Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2016

Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya bunge kuonyesha kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson

Picha
Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. Tulia Acksonkuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia. Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee. Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena. Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili. Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia. Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake...

CHECK VIDEO WIMBO WA DIAMOND PLATINUMS ZINAVYOTESA KUMBI ZA SATREHE MAREKANI

Picha

Mambo ya Msingi Kuyafanya Kabla ya Kuoa/Kuolewa

Picha
Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA' 1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati 2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya 3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana 4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja 5. Muwe wa imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa. 6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje 7. Pimeni afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine. 8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani. 9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi. N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukite...

Kosa lililowasimamisha Wabunge Saba wa Upinzani

Picha
Bunge jana limeazimia kuwasimamisha vikao wabunge 7 wa kambi ya upinzani kwa kosa la kukiuka sheria na kanuni za bunge na kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo imekwisha tolewa maamuzi kinyume na utaratibu wa kanuni za Bunge. Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari 27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na kiti hicho. Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Zitto Kabwe, John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Godbless Lema, Pauline Gekul na Esther Bulaya. Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6). Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Ester Bulaya naTundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Ku...

Baadhi ya Wabunge Wapongeza Wenzao Kusimamishwa

Picha
Baadhi ya wabunge wa chama tawala wamepongeza uamuzi wa bunge wa kuwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kutofuata sheria za bunge kwa kutaka kushinikiza kujadiliwa kwa hoja ambayo ilikuwa imeshatolewa maamuzi kuhusu bunge kurushwa live. Baadhi ya wabunge hao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye ameupongeza uamuzi wa Bunge na kusema kwamba ni lazima ifike sehemu adhabu itawale bungeni. Wabunge 7 waliosimamishwa wamepewa kitu wanachostahili kwa kuvunja kanuni. Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma amesema kwamba adhabu hiyo ni sawa kwa wabunge hao ili iwe fundisho kwa wabunge wapya. Kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amesema kwamba kusimamishwa huko kutajenga heshima ya Bunge na kuwa fundisho kwa wengine. Aidha Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu na Ester Bulaya vikao vya mkutano wa tatu na wanne, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Paulin Gekul, na Halima Mdee vikao vyote vya mkutano wa tatu na John Heche vikao 10 vya mkutano unaoendelea sasa.

Meneja wa Alikiba Afafanua Kuhusu ‘Alikiba TV’

Picha
Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi na msanii Ali Kiba, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’ Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi. “Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5. “Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza. Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote. Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recor...

MAJIBU YA AZAM FC KUHUSU KIPRE TCHETCHE KUTIMKIA UARABUNI

Picha
Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam FC Saad Kawemba amekanusha taarifa za nyota wao Kipre Tchetche kusaini kwenye klabu moja ya nchi za falme za Kiarabu lakini akasema, wapo tayari kuzungumza na klabu yeyote ambayo inahitaji huduma ya mchezaji huyo. “Taarifa hizo tumeziona na kwa maana ya wakati usajili hivyo ni vitu vya kawaida kwenye mpira, unasikiliza halafu unasubiri matokeo yake. Kwasasababu sisi ni klabu na nimeona kwenye mtandao mmoja amesema anamkataba na klabu na ni kweli bado tunamkataba naye wa mwaka mmoja”, amesema Saad Kawemba mtendaji mkuu wa klabu bya Azam FC alipohojiwa na Sports Extra ya Clouds FM. “Kwahiyo tunaamini yeyote ambaye anamuhitaji atafika kwenye klabu yetu tuzungumze. Lakini katika kipindi hiki cha usajili tunategemea mambo kama hayo kutokea kwa wachezaji wengi na si yeye pekeyake.” Jana pia zilitoka taarifa zinazomhusu raia huyo wa Ivory Coast kutakiwa na mabingwa VPL na FA Cup Dar Young Africans.

Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9

Picha
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’. Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake. “Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu

MAJONZI NA VILIO VYATAWALA KUAGWA DADA WA BILIONEA MSUYA

Picha
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu Anathe Msuya Dada wa marehemu wakiaga mwili wa ndugu yao. M toto wa marehemu Anathe, Allan Kimario (aliyelala). Majonzi na huzuni vimetawala kwenye tukio la kuagwa kwa mwili wa mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa risasi mwaka 2013, Anathe  Simon Msuya ambaye yeye aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar, Mei 25 mwaka huu. Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za mwisho. Mtoto wa Anathe aliyetajwa kwa jina la Alan Kimario (4) alionekana akilazimishwa kwenda kuuaga mwili wa mama yake kwani alikuwa akitaka aachwe aendelee na michezo yake kutokana na ukweli kwamba, alikuwa hajui hata kinachoendelea. Mwili wa marehemu Anathe umesafirishwa kwenda Mererani jijini...

Symbion Yaionya TANESCO.....Yasema Maneno ya Kizushi na Ukiukwaji wa Mkataba Wanaoufanya Utaligharimu Taifa

Picha
Kampuni ya kufua umeme ya Symbion imesema maneno ya uzushi na ukiukwaji wa mikataba unaofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) utaligharimu Taifa na kulitaka shirika hilo kusema ukweli kuhusu makubaliano yao. Kampuni hiyo pia imeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka jana, kigogo mmoja wa Tanesco (ametajwa jina lakini tunalilisitiri jina lake kwa sababu hakupatikana jana) alisaini mkataba na Symbion wa kuliuzia umeme shirika hilo la umma kwa miaka 15. Taarifa iliyoletwa jana kwa vyombo vya habari na mshauri wa Symbion, Julius Foster inaeleza kuwa taarifa zote zinazotolewa na Tanesco kuhusu uhusiano wao wa kimkataba ni za uongo na zimewashtua kwa kuwa shirika hilo la Serikali halijawahi kuieleza Symbion kuhusu tuhuma hizo. “Kama itatokea suala hili likaleta mgogoro wa kitaifa, tunataka Tanesco na Serikali na yeyote yule kufafanua masuala haya kwa kiapo na mbele ya mahakimu na tutaujulisha umma kila kitu,”  inasema taarifa hiyo. “Zaidi ya barua ambayo walitaka k...

Diwani wa Mtibwa Ashikiliwa kwa Tuhuma za Ubakaji

Picha
Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14, mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni. Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 29 saa 12 jioni kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sultan, Manispaa ya Morogoro. Matei alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo, kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo, hivyo askari walifuatilia nyendo zake na kumkamata. Alisema askari baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108. Alisema uchunguzi wa kitabibu unaendelea kuthibitisha tuhuma hizo. Akizungumza kwa simu, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhan alithibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu ni kwa tuhuma gani. Ramadhan alisema kwa sasa wao kama viongozi wa chama w...

Mwalimu Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumkuwadia Mwanafunzi Wake

Picha
Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo. Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo. Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono. Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita. “Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alin...

China Wammwagia Sifa Rais Magufuli....Wasema Kaipaisha Tanzania Kimataifa

Picha
SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania inasifika duniani. Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida. Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu bure.  “Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,”  alifafanua. Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli. “Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena...

Maalim Seif Kikaangoni LEO.....Polisi Wamtaka Aripoti Makao Makuu ya Polisi Kwa Ajili ya Kuhojiwa

Picha
Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa. Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi. Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika majimbo ya Unguja. “Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,”  alisema Bimani  Bimani aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita. Barua hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa  na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34 kwenda kwa...

Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa

Picha
Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne. Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January. Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya…… ’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’ ’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao y...

MKE WA TRAFIKI ADAWA KUKIRI KUMUUWA MUMEWE

Picha
MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani. Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo. Anayetuhumiwa kuua mumewe Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori amekiri kuhusika. Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliam...

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Tunus Mgaya Aliyesimamishwa Kazi na Waziri wa Elimu Afunguka Mambo Mazito

Picha
ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa. Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao. “Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi. Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na lina...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 31

Picha