SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 3 Juni 2016

T media news

DIEGO SIMEONE, MACHO YANAUMIA KWA KUKOSA MZIMU WA BILL SHANKLY

Na Brian Marian Mrope (Gascoigne Brian)

Kila mwanadamu katika hii dunia anakuwa na bahati yake katika maisha. Wapo wachache ambao bahati huwa ya kwao maradufu. Nilitamani kumshuhudia Bill Shankly katika kizazi chake, ila ukuaji wangu ulichelewa kuletwa katika uso wa dunia hii. Hivyo nikakosa fursa ya kufahamu mambo mengi yaliyomhusu huyu
mwanadamu Bill Shankly.

Kutokana na ukuaji wa hii teknolojia, nimeweza kujua ubora wake ulioambatana na bahati katika maisha
yake. Diego Simeone najua macho yanauma kwakukosa kombe hili, ila wakati utakapofika nenda kaisikie hata harufu tu ya huyu Bill Shankly, katika kaburi lake huenda akakuachia kitu juu ya michuano hii ya Ulaya.

Nimemwangalia Torres yale machozi aliyokuwa ameyatoa usiku ule pale San Siro. Unafikiri yalikuwa
machozi ya usoni, hapana yale yalikuwa machozi halisi katika mboni ya macho yake. Nani asiyependa kuvaa medali ya ubingwa akiwa katika klabu yake ya damu?, machozi yake yalikuwa ni ya jasho na damu pale San Siro.

Hawa Real Madrid watakuwa na kitu katika michuano hii, fainali zao tano za mwisho wamefanikiwa kuchukua zote. Simeone ubora wa watu hawa umeambatana na utimamu wa kivuli cha Billy Shanky. Unashindwaje kuwakamata Real Madrid wakati Ronaldo wa sindano za ganzi, Bale akibanwa na misuli katika
zile dakika 120 za nyongeza, Benzema nafikiri skendo yake ile ya ngono bado inamwandama, ki-utimamu Real Madrid walikuwa nusu uwanjani ila kwakua kivuli cha Bill kipo nyuma yao bado waliweza kufanya kitu.

Kwa ubora wa vikosi AT. Madrid walikuwa bora zaidi ya Real Madrid upepo wa kivuli hakikuwa nyuma yenu. Umemwona Zidane tayari ameshaingia katika ukurasa mwingine katika vitabu vya kumbukumbu, nuru yake kutoka gizani mpaka sasa kuwa karibu katika uso wa dunia. Muda umekubali kuwa karibu katika mahesabu yake ndiyo maana hata alichofanya pale San Siro bado kiliweza kuwa sawa katika mfumo wake wa ubongo.

Diego Simeone (El Cholo) wakati mwingine jaribu kukimbizana na dakika wacha muda upite, bado naiona kasi ya ubongo wako haiendani na kasi ya michuano hii. Umemwona Zidane ameamua kukimbizana na dakika  maana humfikisha haraka safari yake.

Ganda ulilokanyaga sasa sidhani kama wakati mwingine utakuja kulikanyaga tena maana kwa utimamu wa mishipa yako ya fahamu bado imani yangu inaniambia tu kuwa utakwenda zako katikati ya kaburi la Bill Shankly na kuzungumza kitu juu ya kivuli chako. Hata mimi pia macho yanauma kwa kushindwa kuchukua
kombe hili pale San Siro moja kati ya maeneo ya ndoto zako Diego Simeone.

Wacha masikio yangu niyategeshe katika michuano ya Euro walau unaweza ukaleta watu watakaokubali
kuongozana na wewe katika vita ya ushindi. Inabidi moyo wa mwanadamu uweze fanya kazi vizuri ili mzunguko wa ufahamu wake uweze fanya kazi vizuri.

DIEGO SIMEONE NAJUA MACHO YANAUMA KWA KUKOSA MZIMU WA BILL SHANKLY.