Machapisho

Hizi Hapa Sababu za Wanaume Wengi Kutokuoa Siku Hizi..!!!

Picha
Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki. Kwa nini hali hiyo hutokea?  Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:  1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano: Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na b...

Onyo kwa Bunge Dhidi ya Adhabu kwa Makonda...!!!

Picha
Ni hakika kwa100% Daud Albert Bashite alimaarufu Paul C. Makonda amekiri tuhuma zote mbele ya Kamati ya Bunge leo, Kinachosubiriwa ni maoni ya kamati hiyo kwenda kwenye Bunge ambapo taarifa na maoni hayo vitasomwa Bunge linaloanza wiki ijayo 04/04/2017. Mimi kama raia mwenye haki na wajibu kwa taifa langu, nikitambua haki yangu kwamba Bunge ni chombo changu cha uwakilishi, Natoa onyo kwa Kamati husika na Bunge pia, Ole wenu mje na hadithi ya kwamba MMEMSAMEHE. Narudia ole wenu, Ole wenu, ole wenu kabisa..... Sisi wananchi tuna kesi nzito sana na huyu mtu nje ya yeye kutudharau na kutudhihaki kupitia bunge letu ambalo nyinyi tumewatuma mtuwakilishe... Nataka mtambue kila mnachofanya hamfanyi kwaniaba yenu, bali kwaniaba yetu, Hivyo sisi tuliowatuma tayari tulishamhukumu na kufunga file lake. Ole wenu mbadilishe maamuzi ya umma, Sisi ndio wenye mamlaka ya mwisho katika nchi hii, sio rais, sio jaji, sio spika, bali sisi tukisema na kuamua mbinguni na duniani tumeamua.... Hii ni kwam...

Orodha Ya Majina Yaliyopitishwa Na Kamati Kuu CCM Kugombea Ubunge Afrika Mashariki

Picha
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge ujao. Akisoma majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo. Mchanganuo Miongoni mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani. Walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni; Wanawake Tanzania Bara;     Zainabu Rashid Mafaume Kawawa    Happiness Elias Lugiko    Fancy Haji Nkuhi    Happiness Ngoti Mgalula Wanaume Tanzania Bara;     Dkt Ngw...

Julius Mtatiro: Sophia Simba Anaweza Kumfukuza Kinana?

Picha
Na. Mtatiro J Sofia Simba na wale wenyeviti wa CCM waliofukuzwa na Halmashauri Kuu ya CCM hawawezi kuitisha kikao chochote ndani ya CCM ila wanaweza kuitisha Vyombo vya Habari na kuvieleza kuwa kikao chao kimemfukuza Kinana. Kama ingehusu CCM, tamko hilo moja feki la Sofia Simba na wenzake lingelitosha kuwapa kesi ya jinai hata isiyo na dhamana.  Lakini kwa CUF jambo hilo hilo linaleta maswali na hofu. Kwa ufupi, Baraza Kuu rasmi la CUF lilichaguliwa na Mkutano Mkuu mwaka 2014 na litakuwa madarakani hadi mwaka 2019 na ndilo lilimfukuza Lipumba uanachama mwezi Septemba mwaka 2016, na Baraza Kuu hilo hilo ndilo limekutana Zanzibar wiki moja iliyopita kwa mahudhurio ya asilimia 81 ya wajumbe wote na likafanya maamuzi mbalimbali ya chama.  Baadaye Lipumba (aliyekwishafukuzwa uanachama) naye akaita kundi la watu wanaomuunga mkono (wanachama wa kawaida) pamoja na Wajumbe wa Baraza halali wasiozidi watano eti akadai hicho ni kikao cha Baraza Kuu la CUF. Akaenda mbele zaidi akaita...

Zitto: Tumejulishwa na NECTA Hakuna Rekodi za Daud Albert Batishe Wala Paul Makonda...!!!!

Picha
Tumejulishwa Kwenye Kamati Kuwa Nacte Hawana Rekodi ya Albert Bashite Wala Paul Makonda..Yani Wote Hawapo kwenye Taarifa za NECTA

Makonda: Zitto Amenisaidia Sana Kuelewa Siasa..!!!!

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paul Makonda akiwa kwenye interview amesema Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT) ndiye Mbunge anayemsaidia kuelewa siasa. Afafanua kuwa, Zitto anajua kujenga hoja za kuiyumbisha serikali hasa kwenye kusimamia mambo mbalimbali yenye maslahi ya kitaifa.

Fahamu njia bora ya kutumia likizo yako ya kazi

Zaidi ya nusu ya wafanyakazi wengi huwa hawatumii muda wao wote wa likizo, na huwa wanakosa vingi zaidi ya furaha na kupumzika. Utafiti uanonyesha kuwa kupata muda wa kupumzika kuna faida kiafya. kupumzika mara kwa mara hukusaidia kupunguza mawazo, kupunguza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo, kuongeza ufanisi kazini na vilevile hukufanya kuwa karibu na familia yako. Unawajua wasiosumbuka kutumia muda wao mwingi kutalii? Familia ya Kardashians inajulikana sana duniani kwa safari zao za kifahari katika maeneo tofauti tofauti ulimwenguni. Huwa wanatumia gharama kubwa sana katika matembezi yao kama kukodisha jumba la ghorofa lililokombele ya ufukwe wa bahari huko Costa Rica kwa gharama ya dola za kimarekani 17000 na magari ya kifahari kama Rolls Royce Itazame video hii na ujifunze mengi kuwahusu Kim, Khoe na kundi lao wanavyotumia muda mwingi wakiwa mbali na nyumbani. Japo yawezekana huwezi kugharamia safari za likizo za gharama kama wao, ila kuona tu namna wanavyofurahia inaweza kukuv...