Machapisho

TRUMP AKUMBANA NA UPINZANI WA KIMATAIFA KUHUSU MLANGO WA HORMUZ

Picha
  Rais  wa Marekani, Donald Trump, amejikuta akikabiliwa na upinzani kutoka kwa mataifa mbalimbali duniani kufuatia wito wake wa kuundwa kwa muungano wa kimataifa wa kulinda usafirishaji wa meli katika Mlango wa Hormuz. Njia hiyo muhimu ya bahari ni kiungo kikubwa cha usafirishaji wa mafuta duniani, hivyo mvutano wowote katika eneo hilo huathiri uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa. Katika majibu yaliyotolewa, nchi kadhaa zilionesha tahadhari na kusisitiza kuwa haziko tayari kujiingiza moja kwa moja katika mgogoro huo. Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alisema kuwa nchi yake inashirikiana na washirika wake kutafuta suluhisho la kidiplomasia la kuhakikisha usalama wa Mlango wa Hormuz, lakini akaweka wazi kuwa haitakuwa operesheni ya NATO. Kwa upande wa Ujerumani, Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius alikataa wazi kushiriki katika mpango huo, akisema kuwa mgogoro huo hauhusiani na nchi yao. Kauli hiyo inaonesha msimamo wa baadhi ya mataifa ya Ulaya ya kuepuka kuingia katika mivut...

UKUMBUSHO WA LEO

Picha
  Ipo Siku Nitakufa na Mimi Ewe ndugu yangu, Mara nyingi tunasikia habari za vifo vya watu wengine. Tunasema: “Fulani amefariki.” Lakini mara chache tunakumbuka kuwa: Ipo siku nitakufa na mimi. Siku hiyo itafika bila kuchelewa wala kuwahi. Siku ambayo jina lako litasemwa: “Fulani amefariki.” Utaachana na nyumba yako, utaachana na mali yako, utaachana na marafiki zako. Na utabaki na kitu kimoja tu  matendo yako. Allah Anasema katika Qur’an kuwa kila nafsi itaonja mauti. Hivyo kabla siku hiyo haijafika: 🌿 Tubu madhambi yako. 🌿 Linda Swala zako. 🌿 Soma Qur’an mara nyingi. 🌿 Fanya mema kwa watu. Kwa sababu siku moja utalala usingizi ambao hautakuwa na kuamka tena duniani. Lakini utakuja kuamka katika siku ya hesabu. 🤲 Dua “Ewe Allah, tujalie mwisho mwema katika maisha yetu. Utujalie tukutane na Wewe tukiwa katika hali ya imani na utiifu. Ufanye kaburi letu liwe bustani katika bustani za Peponi. Aamiin.”

Hukumu ya Talaka Kutokana na Kukosa Kizazi Katika Ndoa ya Kiislamu

Picha
  Assalamu a’laykum warahmatullahi wabarakatuh. Swali ambalo mara nyingi huulizwa katika jamii ni kuhusu hukumu ya mume kumpa talaka mke wake kwa sababu ya kukosa kupata watoto kwa muda mrefu. Wengine hujiuliza ikiwa inaruhusiwa katika Uislamu au la, hasa pale ambapo wanandoa wameishi pamoja kwa miaka mingi bila kupata kizazi. Kwa mujibu wa wanazuoni wengi wa Kiislamu, kukosa kupata watoto kwa muda mrefu kunaweza kuwa sababu inayoweza kupelekea wanandoa kuachana ikiwa hali hiyo inaleta matatizo makubwa katika ndoa. Hata hivyo, Uislamu hauhimizi talaka kuwa suluhisho la haraka. Talaka ni jambo linaloruhusiwa, lakini ni bora lichukuliwe kama hatua ya mwisho baada ya jitihada nyingine zote kushindikana. Katika Uislamu, moja ya malengo muhimu ya ndoa ni kuendeleza kizazi. Ndiyo maana wanandoa wengi hutamani kupata watoto ili kuendeleza familia na jamii. Hata hivyo, kupata mtoto si jambo ambalo mwanadamu analidhibiti moja kwa moja, bali ni riziki inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Ndiyo maan...

USIACHE ASILI MAFANIKIO YAKO MIKONONI KWAKO!

Picha
  Iliki & Pilipili Manga Ni miongoni mwa mazao ya Asili yana faida lukuki kama tiba ya kimwili na kiroho.Yanafungua vifungo.. Ndio maana ukifungua jioni mwezi wa ramadhani upate uji au chai ya pilpil manga au iliki inafungua vifungo na tiba ya mwili hata vidonda tumbo. 💥NGUVU ZA KIROHO Kuvutia wateja na bahati katika eneo lako la biashara. Tumia iliki na pilipili manga ya unga kupigia deki na kupulizia ndani ya eneo lako la biashara yako kila siku kabla hujaanza kufanya biashara. Huondoa nguvu za giza kuleta nuru ya mwangaza wa mafanikio. Pia unaweza kutumia iliki na pilipili manga ya unga siku ya jumatatu usiku wa 6 kumwaga unga wake ndani ya eneo lako la biashara na kusubiri baada ya lisaa limoja au zaidi ukafagia kwa kutoa njee na mabaki hayo ya iliki na pilipili manga uliyofagia ukayafukia njee mbele ya eneo lako la biashara. 💥MVUTO WA MAPENZI/BIASHARA Kwa, kutumia iliki na pilipili manga ya punje. Unaweza kuvutia unavyohitaji kwa kuvichoma kwa pamoja kwa manuizi mfano ka...

KAMPUNI YA CHINA YADAI KUKAMATA MAWIMBI YA NDEGE ZA KIVITA ZA MAREKANI

Picha
  Kampuni binafsi ya teknolojia na ulinzi kutoka China inayojulikana kama Jingan Technology imedai kuwa imefanikiwa kukamata mawimbi ya redio kutoka kwa ndege za kivita za Marekani aina ya Northrop B‑2 Spirit wakati wa operesheni ya kijeshi iliyofanyika nchini Iran tarehe 1 Machi. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kampuni hiyo, mfumo wao wa kisasa wa ujasusi unaotumia akili bandia (AI) unaoitwa “Jingqi” uliweza kugundua na kuchambua mawimbi ya mawasiliano yanayohusishwa na ndege hizo za kivita wakati zilipokuwa zikirejea katika kambi zao baada ya kukamilisha misheni ya kijeshi. Mfumo huo unadaiwa kutumia mchanganyiko wa teknolojia za kisasa kama uchambuzi wa data kubwa, picha za satelaiti pamoja na taarifa za ndege zinazopatikana hadharani ili kufuatilia shughuli za kijeshi. Ripoti zinaeleza kuwa mfumo huo uliweza kuchambua vipande mbalimbali vya taarifa kama vile picha za satelaiti, njia za safari za ndege na rekodi za anga ili kuunda taswira kamili ya operesheni iliyohusisha ...

FAIDA KATIKA KUIENDEA SWALA

Picha
  ➡ *Hukmu ya kuswali huku ukijizuwia moja ya Haja mbili ima kubwa au ndogo* 🍃♦️▫️الٳمـام العـلامـة ابـن بـاز رحمــه اللـہ وغـفــر لـه : 🍃♦️▫️ الســــــــــــــؤال : swali : 🍃♦️▫️ أصلي وأنا أدافع الريح أحيانا، فهل صلاتي صحيحة؟ Ninaswali huku nikiwa najizuwia na kutokwa na upepo baadhi ya nyakati je swala yangu sahihi ? 🍃♦️▫️الجـــــــــــــواب : Jibu : 🍃♦️▫️ الواجب على المؤمن إذا شُغِل بالريح أو البول أو الغائط شغلًا يؤذي أنه لا يدخل الصلاة lililo la wajibu kwa muumin anapo shughulishwa na upepo au haja ndogo au haja kubwa mshughuliko  ambao unampa dhiki hakika haifai kuingia katika swala   🍃♦️▫️بل يقضي حاجته من غائط وبول وريح ثم يتوضأ ويصلي وهو خاشع القلب والجوارح مقبل على صلاته، *Bali inampasa akidhi Haja yake ima haja kubwa au haja ndogo au upepo kisha atawadhe na aingie katika swala akiwa mwenye utulivu wa moyo na viungo akiikabili swala yake* 🍃♦️▫️ هذا هو الذي ينبغي لكل مؤمن ومؤمنة لقول النبي صلى الله عليه وسلم:  hii ndio inampasa kila muislam wa kik...

NAMNA YA GHUSL (KUOGA) JANABA

Picha
  Kuoga Ghusl (Janaba) ni kuoga kwa ajili ya kujitwaharisha baada ya janaba ili mtu aweze kuswali na kufanya ibada nyingine. Hatua za Kuoga Ghusl 1. Kuweka nia Unanuia moyoni kuoga ili kujitwaharisha na janaba kwa ajili ya Allah. 2. Kusema Bismillah Ni vizuri kuanza kwa kusema: Bismillah. 3. Kuosha mikono Osha mikono yako mara tatu. 4. Kuosha sehemu za siri Osha sehemu za siri na uondoe uchafu wowote uliopo. 5. Kutawadha udhu kama wa swala Tawadha kama unavyotawadha kwa ajili ya swala (unaweza kuacha kuosha miguu mpaka mwisho). 6. Kumimina maji kichwani Mimina maji kichwani mara tatu na hakikisha maji yanafika kwenye ngozi ya kichwa na mizizi ya nywele. 7. Kuosha mwili wote Osha mwili wote ukianza upande wa kulia kisha kushoto, na hakikisha maji yanafika sehemu zote za mwili. 8. Kuosha miguu Ikiwa hukuosha miguu wakati wa udhu, basi ioshe mwisho wa kuoga. 📃Dalili kutoka Sunnah Aisha (RA) amesema: “Mtume ﷺ alipokuwa akioga janaba, alianza kwa kuosha mikono yake, kisha akatawadha ka...