Machapisho

MKUU MPYA WA WILAYA YA HAI LENGAI OLE SABAYA AAPISHWA KILIMANJARO LEO

Picha
Na Dixon Busagaga wa Globu  ya Jamii, Kanda ya Kaskazini MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya katika hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai. Mkuu mpya wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (hayupo pichani) ,Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akitia saini katika karatasi ya Kiapo mara baada ya kuapa kushika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) akitia saini katika karatasi ya kiapo,mbele yake ni...

Umri sahihi wa kufunga ndoa ni huu hapa

Picha
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Utah kilichopo nchini Marekani imebainisha kwamba watu ambao wamefunga ndoa kati ya umri wa miaka 28 mpaka 32 wamekuwa na ndoa yenye mafanikio zaidi. Utafiti huo umebainisha kwamba ndoa ambazo zipo katika hatari ya kuvunjika ni zile ambazo mmoja wa wanandoa ana umri wa chini ya miaka 20 na wale waliofunga ndoa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 45 na kuongeza kuwa ndoa hizo hazijadumu zaidi ya miaka mitano. Taarifa za utafiti huo umeongeza kuwa kwa watu ambao wanasubiri kufika umri wa miaka 30 ili kufunga ndoa wanahatari ya kupata shida sana katika miaka mitano ya mwanzo ya ndoa yao Awali ilijulikana kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri mkubwa ndiyo wananafasi ndogo ya kuachana, lakini utafiti huu umeonesha kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri wa miaka 45 uwezekano wa kupeana taraka unaongezeka kwa asilimia 5 kila baada ya mwaka mmoja. Sababu kubwa inayosababisha watu walio katika umri mkubwa kupeana taraka ni historia za nyuma za kila m...

Dalili za awali za ugonjwa wa figo na jinsi ya kuweka figo zako katika afya bora

Picha
Figo zina majukumu muhimu sana katika mwili wa binadamu- kwanza inaondoa sumu kutoka mwili wa binadamu na kusafisha damu na kutoa sumu zote. Kama figo haifanyi kazi vizuri, basi hii inaweza kusababisha mkusanyiko wa sumu katika mwili na inaweza kusababisha baadhi ya matatizo makubwa ya afya. Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo na jinsi ya kuweka figo zako katika afya nzuri Figo inafanya kazi nyingi muhimu katika mwili wa binadamu 1. Kuweka katika uwiano mzuri kiwango cha maji Figo ina uwezo wa kusawazisha kiwango cha maji katika mwili wa binadamu,na pia inashiriki katika kutoa kemikali kwa njia ya mkojo 2. Kutoa taka mwilini Sisi sote tunajua moja ya kazi kuu za figo ni kusafisha mwili, kutoa sumu,chumvi na urea 3. Kusimamia kanuni za damu Kama kiwango cha oksijeni kitakuwa chini katika figo, itasababisha kuundwa kwa erythroprotein, homoni ambayo inachochea marrow katika mifupa(bone marrow) 4. Kusimamia Kanuni za asidi Hii ni muhimu sana katika kazi za figo, figo zinawajib...

Sugu Atinga Rasmi Bungeni....Wapinzani Walipuka kwa Furaha

Picha
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, ameingia bungeni kwa mara ya kwanza leo Mei 21, 2018 tangu aachiwe kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10 mwaka huu. Baada ya kuingia bungeni, wabunge wa upinzani walilipuka kwa furaha wakimshangilia huku wakigonga meza zao kwa takriban dakika mbili, hali iliyosimamisha shughuli za Bunge kwa muda. Sugu ameingia ukumbini saa 3:20 asubuhi akiwa ameambatana na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Kunti Yusuph ambaye alisikika akisema: "Leo bungeni ni Sugu tu." Wakati anaingia, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege alikuwa anajibu maswali ya wabunge, lakini akalazimika kunyamaza kwanza. Sugu alikwenda moja kwa moja kwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na kumpa mkono kisha  kwa  waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu,  Jenister Mhagama na kumpa mkono. Alielekea kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Ut...

Anachotarajia Shaffih Dauda baada ya mabadiliko Simba

Picha
Jumapili Mei 20, 2018 klabu ya Simba imefanya mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya mabailiko ya katiba yao ili kuendana na mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo. Wanachama wa Simba kwa pamoja wamepiga kura ya ndio kupitisha mabadiliko ya katiba yao ili kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu ambapo kuanzia sasa klabu hiyo itaendeshwa kwa mfumo wa hisa. Mwekezaji Mohammed Dewji amechukua hisa asilimia 49 na wanachama wengine wamebaki na hisa 51%. Baada ya mabadiliko hayo ya mfumo na katiba ndani ya Simba, Shaffih Dauda amesema tatizo la vilabu vya Simba na Yanga sio mfumo tatizo ni watekelezaji wa mfumo husika. “Tatizo la Simba na Yanga siamini kama ilikuwa ni mfumo uliokuwepo, mfumo si tatizo wanaoingia kwenye mfumo kwa ajili ya utekelezaji ni akina nani? “Mfumo unaweza ukabadilishwa lakini inapokuja suala la utekelezaji hapo ndio kwenye tatizo. Ukifuatilia vizuri sio tatizo kwenye mpira peke yake, ‘human capital’ ni tatizo kubwa la nchi.” “T...

Mambo 5 waliyoazimia Viongozi wastaafu Afrika

Picha
KONGAMANO la Kikanda la Viongozi Wastaaafu wa Afrika limeazimia mambo makuu matano ikiwamo la kuwataka viongozi walio madarakani kuimarisha mifumo yao ili kusaidia kulinda amani na kuzuia migogoro. Kongamano hilo lililoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, lilihudhuriwa  na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na washiriki wengine kutoka  taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa zinazojihusisha na masula ya usalama na kulinda amani.  Akisoma mazimio hayo jana jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa chuo cha Uongozi, Gerase Kamugisha, alitaja maazimio hayo kuwa ni kuimarisha taasisi za kanda na Umoja wa Afrika zenye jukumu la kujenga na kulinda amani. Alitaja aazimio lingine kuwa ni kuongeza uratibu, ushirikiano na mashauriano miongoni mwa taasisi za kitaifa, kikanda na bara zima zinazohusika na juhudi za kuzuia migogoro au kulinda amani ikiwamo kuimarisha mifumo ya ushirikiano baina ya Baraza la Amani...

Hizi ndio sababu za Dewji kupewa Simba

Picha
Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa Mwanasheria wake Evodius Mtawala, leo imeweka wazi sababu za mshindi wa zabuni ya kuwekeza kwenye klabu hiyo Mohamed Dewji, kupewa asilimia 49 ya hisa tofauti na 51 kama alivyotaka yeye. Mtawala ameyasema hayo ikiwa ni siku chache zimebaki kuelekea kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo Mei 20 ambapo wanachama wataamua iwapo wanapitisha katiba mpya yenye kuruhusu mfumo wa hisa au la. ''Kwanza wanachama wanatakiwa kufahamu kuwa tayari  Mohammed ‘Mo’ Dewji amekubali kununua asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba SC na sio 51 kama aliyoomba awali na hii ni kwasababu ya kanuni na maelekezo ya Serikali'', amesema. Mwanasheria huyo ambaye amewahi kuwa katibu wa Simba ameongeza kuwa wao kama klabu walikuwa tayari kuuza asilimia 50 mpaka 51 kwa bilioni 20 alizotoa Mo Dewji lakini baadae serikali iliagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja. Kwa upande wa wanachama, Mtawala amesema watamiliki hisa ndani ya kampuni ya 'Simba ...