Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema licha ya kituo cha Redio Times kuomba radhi katika kipindi cha mahojiano kati yake na msanii Diamond, hatua ya kufika mbele ya kamati ya maudhui kwa ajili ya kuhojiwa ipo pale pale. Hayo yamesemwa leo Machi 29 na Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji wa mamlaka hiyo, Andrew Kisaka, alipohojiwa na MCL Digital, na kutakiwa kueleza kama uombaji wa radhi wa kituo hicho ndio salama yao ya kutoitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua. Katika maelezo yake, Kisaka amefafanua kwamba suala la kituo cha Redio au Televisheni kinapokosea ni lazima uongozi wake ufike mbele ya kamati hiyo na kuongeza kuwa hiyo ni sheria hivyo huwezi kuikwepa. Amesema sheria hiyo inabaki palepale hata kama itatokea uongozi huo, ukaomba radhi kwa kupitia njia nyingine kama hiyo waliyoifanya times. Sakata la Diamond, Times FM waomba radhi Akielezea kuhusu adhabu inayotolewa kwa kituo ambacho kimekosea, amesema ni pamoja na kupigwa faini au kufun...