Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2016

Benki Zaanza Kuwakamua Watanzania kwa Kuongeza kodi (VAT) ya 18%

Picha
Ukifanya muamala wowote wa kutoa pesa benki kuna makato mfano kwa CRDB ni 2,200. Maana ya hii kodi ni kuwa sasa utakatwa TZS 2,596. Vile vile ukifanya malipo kwa njia ya TISS makato yalikuwa ni TZS 10,000; kwa sasa utakatwa TZS 11,800. TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA NCHI YETU

CHID Benz Afunguka ya Moyoni..'Dawa za Kulevya Sitaki Hata Kuzisikia Zimeniumiza Sana na Kunidhalilisha Sana'

Picha
“Dawa za kulevya kwangu zinabaki kuwa historia, sitaki hata kuzisikia zimeniumiza sana kimawazo, zimenidhalilisha na zimepoteza mwelekeo wa maisha yangu, sina hamu nazo tena nina hasira nazo siwezi kuzirudia kwa sasa naangalia maisha yangu mapya katika muziki,” - Chid Benz. 8

FURAHA YA DC MPYA ILIPOGEUKA KUWA MAJONZI NDANI YA IKULU SOMA SABABU HAPA LIVE!!

Picha
😷 FURAHA YA DC YAGEUKA MAJONZI IKULU Emile Yotham Ntakamulenga akitoka katika Ukumbi wa Ikulu, Dar es Salaam jana baada ya kubainika kuwa aliteuliwa kimakosa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.

MKE WA ZAMANI WA MUNGE WA CHADEMA SUGU AMCHANA BABA WATOTO WAKE LIVE KUHUSU KUFUNGIWA BUNGE HAPA LIVE!!

Picha
Mbunge wa Chadema Sugu ambaye amefungiwa kutohudhuria vikao 10 vya Bunge baada ya kufanya mambo ya kihuni bungeni, Chini akiwa na mke wake zamani na mtoto wao na mke wake Faiza akimchana live chini. Faiza Ally · "Huyu nae bwana, mi nilifikiri usela mavi unaleta kwa mtoto tu kumbe hadi bungeni unapeleka usela, asa dole la kati ndio nini  😆 😂 😂 😂 😂 😂  ona sasa hadi ume simamishwa vikao"

MBUNGE WA UKAWA AZIDI KUOZA RUMANDE SOMA HAPA LIVE!!

Picha
Mbunge wa Chadema na Mwanasheria pia wa chama hicho Tundu Lissu, bado anasota Rumande kuhusiana na kitendo chake cha kumshambulia Rais wa Jamhuri juzi. Stay tuned kwa habari zaidi.

Magufuli: Kuna Mtu Alikuwa Anahamisha Kati ya Tsh milioni 7-8 kila dakika. Yuko Mikono Salama...

Picha
Jana Mtukufu wa nchi mkuu sana Rais Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya kula kiapo cha uadilifu alitamka ''Tulikuwa tunafuatilia kwenye revenue, yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha'' Kauli hii imeniacha njia panda, kwamba huyu mtu - Alipata wapi ujasiri wa kuhamisha kiashi hicho cha fedha kila baada ya dakika moja? - Hizo fedha zilikuwa kwa wema au ubaya? - Huyo mtu ni nani mpaka asitajwe wananchi wakamjua? - Yuko mikono salama, Hiyo mikono salama ni ipi kwa mtu wa namna hii? - Watazirudisha vipi pesa zote alizohamisha? - Amekuwa akihamisha pesa kwa muda gani na mpaka anawekwa mikono salama alikuwa kashachukua kiasi gani? - Atapelekwa mahakama ya uhujumu/mafisadi? By Chachu Ombara/JF

Fella: Mwanamuziki Ruby Ana ‘stress’ Ndio Maana Hajaonekana Kwenye Video Yamoto Band

Picha
Ruby alikuwa ana ‘stress’ ndio maana alishindwa kutokea kwenye video ya wimbo SU wa Yamoto Band alioshirikishwa. Meneja wa kundi hilo, Said Fella amekiambia kipindi cha E News cha EATV kuwa hiyo ndio sababu aliyokuwa akipewa na Ruby. Amedai kuwa baada ya kuona kuwa Ruby amekuwa akitoa sababu hiyo kwa muda na hawakutaka asishiriki akiwa hana mood, walilazimika kuifanya bila yeye. Kwenye video hiyo anaonekana msichana mwingine akiimba sehemu ya Ruby. Haijafahamika mara moja ni mambo gani yanamsibu muimbaji huyo kiasi cha kumpa msongo wa mawazo lakini kwa wanaofahamu, stress ni kitu kinachoweza kukuondelea mood ya kufanya vitu vingi. Bongo5

Je, Tundu Lissu Anajijenga ili Kugombea Urais 2020?

Picha
Hii ni kama strategy ya ukawa kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo. Kauli na matendo ya Lisu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo. Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani ukawa kama Lowasa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawisi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020. Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye. Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lisu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni. Je huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?

Henry Kilewo ' Hakuna Haja ya Onesmo Nangole Kukata Rufaa ya Kuenguliwa Ubunge, Twendeni Longido Tukawakimbize CCM Mpaka Watajuta'

Picha
Mungu ampe ujasiri mzee wetu Onesmo Nangole wala asihangaike na Rufaa, twende na hawa magamba tukawaambie namna ambayo Umma unawachukia kwasasa... Tutawapeleka mpaka mtajuta kushiriki uchaguzi.... Mtakuwa wepesi kuliko ile pamba... Yaani nyie maccm tukikutana huko mtaomba uchaguzi uishe ili mkimbie aibu... Ni huzuni kwa mzee wetu kuenguliwa ila itakuwa somo sahihi kuiambie ccm namna ambavyo Hawapo na UMMA tena.... Twendeni Longindo...... By Henry Kilewo

POLISI YAUWA MAJAMBAZI MATATU YALIYOKUWA YAMEJIFICHA KATIKA MAPANGO YA AMBONI

Picha
POLISI mkoani Tanga imewaua watu watatu katika mapigano ya risasi wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya watu jijini humo wakiwamo watu wanane waliochinjwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima.Limewahakikishia wananchi kwamba eneo la Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto yanayodaiwa kutumiwa na wahalifu waliosababisha mauaji hasa ya wakazi wanane wa Kibatini lipo salama, baada ya watuhumiwa wengine watatu na silaha mbalimbali kukamatwa juzi. Waliokamatwa ni Abdulkarim Singano, Seif Jumanne na Ramadhani Mohamed ambao baadaye walikufa kutokana na majeraha ya risasi wakati wa mapigano katika msitu wa Kibatini wakati askari wakijaribu kuwadhibiti, siku moja baada ya Abuu Seif anayedaiwa kuwa kiongozi wao kuuawa jijini Dar es Salaam. Silaha zilizokamatwa ni bunduki mbili aina ya SMG, bastola moja, risasi 30, mapanga, majambia ambavyo vimepatikana kupitia msako ulioshirikisha kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama vilivyohusisha askari kutoka majeshi yote. Kamanda wa Polisi ...

SAKATA LA CLOUDS TV KUMHOJI SHOGA MAPYA YAIBUKA,WABUNGE WAISHUKIA VIKALI,WATAKA CLOUDS IADHIBIWE,

Picha
WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja.  Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga.  “Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo.  Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia ki...

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Saba

Picha
Mtunzi:  Enea Faidy Ilipoishia sehemu ya  Sita ( kama hukuisoma bofya hapa). .....DOREEN alimkubalia Eddy kuwa mpenzi wake lakini alimweleza kuwa kuna sharti ambalo Eddy lazima alifuate ndipo awe nae.Dorice hakutaka kukubali kirahisi kumwachia Doreen kuwa na Eddy hivyo alipanga kulipiza ili Doreen asije kumsahau.Mwalimu John alipigwa na mkewe mpaka akapoteza fahamu ambapo mkewe alichanganyikiwa sana baada ya kumwamsha bila mafanikio.... Endelea..... ...MWALIMU JOHN alikuwa kimya pale kitini akiwa hana fahamu yoyote, mkewe akazidi kuchanganyikiwa sana kwani alihisi tayari mumewe ameaga dunia. "Jamani mume wangu amka bado nakupenda! Nisamehe Mimi John wangu!" Alizidi kulia mke wa mwalimu John kwa huzuni na majuto makali. Alijiona mjinga sana kwa kujichukulia maamuzi mkononi bila hata kumdadisi vizuri. Simanzi ilimtanda mwanamke yule bila kujua la kufanya, machozi yalichuruzika kama mito miwili usoni kwake kwani ndio kwanza ndoa yao ilikuwa changa kabisa tangu waoane mie...

SERENGETI BOYS NDANI YA ‘PIPA’ KUSAKA USHINDI MWINGINE

Picha
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea Seychelles kwa ajili ya mchezo wao wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Julai 2. Kikosi cha Serengeti Boys kinatarajiwa kuwasili Seychelles majira ya saa 9 alasiri huku mchezo wao ukitarajiwa kuchezwa saa 10:00  kwa saa huko. Kwenye mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa taifa, Serengeti Boys walipata ushindi wa magoli 3-0 hivyo wanahitaji ushindi au sare yeyote ili kufuzu kwa raundi inayofuata.

RAIS MAGUFULI AMTANIA HIVI GODWIN GONDWE ALIPOWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA

Picha
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya 139 na wakuu wa mikoa wanne kwenye hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli akiwa na baadhi ya wakuu wa wilaya kwenye picha ya pamoja Ikulu Jumatano hiiMiongoni mwa wakuu wa wilaya wapya ni mtangazaji nguli wa redio na TV, Godwin Gondwe. Gongwe sasa ni mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Akiongea kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli anayefahamika kwa utani mwingine alimsifia Gondwe kuwa ni mtangazaji mzuri na kumtaka atumie uwezo huo kutangaza maendeleo. “Gondwe najua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu,” alisema. Godwin Gondwe kama anavyojulikana pia alikuwa mtangazaji maarufu wa habari kwenye kituo cha runinga cha ITV. Amewahi pia kufanya kazi kwenye vituo vya redio vya Radio Free Africa na Radio One. Lakini pia alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 30, Ikiwemo ya Magufuli Kamnasa Mwizi wa Mil 7 Kila Dakika

Picha
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 30, Ikiwemo ya Magufuli Kamnasa Mwizi wa Mil 7 Kila Dakika