Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2016

Man United miaka mitatu baada ya Ferguson

Picha
Soka sasa limebadilika Mno. Kimsingi ladha halisi ya mpira wa miguu inapotea kwa kiasi kikubwa mno. Kuanzia kwa makocha wenyewe, wamiliki wa vilabu hivi, wachezaji mpaka mashabiki hali inayopelekea kupunguza ladha halisi ya mpira wenyewe. Wamiliki pamoja na mashabiki wa vilabu hivi hasa vilabu vikubwa, kwa kiasi kikubwa mara nyingi  huwa wanakosa sana uvumilivu wa timu zao kutofanya vizuri. Wanalazimisha mabadiliko ya ghafla ambayo kamwe hayawezekani kwa mchezo wa soka. Kutokana na hali hiyo, makocha  wengi wa siku hizi wanajikuta wakifundisha soka la kupata matokeo tu na sio soka hasa la kuburudisha linaloambata na matokeo. Muda wanaopewa kufundisha timu hizi ni mdogo mno kutokana na kukosekana kwa uvumilivu kwa wamiliki na mashabiki. Na hivyo kusababisha ladha halisi ya mchezo wa soka kupungua, na ili kuendana na hali hii ndiyo maana unakuta siku hizi kuna wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ila pasipo kucheza nafasi hizo kwa u...

HABARI HIZI ZA KUHUSU TETSI ZA ALICHOKIFANYA RAIS MAGUFULI NAIROBI LEO ZIAFUNIKA MITANDAO YOTE YA KIJAMII AFRICA LIVE!!

Picha
Rais Magufuli aliyeko ziarani nchini Kenya amelazimika kutembea kwa miguu kufuatia msongamano mkubwa wa magari kwa kile kilichodaiwa barabara haikuwa imeandaliwa kwa kiongozi huyo kupita. Mashuhuda wa tukio hilo waliimbia tovuti ya  The Star  ya nchini Kenya kuwa Rais Magufuli alitembea kwa sababu ya msongamano wa magari katika barabara kuu ya Uhuru alipokuwa akielekea lilipo kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta. Watumiaji wengi wa mitandao nchini Kenya wameandika kuhusu kitendo hicho cha ujasiri cha Rais Magufuli huku wakiwaponda viongozi wao kuwa hawana ujasiri huo. Rais Magufuli amewasili nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili kufuatia mualiko wa Rais Uhuru Kenyatta ambapo pamoja na mambo mengi anatakayoyafanya, atatembelea kaburi la Rais Jomo Kenyatta, atazindua barabara jijini Nairobi na kujadiliana na Rais Kenyatta kuhusu mambo mengi ikiwa ni pamoja na ada wanayotozwa wanafunzi wa Kenya Tanzania, masuala ya kibiashara na diplomasia.

Spika kataja vitu vitakavyojadiliwa kwenye bunge linaloanza kesho

Picha
Kesho Nov 1 2016 tunatarajia kuanza kuzisikia habari za kutokea bungeni Dodoma ambapo vikao rasmi vya mkutano wa tano wa bunge la 11 utaanza. Leo Spika wa bunge Job Ndugai alikutana na waandishi wa habari Dodoma na kuelezea baadhi ya mikakati itakayofanyika ikiwa ni pamoja na kujadili muswada wa sheria ya za huduma za habari. ‘Mkutano wetu wa tano wa bunge la 11 unaanza kesho November 1 hadi November 11 2016 ambapo shughuli yake ya kwanza inaongozwa na kanuni ya 94 lengo likiwa ni kujadili na kupokea maoni kuhusiana na bajeti ijayo ya serikali‘ –Job Ndugai ‘Jambo lingine ni kwamba katika mjadala huo tunatarajia serikali itapokea ushauri kuhusiana na vyanzo vya mapato, vipaumbele vya uandaaji bajeti ijayo ambapo haya yote yatafanyika katika siku tatu mfululizo‘ –Job Ndugai ‘Kutakuwa na taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali yani CAG katika kazi zilizokaguliwa kwa mwaka 2014/2015 pia kutakuwa na majadiliano ya makubaliano ya makubaliano ya Afrika...

TAARIFA TOKA IKULU JUU KINACHOENDELEA ZIARA YA RAIS MAGUFULI NCHINI KENYA

Picha

SERENGETI NA BUNDA WANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SINGITA GRUMETI.

Picha
Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti. Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti. Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti. Madawati yaliyotolewa na Mfuko wa Singita Grumeti kwa ajili ya Wilaya ya Bunda. Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha h...

KITU CHA KWANZA RAIS MAGUFULI ALICHOWAAMBIA WAKENYA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameomba Wakenya kuja kufanya biashara Tanzania Ameyasema hayo akiwa katika ziara ya siku mbili nchini humo na kuwaeleza kuwa wanaweza kuja kufanya biashara hata leo. “Ninawakaribisha tena Wakenya wote wanaotaka kufanya biashara Tanzania, waje hata leo” amesema Magufuli. Dkt Magufuli yupo jijini Nairobi, katika ziara yake ya kiserikali ya siku mbili nchini humo. Chini ni picha za mapokezi yake nchini humo.

TAZAMA PICHA ZA HARUSI YA KLEYAH NA MCHUMBA WAKE WA MIAKA 7

Picha
Baada ya kuwa katika mahusiano yaliyodumu kwa miaka 7 na kufanikiwa kuweka uhusiano wao nje ya macho ya umma, msanii maarufu wa Bongo Kleyah amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye pia ni meneja mshirika, Mhandisi Barnabas Ndyanabo mjini Kampala, Uganda Septemba 10, 2016. Harusi ilifanyika katika hoteli ya kifahari ya Serena. Sherehe hiyo ilibarikiwa na mualiko wa wageni 100 ambao ni watu wa karibu sana wa familia na marafiki. Bongo songstress huyo alivalia lulu beaded fascinator na lace Berta vilivyonogesha gauni maalum lililotengenezwa na designer maarufu kutoka nchini Afrika Kusini na lilikuwa kama mermaid silhouette na alivalia viatu vya Bradgley Mischaka.

Makonda azindua nembo ‘I love Dar’

Picha
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua nembo ya I love Dar (naipenda Dar) inayobeba dhana nzima ya utalii wa ndani hususan mkoa wa Dar es Salaam. Tukio hilo lilotokea juzi usiku majira ya saa saba huku likishuhudiwa na mamia ya watu waliojitokeza kwenye uzinduzi huo uliofanyikia katika baa ya Element iliyopo Oyster bay. Akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo hiyo Makonda alisema kuwa ni hatua nzuri kwa wadau binafsi kujitokeza na kuendeleza mazuri kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Alisema kuwa kwa kupitia nembo hiyo ya I love Dar inahamasisha kuendeleza uzuri wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kutangaza kila aina ya kivutio chake. Alisema, vipo vitu vya asili ambavyo vinatumiwa kama utalii hasa kuanzia majengo ya kizamani hasa maeneo na mjini, makumbusho za taifa zenye kuhifadhi historia ya Mkoa pamoja na mengineo. Alisema kuwa nembo hiyo inaenda mbali hadi kuhamasisha masuala ya kimaendeleo ya Dar es Salaam likiwamo suala zima la usafi pia. ...

Malinzi ameteuliwa nafasi hii CAF

Picha
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Issa Hayatou ameteua Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati maalumu ya mageuzi ya muundo wa CAF itakayokuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho, imefahamika.  Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, katika Kamati hiyo ikayoongozwa na Rais Issa Hayatou mwenyewe, Malinzi ameteuliwa katika Kamati hiyo iliyotangazwa leo Oktoba 30, 2016 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Korea Kusini ametakiwa ajiuzulu

Picha
Maelfu ya wananchi wa Korea Kusini, waliandamana kwenye mji mkuu Seoul, Jumamosi, kumtaka Rais Park Geun-hye ajiuzulu. Polisi wamekadiria kuwwa karibu waandamanaji 12,000 walishiriki. Rais wa Korea Kusini yupo kikaangoni kwa kudaiwa kuvujisha nyaraka za serikali kwa rafiki yake. Wananchi wanataka na mawaziri kadhaa nao wajiuzulu. Jumanne iliyopita, Bi. Park alikiri kumuonesha rafiki yake Choi Soon-sil nyaraka hizo. Choi ambaye hana nafasi yoyote serikalini, alikuwa akimsaidia Park maoni kwenye hotuba zake kabla ya uchaguzi wa Rais mwaka 2012. Rais huyo ameomba radhi.

RAIS MAGUFULI AAGWA AKIENDA KENYA KWA ZIARA YA SIKU 2

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiser...

Faraja Kotta Afunguka Haya Baada ya Miss Tanzania 2016 Diana Edward Kuandamwa Mitandaoni.

Picha
Aliyewahi kuwa mshindi wa Miss Tanzania kwa mwaka 2004, Faraja Kotta Nyalandu amechukizwa na yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii juu mshindi wa taji la Miss Tanzania 2016, Diana Edward. Hatua hiyo imekuja baada ya watu katika mitandao ya kijamii kuanza kumshambulia mshindi huyo juu ya umri wake. Hata hivyo kamati ya Miss Tanzania ilitolea ufafanuzi juu ya suala hilo. Miss Faraja Kotta ambaye na yeye pia alipitia kipindi kigumu pindi alipotangazwa mshindi, ameandika ujumbe huu. Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda. Asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano. Nilipigiwa simu kuamshwa. Nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani. Nilitetemeka, nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki Miss Tanzani...

Gareth Bale Aongeza Mkataba Mpya Real Madrid.

Picha
Uhamisho wa Bale ulivunja rekodi ya dunia 2013 Real Madrid imemsainisha mkataba mpya winga wake Gareth Bale na kumfanya aendelee kudumu klabuni hapo mpaka 2022. Bale mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013. Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135. Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu. Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000

Rais Magufuli Kuzindua Barabara Nairobi.

Picha
Rais Magufuli na Rais Kenyatta wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara yake ya kikazi katika nchi jirani ya Kenya leo. Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake na pia kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi. Barabara hiyo, ambayo inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini, ni moja kati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Kenya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kuu. Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi. "Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini ...

Shearer: Aguero ndiyo mchezaji pekee world class EPL

Picha
Legend wa Newcastle United Alan Shearer amekuja na habari mpya iliwastua wengi kwa kusema kuwa kwenye Ligi Kuu ya England kuna mchezaji mmoja tu mwenye uwezo wa kucheza timu yoyote ulimwenguni ambaye ni Sergio Aguero. Licha ya vilabu vingi kumwaga pesa kwa ajili ya usajili wa wachezaji mbalimbali, mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa England amesisitiza kuwa straika huyo wa Kiargentina ndiyo mchezaji pekee ambaye anaweza kuamua ubingwa kwenye timu. Aguero alifunga mara mbili kwenye mchezo ambao Manchester City ilishinda mabao 4-0 dhidi ya West Brom kwenye Uwanja wa Hawthorns, hali iliyompelekea Shearer kusema maneno hayo. Akiongea kwenye Match of the Day, Shearer amesema: “Ni moja ya wachezaji waliojipambanua kuwa bora na wa kiwango cha dunia, nadhani ndio hyuo pekee tuliye naye hapa Premier League na ni mshambuaji bora kabisa wa kati kwa sasa kwenye ligi.” Alipoulizwa na Gary Lineker sababu gani zinamfanya aseme hivyo, Shearer aliendelea kumtetea kwa kusema: “...

JOKATE KIDOTI AMTAJA HUYU MTU AMBAYE YUPO TAYARI KUFA KWA AJILI YAKE

Picha
Mrembo wa Tanzania na Mwanamitindo Jokate Mwegelo, ameamua kuweka wazi mtu ambaye  yupo tayari kufa kwa ajili yake ikiwa hamna namna. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Jokate amedai mtu Pekee ambaye yupo tayari kufa kwa ajili yake ni Mumewe.   Jokate Mwegelo “Mume wangu” alimjibu swali Shabiki aliyemuuliza katika mtandao huo.

Ajinasua Jela Kwa Kulipa Sh138 Milioni

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu mtoto wa Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (CCM) kulipa faini ya Sh138,390,000 au  kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kukiri kosa na kutiwa hatiani kwa kumiliki nyara mbalimbali za Serikali. Katika kesi hiyo, mtoto huyo Pirmohamed Haroon alikutwa akimiliki kilo 46 za nyama ya tandala, mbawala, swala pala, tohe, njiwa pori, kanga pori na pembe za tandala na tohe vyote vikiwa na thamani ya Sh138,390,000. Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alimhukumu mshtakiwa huyo kulipa faini hiyo ambayo ni mara 10 ya thamani ya nyara alizokutwa nazo na iwapo atashindwa atumikie kifungo cha miaka 20. Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Haroon alikwepa adhabu ya kifungo kwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kupatiwa risiti ya malipo ya Serikali namba 8870022.

Saluti ya Polisi Kwa Prof Lipumba Yazua Gumzo

Picha
Suala la polisi kumpigia saluti mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba limezua mjadala baada ya kuonekana kuwa si mmoja wa viongozi wanaopaswa kupata heshima hiyo kisheria. Juzi, Polisi alionekana akimpigia saluti Profesa Lipumba katika eneo la Buguruni alipokwenda kufanya usafi. Kitendo hicho kimeibua mjadala mitandaoni, watu wakihoji uhalali wa mwanasiasa huyo kupewa heshima hiyo. Juni 2005, aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Kapteni John Chiligati alipokuwa akijibu swali la aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Salome Mbatia alibainisha maana ya saluti na makundi ya watu wanaostahili kupigiwa saluti na askari. Chiligati alisema saluti ni kitendo kinachofanywa na askari kwa maana ya kutoa salamu kwa ishara yenye kuonyesha heshima. Pia, alisema saluti ni njia mojawapo ya kuonyesha heshima na utii kwa kiongozi mkuu kwenye asasi za kijeshi.

Kilichosemwa na Umoja wa Mataifa Kuhusu Kenya Kuondoa Adhabu ya Kifo

Picha
Siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kubatilisha hukumu ya Kifo na kuwa kifungo cha maisha jela, Umoja wa Mataifa umepongeza maamuzi ya Kenya juu ya kufuta adhabu ya kifo kwa maelfu ya watu waliokuwa wakisubiri kutekelezwa hukumu hiyo dhidi yao. Kwa mujibu wa msemaji wa wa idara ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani, amesema hatua hiyo ya serikali ya Kenya ni ya kupongezwa, yenye kutia matumaini na inayofaa kufuatwa na nchi nyingine. Ravina amesema anaamini kuwa serikali ya Kenya itafanya mikakati ili kuhakikisha kuwa hukumu hiyo inafutwa kabisa kwa misingi ya sheria na katiba. Rais Uhuru Kenyatta, Jumatatu iliyopita alibadili hukumu zote za kifo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kuzifanya kuwa kifungo cha maisha jela. Hatua hiyo imewaondolea adhabu ya kifo wafungwa 2,747 katika nchi hiyo ambayo haijamyonga mfungwa yeyote aliyehukumiwa kifo kwa kipindi cha miaka 30 mpaka sasa. Kupunguzwa adhabu ya kifo kwa idadi kubwa ya wafungwa kulifanyika m...

Simba hakuna kulala, yaanza mipango ya kuimaliza Stand United

Picha
Baada ya ushindi wake wa 3-0 dhidi ya Mwadui mkoani Shinyanga, kikosi cha Simba kimeendela na mazoezi chini ya kocha mkuu Joseph Omog na wasaidizi wake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Jumatano dhidi ya Stand United. ‘Mnyama’ anaisubiri Stand United ambayo Jumapili ilicheza dhidi ya Ruvu Shooting ambapo mchezo huo ulimalizika kwa suluhu. Camera ya  shaffihdauda.co.tz  imezinasa picha wakati Simba wakipiga jaramba kwenye uwanja wa Kambarage, unaweza kuziangalia hapa chini.