‘Tutafanya kila kitu kinachowezekana kutetea ubingwa wetu – Hans van Pluijm’

Na Baraka Mbolembole

MUDA mfupi baada ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu kuinoa timu ya Yanga SC, mkufunzi raia wa Holland, Hans van der Pluijm amesema atafanya kila awezalo pamoja na wachezaji wake kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wake wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.

“Nimefurahi kurejea Yanga,” anasema Hans nilipofanya naye mahojiano mafupi mchana wa leo. Hans alijiuzulu katika nafasi yake muda mfupi baada ya timu yake kushinda 6-2 dhidi ya Kagera Sugar FC wiki iliyopita katika uwanja wa Kaitaba, Bukoka baada ya uongozi wa Yanga kufungua mazungumzo ya kumuajiri kocha raia wa Zambia, George Lwandamina.

Mwanachama wa klabu hiyo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Tanzania, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba alikutana na kufanya kikao na kocha huyo mshindi mara mbili wa VPL na kufanikiwa kumshawishi kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu.

“Tutafanya kila kitu kinachowezekana ili kutetea ubingwa wetu kwa mara nyingine. Asante kwa sapoti yako,” anasema Hans mwenye miaka 67.

Yanga ilicheza bila mkufunzi huyo na kuisambaratisha JKT Ruvu kwa magoli 4-0 siku ya Jumatano na kufikisha alama 24, pointi tano nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC. Jumamosi hii, Hans ataingoza timu yake katika mchezo vs Mbao FC ya Mwanza katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA