Anthony Davis Afanya Makubwa, lakini timu yake yachapwa.

Kocha wa Denver Nuggets, Mike Malone aliamuakuwa timu yake haikuwa na haja tena ya kupambana na mchezaji aliyekuwa kwenye kiwango cha juu Alfajiri ya leo, Anthony Davis. Aliamua Denver Nuggets wahakikishe wanabaki kwenye misingi yao ya kawaida ya kiulinzi na ikawalipa.

Jusuf Nurkic alifunga pointi 23, Will Bartonakaongeza 22 na kuisaidia Nuggets kuepuka kufungwa katika siku ambayo mchezaji Anthony Davis alikuwa katika kiwango bora hivyo kuifunga Pelicans kwa pointi 107-102 ikiwa ni michezo ya kwanza kwa vilabu vyote.

“Ukicheza dhidi ya mchezaji bora wa kiwango chake unakuwa na maswali unayotakiwa kuyajibu, aidha umkabe kuhakikisha hachezi kwa uhuru ila usababishe shida katika maeneo mengine ya ulinzi au umwache katika kiwango chake ila uhakikishe hapati msaada kutoka kwa wengine. Alisema kocha Malone.

Denver wakaamua kufanya la pili, katika siku ambayo mchezaji Anthony Davis alifunga pointii 50, akadaka rebound 16, akaiba mipira mara 7, assist 5 na kupiga block mara 4. Athony Davis alikuwa katika kiwango bora sana.

Davis amekuwa mchezaji wa kwanza kuweza kupata walau pointi 45, rebound15, assist 5 na kupokonya mipira mara 5 tangu NBA ianze kuhesabu utaratibu wa kupokonya mipira msimu wa mwaka 1973-74.

Hata hivyo Anthony Davis hakupata msaada kwenye eneo la ushambuliaji kutoka kwa wenzie. Davis alipata mitupo 17-kati ya-34; Huku wachezaji wa Pelicans waliobaki walipata mitupo  21-kati ya-58 kwa pamoja.

Tim Frazier alifunga pointi 15 kwa upande wa Pelicans. E’Twaun Moore akaongeza 10 lakini akakosa mtupo wa pointi 3 ambao ungeweza kufanya walingane kwa alama kwa sekunde 24 zilizobaki.

Danilo Gallinari alifunga pointi 15 kwa upande wa Denver, Wilson Chandler alifunga pointi 12 huku Kenneth Faried akimaliza mchezo na rebound 14.

HIGHLIGHTS

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA