Machapisho

Updates: Watu 76 Wamethibitika Kufariki Dunia na 5 Kunusurika Katika Ajali ya Ndege

Picha
Watu 76 wamethibitika kufariki dunia na 5 kunusurika baada ya ndege ya wachezaji kutoka Brazil kuanguka asubuhi ya leo. Kati ya waliofariki 22 ni Waandishi wa Habari. Timu Atlético Nacional ambayo ilipaswa kucheza wa kwanza wa fainali dhidi ya timu ya Chapeonense yaomba Shirikisho la Soka barani Amerika Kusini(CONMEBOL) kukabidhi kombe kwa timu hiyo. Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Medellin Bwana Jose Maria Cordova amesema kuwa ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa katika ukanda huo, kwani kupitia Sattelite radi na mawingu mazito yalionekana katika anga.

Daktari Feki Afanya Upasuaji Wagonjwa 9 na Kufariki Mmoja, Apewa Ofa ya Kujiendeleza Kielimu

Picha
KENYA: Kamati ya maswala ya afya nchini Kenya imependekeza daktari feki aliyekamatwa nchini humo aruhusiwa kujiendeleza na masomo ya udaktari badala ya kutumikia kifungo gerezani. Kauli hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa daktari huyo feki alifanikiwa kufanya upasuaji kwa wagojwa tisa ambao kati ya yao wanane walipona na mmoja ambae alikuwa mjamzito ndiye aliyepoteza maisha huku akifanikiwa kumuokoa mtoto aliyekuwemo tumboni mwa mjamzito huyo.

Ratiba ya mechi za EFL zitakazo chezwa wiki hii

Picha
  Wiki hii tena timu zinazoshiriki ligi mbalimbali zinakutana kwenye ligi moja ya EFL CUP, itakayozikutanisha timu kadhaa za ligi mbalimbali. November 30 ya mwezi huu unazikutanisha timu nne zinazoshiriki ligi kuu ya England,na huwenda mambo yakawa safi kwa timu kubwa mbili kati Manchester na Arsenal. Orodha ya mechi zitakazo pigwa November 30 ya mwezi huu. Arsenal vs SouthamptonManchester united vs West harm United. Bongoswaggz  itakusogezea mechi hii na utaitazama hapa live hapo kesho mida ya saa 2 usiku

Zaidi ya asilimia 91 ya wanafunzi chuo cha Kampala wakosa mikopo.

Picha
Waziri wa elimu Prof Joyce Ndalichako ameombwa kuingilia kati sakata la wanafunzi wa chuo kuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam ambao zaidi ya asilimia 91 ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wamekosa mikopo huku wengi wao wakionekana kukata tamaa ya kuendelea na masomo yao baada ya kukosa mikopo. Ujumbe wa wanafunzi hao ukiongozwa na waziri wa elimu wa chuo hicho cha Kampala uliwasili katika kituo cha matangazo cha ITV Mikocheni Dar es Salaam majira ya mchana huku wengi wao wakionekana dhahili kukata tamaa kwa kile walichodai ni majibu yasiyoridhisha waliyojibiwa na maafisa wa bodi ya mikopo. Takwimu zinaonyesha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa 2016/17 katika chuo cha Kampala ni wanafunzi 1486, ambapo ni wanafunzi 135 pekee ndio waliokwisha kupata mikopo huku wanafunzi 1359 wakiwa hawajui nini cha kufanya ikiwa ni siku chache kabla ya wao kufanya mitihani yao.

Hii ndio sababu ya El Classico kutoonyeswa Live ndani ya England.

Picha
Habari zilitoka ni kwamba mechi pendwa ya El Classico haitaonekana Live kwenye Tv za England. Mechi hii itachezwa Dec 3 na kutokana  sheria za kurusha matangazo live siku hiyo inafanya mechi hii isiruke Live ndani ya England. Sheria zinasema kwamba hairuhusiwi mechi yoyote kurushwa live kati ya 2:45pm na 5:15pm kwa siku hiyo. zaidi ya nchi 100 watashuhudia mechi hii ambayo inawahusisha mastaa Ronaldo na Messi. Sky Sport wataonyesha full mechi lakini watachelewa muda kidogo tofauti na kama inavyotokea live duniani kote. Rais wa La Liga alisem, “Mechi haitaonyeshwa Live ndani ya England kutokana na katazo lililo kwenye kurusha mechi live kwa muda huo. Tulikua na nafasi tatu kwa ajili ya mechi hii ambayo ni 1pm,4:15pm na 6:30pm. Baada ya kuongea na washauri wetu wametuambia tucheze kucheza 6pm itakua imechelewa sana kwa Asia na 1pm itakua mapema sana kwa America.” “So tumechagua 4:15. Uchaguzi wa muda ni muhimu kwa kujali idadi kubwa ya watu watakao kuwa affected...

Christmas imekuja mapema kwa Arsenal

Picha
Zimebaki siku nyingi kidogo hadi sikukuu ya Christmas ifike lakini kwa upande wa Arsenal kama vile imekuja mapema kidogo. Kwa mashabiki wa Arsenal wanaweza kuwa wameiona hii picha ikimuonyesha manager wao na wachezaji Cazorla na Bellerin wakiwa kwenye muonekano wa Christmas. Picha hii na video zimetoka kwenye kurasa wa Arsenal ambapo hii ni kampeni ya kijamii ya Arsenal. Tangazo lenyewe linamuonyesha Wenger akiwa anajibu swali la mwandishi wa habari ambapo mwishoni video inawahamasisha mashabiki wa sign up kuchangia watoto. Arsenal wameanza msimu wa sikukuu vizuri baada ya kushinda magoli 3-1 dhidi ya Bournemouth. Ili kuendeleza msimu huu Arsenal foundation na Save the Children’s Christmas imekuja kwa wakati wa muafaka ikiwa ni jukumu lao la lazima kijamii. Enjoy kuangalia video

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO,PIGA MARUFUKU UUZWAJI WA SARE ZA MAJESHI KWA WATU BINAFSI

Picha
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016  Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pomb...