundo wa London wakashinda 3-2, na sasa Man United wana hatari ya uwezekano wa kucheza msimu wa 2016-17 bila uwepo wa michuano wa ulaya yote. 

 
 Kufuzu Europa League 
Chini ya sheria zilizopo, timu yoyote itakayomaliza nafasi ya 5 na 6 katika Premier League msimu huu basi itafuzu kucheza Europa League msimu ujao. 
Kwa namna ilivyo, ikiwa West Ham waliopo nafasi ya 6 hivi sasa, nafasi moja nyuma ya Man United – wakifanikiwa kuifunga Stoke City katika siku ya mwisho ya ligi, basi watafuzu kucheza Europa League msimu ujao. 

Fainali ya FA Cup pia inaweza kuchangia timu za EPL zitakazoshiriki EL msimu ujao. Kwa namna ilivyo sasa mabingwa wa FA Cup watacheza Europa League. Hivyo ikiwa Manchester United itaifunga Crystal Palace watafuzu kuingia Europa League. Na Kama Red Devils watamaliza katika Top 6, basi timu ya 7 katika Premier League pia itafuzu Europa League. 

Southampton kwa sasa wapo nafasi ya 7, Saints wapo mbele ya Liverpool kwa pointi 2.

Nini kitatokea ikiwa Liverpool wataifunga Sevilla? 
Liverpool wana funguo ya matukio ya kushangaza katika wiki chache zijazo. 
Kikosi cha Jurgen Klopp kitakutana na Sevilla katika fainali ya msimu huu ya Europa League, na mshindi atapata nafasi ya kushiriki katika Champions League msimu ujao.  
Haya fikiria ikitokea Crystal Palace akashinda FA Cup. 
Ikitokea Eagles watawafunga Man United, na Liverpool wakashinda Europa League na wakamaliza nafasi ya 7, then EPL watapoteza nafasi yao moja  ya kushiriki Europe League. 

Hiyo ni habari mbaya kwa Southampton, na pia Man United, kwa sababu Man United inaweza kupitwa pointi na West Ham, Saints na Liverpool ikiwa vilabu hivi vyote vitashinda mechi zao za mwisho mwa msimu na United ikapoteza dhidi ya Bournemouth. 

Ikiwa Liverpool watashinda Europa League lakini wakamaliza nafasi ya 8 katika Premier League, basi yoyote atakayemaliza nafasi ya 7 atafuzu kucheza Europa League msimu ujao. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA