Askofu: Siogopi kuitwa mchochezi kwa hiki ninachofanya

Askofu wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema kuwa kwa sasa nchi inahita katiba mpya kuweza kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayoibuka, na kwamba hatojali akiitwa mchochezi kwa kutetea haki za wananchi.

Askofu Severin aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano wa asasi mbalimbali za kijamii na kusema kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.

Akifungua mkutano huo uliolenga kujadili suala la katiba mpya, Askofu Severin alisema kuwa yeye kama kiongozi wa dini anahubiri, ukweli na haki na hivyo hatasita kusema ukweli kuwa imefika wakati taifa linahitaji kuwa na dira makini.

Hakuna mwanaharakati wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye mchafuko, badala yake tunalitakia mema taifa na kuona tunapata maendeleo katika misingi mizuri, alisema kiongozi huyo wa kanisa.

Akizungumzia matukio ambayo kwa siku za karibuni yamekuwa yakiripotiwa nchini, Askofu Severen amesema kuwa hiyo si ishara njema kwa taifa ambalo lilikuwa likisifiwa na kwa kuwa na amani.

Alisema kuwa ni kweli Rais anafanya mambo mengi mazuri lakini akatahadharisha kuwa, huenda mambo hayo yakashindwa kulindwa na kuendelezwa baada ya kiongozi huyo kumaliza muda wake kutokana na kutokuwepo kwa katiba yenye misingi mizuri.

Alitoa wito kwa Rais kuona hayo aliyoyasema kama ataona yanafaa basi ayafanyie kazi ili kuwepo kwa mifumo imara itakayoenzi haya anayoyafanya baada ya yeye kuondoka.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA