Machapisho

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amelipongeza Shirika la Afya Duniani (WHO)

Picha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amelipongeza Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kwa juhudi inazofanya kwa pamoja katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola. Waziri Ummy amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika mkutano wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaojumuisha Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika unaoendelea jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo. Aidha, Waziri Ummy amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom kwa kutangaza Ebola kuwa janga la Kimataifa, na kuongeza kuwa Tanzania imefaidika na msaada wa WHO ambao umeiwezesha nchi kujenga uwezo wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utaingia nchini. Waziri Ummy amesema kumekua na uboreshaji wa mpango mkakati wa Ebola uliofanyika Mwezi Machi Mwaka 2019 ambao umelenga kuimarisha ufuatiliaji wa mgonjwa maeneo ya mipakani, kujenga uwezo wa wat...

Harufu chafu kwa wanawake sehemu za Siri na Tiba yake.

Picha
Harufu chafu kwa wanawake sehemu za Siri na Tiba yake. Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimlaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano. Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho,hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama ‘Vaginosis’. Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla. Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni: • Kuwa na wapenzi wengi. • Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango. • Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali. • Uchafu. • Uvutaji sigara. • Pombe. • Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni. Dalili za ugonjwa. •Kutokwa na uchafu...

SIKU MKEO AKIANZA KULALA NA MWANAUME MWINGINE JUA KIFO CHAKO KI KARIBU.......

"Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akawa na upendo wa dhati kwa mke wake lakini mwanamke hawezi kuchepuka na akaendelea kumpenda mume wake kwa dhati.Nasema hivi kwasababu mwanaume hafanyi tendo la ndoa kwa hisia, mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa bila hisia mguso.Ndiyo maana wanaume wanahitaji mahali pa kufanya tendo la ndoa ila wanawake wanahitaji sababu ya kufanya tendo la ndoa. Wanawake wengi wanaoenda mahakamani kudai talaka kwa waume zao ni wale wachepukaji,mwanamke asiyechepuka hawezi kwenda mahakamani kudai talaka isipokuwa kama mumewe atakuwa amezidisha unyanyasaji wa kimwili na kiakili kiwango cha kukaribia kumuua mkewe. Wanaume hawawezi kubadili tendo la ndoa na upendo.Mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa na mwanamke lakini bado akawa hampendi-ndiyo maana wanawake wanaojikuta kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume waliooa wanaowapenda wake zao kwa dhati hupata tabu saana kupata kufurahia mahusiano hayo kwani huwa wanatumika tu na hao wanaume wenye ndoa zao....

HISTORIA YA WANYATURU.

WANYATURU ambao awali walijulikana kwa jina la Warimi ni watu wanaoishi karibu wilaya zote za mkoa wa Singida yenye tarafa saba. Kwa Mujibu wa Patrick Mdachi katika kitabu cha Wanyaturu wa Singida, Mila na Desturi zao, Wanyaturu ni moja ya makabila yanayojumlishwa katika kundi la Nilo-Hamites, lenye asili ya Wabantu walioishi Abysinia ambayo sasa inajulikana kama nchi ya Ethiopia. Watu hao waliihama Abysinia (Ethiopia) kutokana na njaa kubwa kiasi ambacho hawakuweza kustahimili kukaa tena hapo. Njaa ndiyo iliwalazimisha watu hao kufikia kula nzige, katika harakati za kutafuta nzige hao ndio ukawa mwanzo wa safari yao ya kuhama. Mdachi anasema katika kitabu chake hicho kilichochapishwa na Benedictine Publicationss Nandanda - Peramiho mwaka 1991, kuwa Wanyaturu waliingia Tanzania kupitia sehemu ya kaskazini kutokea Kenya na Uganda na kufanya maskani yao eneo la Uzinza, Mwanza, baadaye walihamia eneo la Pasiansi na mwaka 1700 walikutwa na Wasukuma ambao waliwafukuza na kuwafanya w...
          "KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI" KISA ICHI KIMEKUSANYWA  NA KUANDALIWA                VEMA NA TAWFIQ MASSINI.       KISA CHA NABII MUSA NA HIDHIRI               SEHEMU YA KWANZA Ni kisa cha  hidhri ameelezewa kama Nabii au Walii au hata Malaika aliye ahi mpaka leo hii ni nabii ambaye bila ya musa uwenda tusinge mfaham ALLAH natusimlia katika qurani  sura ya 18 aya 60 mpaka 82 "Nakumbukeni musa alipomwambia kijana wake  nitaendelea na safari  mpaka  nifike katikati ya  maungano ya bahari mbili  au niendele karne na  karne mpaka  nikutane na huyo ninayetaka kukutana  naye." Kabula ya kisa cha hidhiri tuanze kisa cha musa nacho kwa uchache........ ...Nabii Musa A.S. alipokuwa mkubwa, mkewe Firauni alimwamrisha mama yake amlete ili apate ...

Costa afungiwa mechi 8 kisa kutoa lugha chafu

Picha
Straika wa Atletico Madrid, Diego Costa amefungiwa mechi 8 na Shirikisho la Soka la nchini Hispania baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi aliyechezesha mechi yao dhidi ya Barcelona siku ya Jumamosi. Kifungo hiko kinamaanisha kwamba Costa atakosa mechi zote zilizobaki za msimu huu ambapo Atletico Madrid wamebakiza mechi saba za La Liga. Costa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumtukana mwamuzi Gil Manzano dakika ya 28. Costa alikuwa akimtukana Mama wa mwamuzi ambapo adhabu yake ni kufungiwa mechi 4 . Na mechi 4 tena zimeongezwa kwasababu Costa alimshika mkono mwamuzi kumzuia kutoa kadi za njano kwa wachezaji 

Picha: Mazoezi ya mwisho ya Simba SC kuelekea DR Congo

Picha
Kikosi cha Simba SC kikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kuondoka nchini kwenda Lubumbashi, DR Congo kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe utaochezwa Jumamosi.