Machapisho

Rais Magufuli apeleka kilio kwa Mbunge Joshua Nassari

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari huenda bado hajaelewa nini kielikumba jimbo hilo baada ya Diwani wa Kata ya Muriet, Credo Kifukwe kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichosema kuwa anamuunga mkono Rais Dkt Magufuli. Diwani huyo wa CHADEMA ambaye ni watano kujiuzulu katika jimbo hilo, alisema jana wakati akitangaza uamuzi huo kuwa, ameridhishwa na utendaji kazi wa kiongozi huyo wa nchi na kwamba kazi anayoifanya ni nzuri na inatakiwa kuungwa mkono na watu wote. Aidha, Kifukwe alisema kuwa, hana mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa, na kwamba anataka kufanyakazi zake binafsi kwani siku zote amekuwa msema kweli akipigania maendeleo ya wananchi wake. Muda mfupi baada wa diwani huyo kujiuzulu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kuwa kiongozi huyo na wengine wote wamekuwa wakinunuliwa na CCM katika mkakati wake wa kuidhoofisha CHADEMA, na kwamba wao hawawezi kumzuia kiongozi aliyeamua kununuliw...

Hili lingine la Rayvanny na BASATA Kuhusu Mapokezi na Tuzo ya BET

Picha
Siku moja baada ya mwimbaji Rayvanny kuwasili Bongo na kukutana na mapokezi makubwa Airport DSM akiwa na tuzo yake ya BET akiwa msanii kwanza wa Bongofleva kutwaa tuzo hiyo…story gumzo ni kuhusu kutooneakana mwakilishi wa BASATA Airport. 255 ya XXL ya Clouds FM leo June 29, 2017 imempata Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ambaye ameelezea sababu za kutoonekana mwakilishi wa Baraza hilo akisema kulikuwa na mawasiliano finyu kati ya Rayvanny na BASATA wakati anakwenda na kurudi kuchukua tuzo hiyo.  “ Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima. “Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee.”  ...

CCM na Edward Lowassa katika mvutano mwingine

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepinga vikali kauli iliyotolewa na mwanasiasa mkongwe hapa nchini kuhusu Masheikh wa Uamsho kikisema kuwa kauli hiyo ni ya kidi ni na kichochezi. Chama hicho kimeitaka serikali kutofumbia macho watu wa hivyo na kwamba endapo watathibitisha kuwa kauli hiyo haikuwa na mrengo mzuri katika jamii, wasisite kumchukulia hatua mhusika mkuu. Akizungumza leo na waandishi wa habari, Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  alisema chama hicho kinalaani kauli iliyotolewa na Lowassa katika futari aliyokuwa amealikwa. Katika futari hiyo, Lowassa aliwataka waislamu nchini kutokuwa wa baridi wakaishia tu kuongea badala yake watafute lugha nyingine ambayo wakizungumza serikali itaielewa ili viongozi wa dini hiyo wanaoshikiliwa kwa miaka minne sasa waweze kuachiwa. Kufuatia kauli hiyo ambayo Polisi walisema kuwa ni ya kichochezi, Lowassa aliitwa na tayari kuhojiwa na Polisi siku ya Jumanne na alitakiwa kurudi tena leo. Alipokwenda leo mahojian...

Picha 5: Stars imefuzu robo fainali COSAFA 2017

Picha
Taifa Stars imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Cosafa 2017 licha ya kupata sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Mauritius kwenye mechi ya mwisho ya Kundi A mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Moruleng Stadium Afrika Kusini. Stars imemaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Kundi A ikiwa na pointi tano sawa na Angola (ambao walilazimishwa sare ya 0-0 na Malawi kwenye uwanja wa Royal Bafokeng) lakini Tanzania inasonga mbele kwa faida ya wastani wa magoli.

Kutana na Jambazi Aliyeiba Fedha Kwenye Banks 50 Kwa Ustadi wa Hali ya Juu zaidi Duniani

Picha
Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17. Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber) Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'! Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 nda...

Taarifa Muhmu Toka Ofisi ya Makamu wa Rais

Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amewaagiza wapelelezi na waendesha mashtaka nchini waepukane na vitendo vya rushwa bali wafanye kazi kwa bidii kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele kwa kuchukua hatua stahiki kwa watu wanaoiba rasilimali za Taifa. Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati anazindua mwongozo kwa wapelelezi na waendesha mashtaka wa kesi za wanyamapori na misitu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais amesema mwongozo aliouzindua utasaidia kwa kiwango kikubwa uboreshwaji wa upelelezi na uendeshaji wa kesi zinazohusu wanyapori na misitu nchini. “Uwepo wa mwongozo huu ni dhahiri unategemewa kutoa matokeo chanya katika mapambano dhidi ya ujangili na uharibifu wa misitu yetu,”  amesisitiza Makamu wa Rais. Makamu wa Rais amesema kuwa ana imani mwongozo huo aliouzindua utasaidia kukomesha vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikiisababishia Serikali hasara kubwa ikiwemo u...

Rais Mgufuli Akutana na Wataalam Wa Umeme Ehiopia .......Wazungumzia Uzalishaji wa Megawati 2, 100 za Umeme katika Maporomoko ya mto Rufiji

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  jana  tarehe 28 Juni, 2017 amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tanzania. Mhe. Rais Magufuli alisema timu hiyo inayoongozwa na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele imekuja nchini kubadilishana uzoefu na timu ya wataalamu wa Tanzania ambayo inasimamia utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project). Katika mazungumzo na timu hiyo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli alielezea nia yake ya kuhakikisha mawazo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka maporomoko ya mto Rufiji, yanatekelezwa haraka iwezekanavyo. “Sasa hivi nchi yetu inazalisha megawatts 1,...