Machapisho

Jinsi ya kuhifadhi mboga za majani kama mchicha, maboga, matembele n.k.

Picha
Hatua 👇👇👇. 1. Chuma mboga zako zilizo tayari. 2. Zichambue kuondoa yasiyohitajika. 3. Safisha kwa maji. 4. Kisha tafuta mfuko mzuri wa kitambaa kisha funga mboga zako humo. 5. Chemsha maji hadi yachemke. 6. Weka mboga zako kwenye kitambaa kwenye hayo maji yaliyo jikoni yamechemka kwa dakika 5. 7. Zitoe kisha ziache zichuruzike maji. 8. Kaanike juani kwenye kichanja ila juu funika kwa kitambaa cheusi. 9. Ikikauka tafuta chombo kisichoingiza hewa ihifadhi vizuri, hakikisha haipati unyevu wa maji. 10. Mboga hiyo inaweza kudumu kwa miezi 6. Nawasilisha.

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI

Picha
MAHITAJI 1. Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01 2. Banda bora 3. Vyombo vya chakula na maji 4. Chakula bora 5. Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa 6. Chanzo cha nishati joto na mwanga 7. Elimu na ujuzi wa malezi bora 8. Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga 9. Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa) 10. Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu KUKU 10 Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa,Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi. Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapa...

TANGAZO:TAWFIQ MONEY SERVICE WAKALA WA KIBANK BUNDA

Picha
ANAPATIKANA BARABARA YA BOMANI MKABALA NA STENDI YA ZAMANI TUNATOA HUDUMA ZIFATAZO KWAJIA YA BANK: -KUFUNGUA AKAUNTI ZA CRDB,EQUITY ,POST  BANK. -KUWEKA PESA -KUTOA     PESA -KUTUMA  PESA -KULIPIA ADA ZA SHULE -KULIPIA MALIPO MBALIBALI YA SEREKALI. KUWEKA PESA NA KUTUMA NI BURE KABISA.  PIA TUNATOA HUDUMA ZA :- - BIMA ZA MAGARI - MOTOR VAHICLE PIA TUMEFUNGUA OFISI  NYINGINE NYASURA STENDI UPANDE WA GARI ZINAZO KWENDA MWANZA KARIBUNI KUPATA HUDUMA LUKU VING'AMUZI VYA TV SIMU NAMBA 0784699901,0756141420

MO aanza kutelekeza ahadi Simba

Picha
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kutangaza kumshukuru mlezi wake bwana Mohammed Dewji kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipia mishahara ya wachezaji,benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika kipindi chote cha mpito kuelekea mabadiliko ya kimuundo ya klabu. Mbali ya hayo mfanyabiashara huyo mkubwa barani Afrika atalipia kodi za nyasi bandia na gharama nyingine za uendeshaji wa klabu. Uongozi wa Simba unamshukuru sana MO,ukizingatia klabu kwa sasa haina mdhamini na unaamini uwekezaji huo ni chachu ya kuwarejeshea furaha wanasimba na hatimae kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya msimu huu na misimu mingi ijayo. Mwisho klabu inawaomba washabiki wake wajitokeze kwa wingi siku ya Jmosi ya Octoba Mosi pale uwanja wa Taifa,kuishangilia Timu yao itakapocheza mechi ya ligi dhidi ya Yanga. Tunaamini mechi hiyo ni mwendelezo wa furaha kwa wanachama na washabiki wetu kote nchini. Pia tuwaombe sana kukumbuka kununua ti...

Vigogo Yanga watua Pemba kupandisha morali

Picha
Vigogo wa Yanga Lameck Lukumay Thobias Lingalangala wametua Pemba kwa ajili ya kupandisha morali ya wachezaji wao kuelekea mchezo wa Jumamosi. Kwenda wa vigogo hao kunatokana na kamati ya mashindano ya Yanga iliowateua wawili hao kutua haraka Pemba kufatilia mazoezi ya timu, ari na morali ya vijana. Inaelezwa kutua kwao kumeambatana na kutoa kiasi cha pesa kisichopungua shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuwapa wachezaji motisha ya kufanya vizuri kabla ya ahadi kamili ambayo uongozi utaitoa kwa wachezaji wao katika kuifunga Simba. Viongozi hao wawili walionekana katika mazoezi ya timu hiyo ya leo jioni wakifatilia mazoezi ambapo kesho watarejea Dar kuleta ripoti juu ya morali ya kambi, ingawa taarifa za awali zinaonesha kwamba morali ya Yanga ipo juu kuelekea mchezo huo.

WATUMISHI WATATU WA SERIKALI NA MENEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA BUKOBA WAMEPANDISHWA KIZIMBANI

Picha
WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016. Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Amantus Msole,mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin Makonda,Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki yaCRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa. Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba no.0150225617300 Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitaki...

TBT: Picha za utoto za mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba

Picha
Mtu wangu wa nguvu najua umezoea kuona nikikuletea TBT Picha za mastaa mbalimbali wa soka wanaofanya vizuri katika soka, ila leo Septemba 29 2016 naomba nikusogezee TBT Picha za utoto za mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba. Kama humfahamu  Paul Pogba  ni jamaa ambaye alizaliwa   Lagny-sur-Marne  wazazi wake wakiwa wametokea  Guinea,  katika soka Pogba  ana ndugu zake wawili ambao ambao wote wanacheza soka pia, kaka yake  Mathias  anachezea timu ya taifa ya Guinea . Paul Pogba muonekano wake wa sasa Paul Pogba muonekano wake wa sasa Pogba wa pili kutoka kushoto waliosimama Pogba wa katikati na kaka zake Pogba wa kwanza kushoto Pogba wa kwanza kushoto