Machapisho

Costa afungiwa mechi 8 kisa kutoa lugha chafu

Picha
Straika wa Atletico Madrid, Diego Costa amefungiwa mechi 8 na Shirikisho la Soka la nchini Hispania baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi aliyechezesha mechi yao dhidi ya Barcelona siku ya Jumamosi. Kifungo hiko kinamaanisha kwamba Costa atakosa mechi zote zilizobaki za msimu huu ambapo Atletico Madrid wamebakiza mechi saba za La Liga. Costa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumtukana mwamuzi Gil Manzano dakika ya 28. Costa alikuwa akimtukana Mama wa mwamuzi ambapo adhabu yake ni kufungiwa mechi 4 . Na mechi 4 tena zimeongezwa kwasababu Costa alimshika mkono mwamuzi kumzuia kutoa kadi za njano kwa wachezaji 

Picha: Mazoezi ya mwisho ya Simba SC kuelekea DR Congo

Picha
Kikosi cha Simba SC kikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kuondoka nchini kwenda Lubumbashi, DR Congo kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe utaochezwa Jumamosi.

Serikali Kuwajengea Uwezo Wananchi katika Masuala ya Mafuta, Gesi

Na Immaculate Makilika- MA Serikali  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea na mkakati wake wa kuwajengea uwezo wananchi  illi waweze kupata taaluma na kuweza kushiriki kwenye sekta ya mafuta na g Akizungumza  Bungeni leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Nishati,  Subira Mgallu alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuvitumia vyuo vilivyopo nchini kuwajengea uwezo wa kitaaluma wananchi katika masuala ya utafutaji,  uendelezaji,  uchakataji,  usafirishaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia. Naibu Waziri Mgallu alisema, “Kwa mfano mwaka 2010 Kampuni ya Petrobras ilitumia dola za kimarekani 350,000 sawa na shilingi milioni 780 kufundisha na kukipatia Chuo cha VETA Mtwara vifaa vya mafunzo. Aidha, kupitia mpango huo, wanafunzi 50 na wakufunzi 2 walifundishwa kwenye fani ya umeme na makanika”. Aidha, Kampuni ya Statoil imekuwa ikifadhili mafunzo mbalimbali kwa ngazi ya vyuo, ambapo mwaka 2013 ilif...

Rais Magufuli Awaonya Wanaosambaza Pembejeo HEWA

Rais Magufuli amekemea vikali watu wanaosambaza pembejeo hewa na amewataka waache kufanya hivyo kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo y Kauli hiyo imetolewa Aprili 11, kabla ya hajafungua barabara ya Mafinga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7 katika eneo la mtewele na uwanja wa Polisi –Makambako mkoani Njom “Mtu anadai amesambaza magunia kadhaa ya pembejeo wakati hayapo, hatuwezi tukaendelea na nchi yenye hewa kwa sababu hatuwezi kushiba hewa. “Nilipoingia madarakani niliahidi nitakuwa daktari wa kutumbua majipu zikiwemo hizi hewa ili fedha halali zitumike katika masuala mengine halali, ninajua wapo waliopata pembejeo za haki na tukishamaliza ufuatiliaji wa pembejeo watalipwa,” amesema. Aidha amewapongeza wakazi wa Mkoa huo kwa ujenzi mzuri wa nyumba ambapo ameitaka mikoa mingine kuiga mfano huo kwa kujenga nyumba nzuri na za kisasa. “Tangu nimeingia Njombe nimeona nyumba zilizojengwa ni tofauti na nyumba zilizonyengwa huko kwetu kwani hakuna nyumba y...

Wanne Watia Mbaroni Jijini Arusha kwa Kutengeneza Fedha Bandia

Picha
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng'anzi amesema jana Ijumaa Januari 18, 2019 kuwa watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia. Amesema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na noti bandia za dola za Marekani  zenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh 1.1 milioni). "Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," alisema Ng'anzi Fedha hizo ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda na Sudan. Alisema watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani. Katika tukio jingine, Ng'anzi amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina Harrier lenye namba za usaili T 241 DKC n...

Kigwangalla Aivunja Bodi ya Utalii (TTB)

Picha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amevunja bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuanzia jana Ijumaa na kutoa miezi mitatu kwa menejimenti kujirekebisha kinyume na hapo ataifumua. Waziri huyo ametangaza kuunda bodi mpya ya wakurugenzi ambayo itakuwa na wajumbe vijana watakaokwenda na kasi katika kazi hiyo ya kutangaza vivutio. Dk Kigwangalla amefikia uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa TTB imeshindwa kutekeleza maelekezo yake yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii. Akitoa uamuzi huo jana Ijumaa Januari 18, 2019 mbele ya waandishi wa habari Dk Kigwangalla ameeleza kutotangazwa kwa vivutio vya utalii kunaifanya Serikali inyooshewe kidole na kuonekana haifanyi kazi. Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ametoa maelekezo zaidi ya 15 lakini hayajafanyiwa kazi jambo linalosababisha yeye kutukanwa. “Serikali ikitukanwa kwenye sekta ya maliasili na utalii maana yake natukanwa mimi naonekana sitoshi kwenye nafasi hii, “ amesema Dk Kigwangalla. Miongon...

Rais Magufuli: Changamoto Zilizopo Sasa Zisipotatuliwa, Sidhani Kama Ajaye Atazitatua

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.   Magufuli ameyasema hayo jana  Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Alisema katika safari ya kutatua changamoto anakutana na magumu mengi na ndiyo maana amekuwa akihitaji nguvu za Mungu kutekeleza majukumu yake. “Viongozi wa dini endeleeni kuliweka Taifa hili kwenye mikono ya Mungu. Hii ni vita kama ilivyo nyingine na vita ya uchumi inahitaji maombi sana, bila maombi kazi hii haiwezi kufanyika,” alisema. “Hao wanaokaa gizani hauwezi kujua ana kisu, ana panga au ameweka nyoka mfukoni lakini huko gizani huwa wanatolewa kwa maombi, yatawapumbaza huko gizani wasitake kufanya walichokusudia.” Alisema kufanya hivyo kutawafanya viongozi wa nchi kusimamia misingi ya uadilifu na up...