Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017

Mademu Waliotembea na Usher Raymond Kutajirika Baada ya Kuambukizwa Gonjwa la Zinaa

Picha
Inasadikika mwanamuziki mashuhuri wa Marekani Usher Raymond keshawahi kuzuru Nchini kimyakimya kula Bata mbugani. Sasa hivi jamaa ana kesi zinamuandama kwa kuwaambukiza mademu magonjwa ya zinaa mkanda wake jeshi (Herpes) na wanadai fidia Hadi 20m $. Na lazima huko mbugani alipokuja kwenye vekeshen alitandaza miti tuu. Yeye kwake Kinga atumii. Kwa mantiki hiyo mademu kama mlitembea naye Na una maambukizi, haya tafuta mwanasheria nakuchangamkia Fursa faster Huyu hapo juu kibonge anaitwa Quantasia Sharpton 21 kaibuka majuzi Na mwanasheria wake huyo mwanamama mzungu akimtuhumu Usher alimuambukiza mkanda was jeshi ( Herpes) akiwa miaka 18.​ Huyu hapa naye Laura Helm tena alikuwa besti wa mke wa Usher naye anataka 20$million kwa kuambukizwa.​ Cha ajabu mke wa Usher Hana maambukizi yeyote. Wazungu wanavyochukia mafanikio ya mablacks hi ishu wameishupalia kichizi kwenye media. Fursa hiyo kwa mademu zetu kama usher alikugegeda.

Hivi Kwanini Baadhi ya Watanzania Wanataka Diamond Aanguke Kimuziki?

Picha
Diamond Platnumz ni mwanadamu ana madhaifu yake kama alivyo binadamu yeyote yule. Lakini katika picha kubwa na kimuziki huyu ndugu yetu anaiwakilisha nchi vyema sana huko nje. Nadhani hili ndilo la Msingi na tungebaki kuliangalia wote kama Watanzania. Kuwa na timu siyo makosa hata Yanga na Simba ni Wapinzani wakubwa lakini tukija kwenye Taifa Stars hizo timu tunazivua na tunavaa Utaifa. (Huu ndiyo Uzalendo jamani) Utaifa ukiisha tunarudi kwenye timu zetu na kuanza kung'oa viti pale uwanja wa taifa. Hivyo basi kwenye kujenga sifa za wasanii wetu awe Ali Kiba, Diamond au Vanessa Mdee tushindane humu ndani lakini tusifanye chuki kiasi cha kutaka kuchafua sia zao. Hao ni watoto wetu kabisa,watoto wa nchi hii: Hakuna mzazi anayetup watoto jamani. Tumtie moyo Alikiba na tumtie Moyo Diamond: Pia tuwakosoe pale wanapofanya vibaya hali tukiwa na dhamira safi kabiaa ya kutaka kuwajenga kimuziki. Tuepukane na fitna,majungu na uzandiki l: haya mambo hayajengi kabisa.

Ray C Amuomba Msamaha Zamaradi Mketema Kisa Ruge

Picha
Ray Ameamua kufunguka na Kusema Haya: "Kiukweli huwa naumia sana ninapoona mastaa tunatumia muda mwingi kulumbana na kugombana kwa mambo ya kipuuzi sana,mastaa wenzetu wa Nigeria wanatushinda kwa mambo mengi sana sababu wao wanashirikiana na kusapotiana katika mambo mengi sana na hata ukiskia wamepishana basi ujue ni kwa ajili ya biashara tu na si vinginevyo! Nilichogundua Mimi ni kwamba kumekuwa na makundi mbalimbali mitandaoni yanayokuza mambo na kusapoti wasanii kulumbana Mara team simba Mara team nyani!naingea kutoka. Moyoni kuwa watanzania tunasifika kwa kuwa na amani na upendo!sasa iweje tena tuishi maisha ya kuchukiana na ugomvi badala ya kuishi kwa amani?najua sisi wasanii tuna mashabiki wengi. Na tunapenda na nnyie mnatupenda kwahiyo mnatakiwa kutupatanisha tunapogombana na si kutushabikia coz mnaposhabikia ugomvvi ndio mnapotufanya tupoteze muda kulumbana badala ya kutumia huo muda kufanya kazi zetu za sanaa kwa bidii tutangaze nchi yetu tunapoteza muda kulumbana,wen...

Ali Kiba Kufunguka Kuusu Kuachia Wimbo Wake Mpya

Picha
Msanii Alikiba ameweka wazi mipango ya mkongwe wa muziki Abby Skillz, kuwa muda si mrefu atakuja na ngoma yake mpya baada ya ngoma yake ya 'Averina' ambayo alikuwa ameshirikishwa yeye pamoja na Mr Blue ambayo ilitoka mwaka jana. Alikiba Alikiba amesema hayo wakati akimpa pongezi mkongwe huyo baada ya kufanikiwa kufunga ndoa jana na mchumba wake Andoya khalifa Mrimi. "Hongera mkongwe nakutakia kheri na mafanikio katika ndoa yako na ngoma mpya inafuata" aliandikwa Alikiba kupitia katika mtandao wake wa Instagram Abby Skillz ni kati ya wasanii ambao walidaiwa kuwa chini ya usimamizi wa Alikiba kupitia 'Label' yake ya King's Music ambapo Alikiba aliwahi kusema kuwa baada ya kuachia wimbo wake mpya ambao ni 'Seduce Me' alisema baada ya hapo utakuwa ni wakati wa wasanii waliopo kwenye Label yake hiyo kutoka na ngoma zao pia.

Ally Hapi Aagiza Kupitiwa Upya Mkataba wa Mwekezaji wa Kituo cha Mabasi cha Makumbusho

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameagiza kupitiwa upya kwa mkataba wa mwekezaji katika Kituo cha mabasi cha makumbusho baada ya kubaini kuwapo kwa ubadhirifu. Mkataba huo ni kati ya Manispaa ya Kinondoni na Kampuni ya Eastern Capital Limited kwa ajili ya kuendesha kituo hicho. Akiwa ziarani hapo  leo, Hapi ameelezwa na wafanyabiashara wakiwamo bodaboda,  bajaji na machinga kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiwalipisha kodi kubwa na michango bila kuwapa risiti wala kutoelezwa matumizi ya tozo hizo. Hapi alitaka kupata ufafanuzi wa kina kwamba  fedha hizo zinapelekwa Manispaa na kama wanatoa risiti za EFD lakini haikuwa hivyo. "Ni marufuku kukusanya fedha nje ya mkataba, kinachokuongoza ni mkataba sasa nataka kujua hicho unachotoza kama hakipo kwenye mkataba nani aliyekutuma?," "Namuagiza Mkurugenzi wa Manispaa, apitie upya mkataba  huu na kama hauna tija uvunjwe," amesema Ametoa siku tatu kwa Kampuni hiyo kutoa taarifa za makusanyo ya fedha pamoja na kueleza...

Wafugaji Watatu Wauwawa kwa Kupigwa na Wakulima Mkoani Morogoro

Picha
Wakulima watatu wakazi wa Kata ya Kolero wilayani Morogoro wameuawa kwa kupigwa walipokamata mifugo iliyokuwa inalishwa kwenye mazao yao. Diwani wa Kata ya Kolero, Eligius Mbena amesema Alhamisi Septemba 28 ng’ombe zaidi ya 140 waliingizwa kwenye mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Kidodi na kula mazao. Ng’ombe hao ambao inadaiwa ni mali ya mfugaji mmoja inaelezwa wameharibu zaidi ya eka tano za mazao ya mahindi, kunde na mbogamboga yaliyokuwa yakikaribia kukomaa. Diwani huyo amesema baada ya wakulima kuona kundi la ng’ombe waliamua kuwasiliana na mtendaji wa kata ambaye alituma mgambo na kwa kushirikiana na wananchi waliondoa mifugo hiyo na kuipeleka ofisi ya kata. “Baada ya mgambo kufika wale vijana waliokuwa wakilinda ng’ombe walikimbia ndipo wananchi na mgambo walipowaswaga ng’ombe hadi ofisi ya Kata ya Kolero kwa hatua zaidi,” amesema. Amesema kwa utaratibu waliojiwekea, ng’ombe wanapokamatwa kwenye mashamba hutozwa faini ya ...

Ndege ya Kijeshi Yaanguka DR Congo

Picha
Ndege ya kijeshi imeanguka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwaua abiria wote. Maafisa wa maswala ya angani wamesema kuwa ndege hiyo ilifeli kupaa vizuri kutoka uwanja wa ndege wa N'djili katika mji mkuu wa Kinshasa na kuanguka katika makaazi ya Nsele. Haijabainika iwapo kuna watu wowote waliouawa ama kujeruhiwa ardhini. Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kinshasa amesema kuwa ndehe hiyo ilikuwa ikibeba mizigo na kwamba haikuwa na abiria wowote. Ripoti nyengine zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuawa.

Uturuki Yafungua Kambi kubwa ya Kijeshi Somalia

Picha
Uturuki imefungua kambi kubwa ya kijeshi mjini Mogadishu, Somalia. Hii itakuwa kambi yake kubwa kabisa ya mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Kambi hiyo itayokuwa kando ya bahari, ina uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Somalia, zaidi ya 1500 kwa wakati mmoja Lengo ni kulipa nguvu jeshi la Somalia, kupambana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab. Wanajeshi zaidi ya 20,000 wa Umoja wa Afrika na wengine wa kigeni, wanapigana na Al Shabaab hivi sasa. Kuna kambi kadhaa za majeshi ya kigeni nchini Somali.

Yanga imeshindwa kupata ushindi kwa mara ya 3 VPL

Picha
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wamebanwa na kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wa Uhuru na kikosi cha Mtibwa Sugar kutoka Turiani, Morogoro. Ni mechi ya tatu Yanga wanatoka sare katika ligi ikiwa ni mechi ya tano tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Wanajangwani walitoka sare kwa mara ya kwanza dhidi ya Lipuli kwenye mechi ya ufunguzi walipolazimisha sare ya kufungana 1-1. Mara ya pili Yanga kutoka sare kwenye mchezo wa ligi ilikuwa mechi dhidi ya Majimaji FC ugenini kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma walipolazimisha matokeo ya kufungana 1-1. Yanga wameshinda mechi mbili kati ya tano walizocheza, walishinda 1-0 ugenini dhidi ya Njombe Mji halafu wakapata ushindi wao wa pili dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Uhuru. Kikosi cha Mtibwa kimepata sare ya pili mfululizo ugenini, mechi yao ya kwanza kupata  sare walitoka 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi. Kiungo Pius Buswita amecheza kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa na Yanga na uhami...

CCM yafuta uchaguzi wilaya nne

Picha
Mkutano Mkuu wa Halmashauri  Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), umefuta uchaguzi wa wenyeviti katika wilaya nne baada ya kubaini wagombea waliojitokeza hawakua na sifa. Akitangaza uamuzi huo leo , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amezitaja wilaya hizo zilizofutiwa uchaguzi kwamba ni Moshi Mjini,  Siha, Hai,  pamoja na Makete. Amesema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba  wagombea waliojitokea hawakuwa na  sifa, pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama. Hivyo kutokana na uamuzi huo  Polepole amesema kwamba  wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi huo.

CCM Yafichua Alipo Kinana, Yatoa Onyo Kali Kwa Makada Wake

Picha
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana hajahudhuria vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu kwa kuwa aliomba udhuru wa kihali kwa kuwa anauguza ndugu yake wa karibu wa familia. "Ndugu yetu Kinana anauguza ndugu yake wa karibu, tumwombee apone lakini Kinana alishiriki vyema kikao cha Sekretarieti. Kinana hajajiuzulu au kuandika barua ya kujiuzulu," amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Chama hicho pia kimetangaza kuwachukulia hatua kali makada wake watakaobainika kukiuka utaratibu wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Polepole amesema hayo leo Jumamosi alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini hapa akitoa taarifa ya vikao vya juu vilivyoanza juzi Ikulu ya Dar es Salaam. Amesema Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema vikao hivyo vimepitisha majina ya wagombea wa uenyekiti ngazi ya wilaya. Amesema kati ya wilaya 161 za kiserikali ambazo ni sawa na za kichama, kikao c...

Apewa Siku 14 Seth Kupelekwa Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kutibiwa

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14. Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea. Amri hiyo ya mahakama imetolewa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kudai kesi ilipangwa leo Ijumaa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba shauri lipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Baada ya maelezo hayo, wakili Joseph Makandege anayemwakilisha Sethi alieleza kuwa kumekuwepo mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake akapatiwe matibabu na kufanyiwa uchunguzi Muhimbili. “Hadi leo asubuhi tuliwasiliana na mteja wetu na kubaini hajapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama amri za Mahakama zilivyoagiza, hivyo ni rai yetu kwamba kitendo hicho cha kutotekelezwa amri za Mahakama ni ukaidi wa amri halali za Mahakama yako tukufu,” amesem...

Tanzia: CUF Yapata Pigo Kiongozi Wao Afariki

Picha
Kiongozi wa CUF Mheshimiwa Ali Juma Suleiman ambaye alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Baadhi ya viongozi wa (CUF) na wanachama pamoja na wananchi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatilia mwili wa Marehemu Ali Juma Suleyman. Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa Mheshimiwa Ali Juma alikuwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatia kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa katika maeneo ya Masingini na makundi ya watu yanayoendesha vurugu Zanzibar. "Nasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa Ali Juma Suleiman, Kaimu Mwenyekiti wa CUF Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Wilaya ya Magharibi A. Amefariki dunia majira ya saa 4 usiku hapa jana hapa Mnazi Mmoja Hospital baada ya kupigwa vibaya na Mazombi juzi usi...

Lema Amuwakia Mwigulu Asema Hana Sifa ya Kuwa Waziri

Picha
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  na kusema Waziri huyo hana sifa za kuendelea kuwepo katika wizara hiyo kutokana na kuwa na majibu mepesi kuhusu matukio ambayo yanagharimu maisha ya watu. Lema amesema hayo leo alipokuwa jijini Arusha akiongea na waandishi wa habari na kusema amesikitishwa sana na majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu sakata la miili ya watu kuokotwa baharini na sakata la shambulio la Tundu Lissu pamoja na kupotea kwa Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe "Mwigulu Nchemba amenisikitisha sana kwa kauli zake alizokuwa anatoa na sidhani kama anastahili kukalia ile ofisi hata kwa masaa 12 na ni wito wangu kwa Mhe. Rais Magufuli na naamini itakuwa hivyo hawezi kumuacha Waziri kama huyu kwenye ofisi ya serikali inayoshughulika na mambo ya ulinzi na usalama wa watu, matumaini yangu yupo hapo kwa muda tu, toka utamaduni wa maiti za watu kuanza kuokotwa zimeokotwa maiti za watu wen...

Ally Hapi Ashtushwa na Upungufu wa Wauguzi Mwananyamala

Picha
Changamoto ya Upungufu wa watumishi Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala imeelezwa kuwaelemea watoa huduma hali inayoathiri  huduma hospitalini hapo. Hali hiyo imetokana na watumishi wakiwamo wauguzi  50 kuondolewa hospitalini hapo baada ya kubainika  kuwa na vyeti feki. Hayo yamebainika leo, wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Ally Hapi aliyetembelea hospitali hiyo kwaajili ya kukagua miundombinu pamoja kuzungumza na watumishi. Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Daniel Nkungu amesema, Hospitali hiyo ina watumishi 300 huku ikiwa na upungufu wa watumishi 200 hasa manesi na wauguzi. "Wakati Hospitali hii inajengwa mwaka 1973 ilikuwa inatoa huduma kwa watu wachache lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la watu hasa wajawazito na watoto," amesema Amesema, idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na wagonjwa 2500 wanaofika kila siku Hospitalini hapo kwaajili ya kupata huduma. Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ameahidi kufikisha suala hil...

Mwanaume Aliyeshauriwa na Mganga Kufanya Mapenzi na Punda Atupwa Jela

Picha
Mwanamme mmoja nchini Afrika Kusini aliyetambulika kwa jina la Ntando Mankungwini ametupwa jela mwaka mmoja baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Punda. Ntando (23) alikutwa usiku wa Jumatano ya septemba 20 mwaka huu kwenye zizi la nyumba jirani na nyumbani kwao mjini Mount Fletcher, Afrika Kusini akiwa nyuma ya punda usiku wa manane, kitendo ambacho wamiliki wa punda huyo walijua kuwa ni mwizi ila walikuja kustuka baada ya kumlika tochi na kumkuta akiwa utupu. Wamiliki hao wa punda walimkamata na kumpeleka polisi na ndipo mtuhumiwa alikutwa na makosa ya unyanyasaji wa wanyama. Mtuhumiwa akiwa Mahakamani alikiri kosa hilo la kufanya mapenzi na punda huyo huku akieleza kuwa alitekeleza sharti alilopewa na mganga wa kienyeji. Ntando amesema alienda kwa Mganga wa Kienyeji kusaka dawa ya kuongeza nguvu za kiume na ukakamavu, ndipo aliposhauriwa kutembea na Punda. Tayari mahakama ya mwanzo wilayani Mount Fletcher, Cape Town imetoa hukumu jana kwa kumfunga mwaka mmoja jela kwa kosa la u...

Fahamu kiwango cha fedha ambacho ukisafiri nacho lazima utoe taarifa TRA

Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali yahusuyo fedha imetangaza kuwa, kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu, mtu yeyote akisafirisha fedha taslimu dola za kimarekani 10,000 ambazo ni sawa Tsh 22.5 milioni ni lazima awe amejaza fomu yenye maelezo kuhusu fedha hizo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, George I. Mnyitafu imeeleza kuwa TRA imepata mamlaka hayo kutokana na Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, Sura 423 na Kanuni yake inayohusu utoaji wa taarifa ya kiasi cha fedha taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini. Sheria hiyo imeipa Mamlaka ya Mapato Tanzania mamlaka ya kusimamia utoaji wa taarifa kuhusu fedha zinazosafirishwa kuingia au kutoka nchini. Taarifa hiyo ya TRA inahusu usafirishaji wa fedha taslimu au hati za malipo (Bearer Negotiable Instruments) zinazofikia au kuzidi dola za kimarekani 10,000 (elfu kumi) au fedha nyingine yoyote yenye thamani sawa n...

Picha: Mchezaji wa Yanga amshambulia mwandishi wa habari

Picha
CHAMA   cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na wahariri wa habari za michezo nchini, tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kushambuliwa kwa mwanahabari John Dande, zinazodaiwa kufanywa na straika wa Yanga, Obrey Chirwa, juzi Jumanne Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. TASWA na wahariri wa habari za michezo, tunaalani tukio hilo la kushambuliwa kwa Dande ambaye ni mpigapicha wa Kampuni ya New Habari 2006 Limited, kwani kitendo hicho si cha kiungwana bali ni udhalilishaji wa taaluma ya habari na hujuma kwa tasnia na mambo kama haya  yanadhoofisha nguzo muhimu ya kujenga jamii yenye uelewa wa mambo yanayoendelea nchini na kudhoofisha mfumo wa kidemokrasia, ambao tunajitahidi kuuimarisha nchini. Kukaa kimya, hata tukiliwazwa na kuombwa samahani kwa jambo hili, hakutatoa tafsiri nyingine kwa wana taaluma ya habari na jamii kwa ujumla isipokuwa kuliona jambo hili kama ni la kawaida. Kama tukio hilo lingefanyika eneo la starehe au mitaani na mwandishi hakuwa kaz...

Ommy Dimpozi Apigwa Stop Kuzungumzia Post Ile ya Mama Diamond

Picha
Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amesema hawezi  kuzungumzia ishu ya post ya mama mzazi wa Diamond katika ukurasa wake wa Instagram. Muimbaji huyo amesema kufanya hivyo ni kuamsha hisia upya kwa mambo ambayo yalishapita na hata menejimenti yake imemkataza kuzungumzia suala hilo. Katika exclusive interview na Bongo5 Ommy Dimpoz amesema asingependa kuzungumzia hayo lakini kikubwa anachoweza kusema ni kwamba mavuguvugu lazima yawepo kwani ndio kuchangamka kwa muziki na ukizingatia Bongo Flava siyo kama kwaya. “Hayo mengine yanayotokea is just a game lakini siyo vitu vya kushikana mashati au kumwagiana tindikali, hatujafikia huko ila ukiangalia industry zote duniani hayo mambo yapo na vinachagia wanamuziki kuumiza vichwa zaidi,” amesema Dimpoz. “Tukiongea tunakuwa tunarudisha hayo mambo tena nyuma, mimi mwenyewe sasa hivi hata menejimenti imesema bwana hayo mambo husizungumzie tena.  Hayo mambo tukizungumza tutaamsha hisia, inakuwa haijakaa sawa, nafikiri...

Wadau wa Habari Watoa ya Moyoni Waitupia Lawama Serikali

Picha
Wadau wa habari wamesema taasisi za kiraia, asasi na vyombo vya habari vinaogopa kutoa taarifa zinazoikosoa Serikali kwa kuhofia usalama na vitisho wanavyotoka kwenye mamlaka. Mtafiti Mwandamizi wa Shirika la Twaweza, Annastazia Rugaba alizitaka taasisi na wadau wote wa utoaji taarifa kutoogopa vitisho, akitolea mfano wa vitisho walivyowahi kukutana navyo katika utoaji wa takwimu. Kauli hiyo iliibuliwa jana kupitia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji Taarifa, yaliyokuwa yameandaliwa na Wadau wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni uamuzi wa Serikali kujiondoa katika Mpango wa Utendaji Kazi wa Serikali kwa Uwazi (OGP), kufungiwa kwa magazeti likiwamo la Mwanahalisi huku wakihoji maslahi ya viongozi katika utekelezaji wa taarifa na ucheleweshwaji kanuni za Sheria ya Kupata Taarifa. Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Amiri Manento ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema haki ya kupata taarifa ...

Upinzani Kenya Waitisha Maandamano Makubwa Wiki Ijayo

Picha
Muungano wa upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya umma kupinga mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi. Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wanafanya hima kupitisha mswada ambao utamwezesha Uhuru Kenyatta kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa upinzani utasusia marudio ya uchaguzi tarehe 26 mwezi Oktoba. Wanachama wa upinzani walitoka nje wakati upande wa serikali ukitumia wingi wake bungeni kuharakisha mabadiko ambayo yatasababisha mswada huo kuwa sheria kabla ya marudio ya uchaguzi. Kati ya yale yaliyo kwenye mswada huo ni kuruhusu mgombea kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa mgombea mwingine atasusia uchaguzi. Viongozi wa upinzani Kenya wazuiwa kwenye uwanja wa ndege Nairobi Upinzani kuandamana Kenya ''Zaidi ya 100 walifariki'' katika maandamano Ethiopia Marudio hayo ya uchaguzi yana wagombea wawili, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Mswada huo pia unasema kuwa mahakama ya juu haiwezi kufuta matokeo ikiwa mf...

Mke wa Jose Chameleone Ashuhudia Mmewe Akitandikwa Mabanzi na P-Funk Majani Kampala

Picha
Kwa wale wanaofuatilia mziki wa bongo fleva, na wa afrika mashariki kwa ujumla matumaini yangu ni kwamba mnamjua mtayarishaji wa beats maarufu kwa jina p-majani kinywele kimoja, Mwaka 2005 na 2006 alitayarisha mlio wa mziki ambao ulitumika kwa wimbo wa mwanamziki nguli Joseph Haule maarufu kwa jina Professor J, wimbo kwa jina unaitwa nikusaidieje, Jose chameleone kwa ujanja ujanja akasema akaiba beat ile na kutumia kwenye mziki wake wa bombo crat, ambayo ilifanya vyema nchini uganda, Baada ya mwenye mali kugundua kuwa kaibiwa, akawasiliana na chameleone. na majibu ya chameleone ikawa kama anaomba msamaha fulani hivi na akaahidi kulipa dola za kimarekani 2400, miaka ikakatika miwili bila kulipa , majani akakaa kimya kwa kujua kwamba basi ngoja asamehe, Mwaka 2008 nchini kenya kulikuwapo na programu ya kutumia miito ya simu ya ala zinazoendana na beats au milio ya mziki iliyotengenezwa na wasanii mbali mbali au watayarishaji , MTN ilishirikiana na kampuni ya nje ya uganda waka loung...

Mama Mwenye Nyumba Anataka Kuniozesha Mwanae Kinguvu Nguvu

Picha
Husika na kichwa cha habari hapo juu, Mimi ni mpangaji nimepanga nyumba moja hapa mjini na nina kama miezi sita kwenye hii nyumba niliyopanga ambayo mpangaji ni mimi mwenyewe mama mwenye nyumba ni mjane yaani single mother na ana watoto watatu wote wa kike. Kinachonisukuma kuomba ushauri hapa ni nyenendo za huyu mama na binti yake mmoja yule wa pili, yaani huyu mama anaforce mwanae nimuoe yaani niishi nae gheto kwangu niwe nalala naye na kuamka naye. Kila chakula kikiiva naletewa nguo nafuliwa na hadi maji bafuni napelekewa na wanafanya yote haya si kwamba mimi nataka hapana ni kwa lazima, yaani chakula unaletewa ki nguvu nguvu kama ni wali unakuwa hadi ushamwagiliziwa maharage na mchuzi sasa kwa mazingira haya ni vigumu sana kukataa. Jana binti kaja usiku kuniletea msosi na hakurudi tena ndani kwao akabaki hadi asubuhi, mimi leo nimeondoka kwenda kazini nimemuacha gheto nimerudi nimekuta kapika chakula chetu wawili tofauti na chao kile cha kwa mama yake. Sasa kwa staili hii ya k...

Meya Ubungo Akomaa na Makonda

Picha
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob ameapa kuendelea kupambana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kuhakikisha mashtaka aliyoyafikisha Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa yanafanyiwa kazi na kusisitiza kuwa hayuko tayari kuyafuta. Jana, Meya Jacob alifika kwenye ofisi hiyo ya Sekretarieti katika kile alichosema kuwa ni kuitika wito kuhusiana na suala lake alilofikisha hapo. “Nitaeleza kwa kifupi tu kile tulichojadiliana huko juu na Sekretarieti,” alisema Meya Jacob baada ya kushuka kutoka ghorofa ya nne ya Jengo la Sukari zilipo ofisi hizi na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri. Meya huyo ambaye mahojiano yake na Sekretarieti yalidumu kwa takriban saa nne, alidai kwamba amekuwa akiombwa kufuta shauri hilo na mara kadhaa. Alidai kwamba watendaji wa Sekretarieti walimwarifu kuhusu ombi la mkuu wa mkoa kukutana naye kwa ajili ya kushauriana jinsi ya kulimaliza shauri lake. Hata hivyo, ...

Mbunge Lijualikali Ashikiliwa Polisi

Picha
Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali na viongozi watatu wa Chadema wilayani Malinyi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya kusanyiko lisilo halali. Mbunge huyo amekamatwa leo Alhamisi saa 12:40 jioni akitoka kwenye kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Kijiji cha Makerere wilayani Malinyi. Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alfonce Mbassa amesema baada ya kumaliza kikao, mbunge huyo na viongozi wengine walipanda kwenye magari ili  kuondoka lakini ghafla lilitokea gari la polisi na askari walimuamuru Lijualikali ashuke. "Tulishuka wote kujua tatizo ni nini lakini askari walimhoji Lijualikali kwa nini amekwenda kufanya siasa Malinyi wakati yeye ni mbunge wa Kilombero," amesema Mbassa. Amesema walijaribu kuwaelewesha polisi kwamba kilikuwa ni kikao cha ndani lakini askari walisisitiza kuwa lilikuwa kusanyiko lisilo halali. Amewataja waliokamatwa pamoja na mbunge huyo kuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Malinyi, ...

Ile Gari Aina ya RAV 4 Aliyopewa Hamisa Mobeto na Diamond Platnumz Yaibua Zengwe

Picha
BADO mrembo aliyezaa na Mbongo Fleva, Hamisa Mobeto ameendelea kutengeneza vichwa vya habari, safari hii, gari lake aina ya Toyota Rav 4 alilopewa na msanii huyo, linadaiwa kuibua zengwe kwa kile kinachoelezwa kuwa ilikuwa msanii huyo ampe mama’ke, akabadilisha maamuzi ghafla na kumpa Mobeto. TUJIUNGE NA CHANZO Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na familia ya Mobeto kimenyetisha kuwa, msanii huyo aliagiza gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tano kabla ya Mobeto kujifungua na ilikuwa amzawadie mama yake mzazi. “Yule msanii alikuwa anataka kumpa ile Rav 4 mama yake sasa ilipotua nchini ndiyo wakati ambao Mobeto alikuwa amejifungua kwa hiyo akaona bora ampe mzazi mwenziye huyo mpya kwanza halafu mama yake akaahidi kumuagizia gari lingine. “Sasa nasikia mama wa msanii hakufurahishwa na kitendo hicho. Kidogo alimaindi kwani tayari yeye alishajiandaa ku-drive mkoko mpya. Akabaki anaumia na moyo wake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “H...

Serikali kuwapatia wabunge ulinzi

Ikiwa nimuda wa wiki tatu umepita tokea kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu huko Dodoma majira ya mchana alipokuwa akitoka Bungeni kuelekea nyumbani kwake, serikali sasa imetangaza kuanza mchakato wa kuboresha ulinzi kwa wabunge wote. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha runinga cha Clouds360 kinachorushwa na Clouds TV. Waziri Nchemba alieleza kuwa maswala ya ulinzi kwa viongozi wa umma yapo kwa mujibu wa sheria, lakini kuna watu ambao bado hawajatambulika na kupewa ulinzi. Aliendelea kwa kusema kuwa suala la ulinzi kwa wabunge linafanyiwa kazi na ulinzi utaongezwa. “Kwa sasa suala hilo la ulinzi kwa waheshimiwa wabunge linashughulikiwa na tutaongeza ulinzi kwenye maeneo yote ya viongozi na kufanya doria za mara kwa mara,” alisema Mwigulu. Waziri aliwataka wananchi wote kuwa na amani na kuondoa hofu dhidi ya matukio ya kihalifu yaliyotokea na kueleza kuwa v...

Amuua mwenzake kisa mabishano kuhusu makalio ya mwanamke

Picha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo. Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo  hayo wakati akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji  cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26). Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuwawa juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao. Alisema baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya kawaida sio  makubwa. Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka ...

Bunge Latoa Ufafanuzi Sababu za Kulichukua Gari la Mbowe na Kulirudisha Nchini

Picha
Ofisi ya Bunge imesema Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe hajanyang’anywa gari. Taarifa iliyotolewa na Bunge  jana  Alhamisi imesema kilichotokea ni kwamba, gari hilo limerudishwa nchini ili dereva afuate utaratibu wa kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi. Mbowe yuko Nairobi nchini Kenya ambako Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea na matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma. Bunge limesema ni kweli gari lenye namba ya usajili STL 4587 aina ya Toyota Prado limetengwa maalumu kwa ajili ya kumuhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kutekeleza majukumu yake ya kikazi na binafsi nchini. “Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni aliomba gari ikamhudumie mjini Nairobi nchini Kenya na Ofisi ya Bunge iliridhia ombi hilo na kuomba taratibu zizingatiwe. Hata hivyo, ofisi iligundua kwamba gari ilikwenda Nairobi na dereva hakupata kibali cha ...

Yasome hapa magazeti ya leo Ijumaa Septemba 29, 2017

Picha