Costa afungiwa mechi 8 kisa kutoa lugha chafu



Straika wa Atletico Madrid, Diego Costa amefungiwa mechi 8 na Shirikisho la Soka la nchini Hispania baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi aliyechezesha mechi yao dhidi ya Barcelona siku ya Jumamosi.

Kifungo hiko kinamaanisha kwamba Costa atakosa mechi zote zilizobaki za msimu huu ambapo Atletico Madrid wamebakiza mechi saba za La Liga.

Costa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumtukana mwamuzi Gil Manzano dakika ya 28.

Costa alikuwa akimtukana Mama wa mwamuzi ambapo adhabu yake ni kufungiwa mechi 4 . Na mechi 4 tena zimeongezwa kwasababu Costa alimshika mkono mwamuzi kumzuia kutoa kadi za njano kwa wachezaji 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA