SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 22 Mei 2016

T media news

BAYERN YABEBA KOMBE LA UJERUMANI, GUARDIOLA AMWAGA CHOZI AKIAGWA


Bayern Munich imeishinda Borussia Dortmund kwa penalti 4-3 na kubeba ubingwa wa Kombe la Ujerumani.

Huo ni ushindi wa 11 kwa Bayern kushinda makombe mawili ya Bundesliga na Kombe la Ujerumani kwa wakati mmoja.

Lakini klabu hiyo, imemuaga vizuri kocha Pep Guardiola ambaye alishindwa kujizuia na kumwaga chozi. Kocha huyo anaondoka na kwenda kujiunga na Manchester City.

Timu hizo zilicheza kwa dakika 120 bila kupata mshindi na zikalazimika kupigiana mikwaju ya penalti.

Kipa nyota wa Bayern, Manuel Neuer aliokoa mkwaju ya Sven Bender na Sokratis Papastathopoulos akakosa.

Kipa mzoefu wa Dortmund, Roman Buerki aliokoa mkwaju wa Joshua Kimmich lakini Thomas Muller akafunga na kuifanya Bayern iendelee kubaki kwenye msitari.