IGP Sirro Kupeleka Magari Mawili uya Polisi Pwani
Inspekta Jenerali was Polisi IGP Simon Sirro akipokea salaam ya heshima kutoka kwa askari was Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. IGP amewataka askari wa Mkoa wa Pwani kutoa huduma bora na kuendelea kuimarisha nidhamu ili wananchi waendelee kuwa na imani na Jeshi la Polisi. Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Sirro akikagua baadhi askari wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Sirro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng, Evaristi Ndikilo alipowasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. IKIWA ni siku chache baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini ya dar es Salaam na kukagua magari ya polisi ambayo yaliingizwa nchini mwaka 2015, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema kwamba magari mawili atayapeleka mkoani Pwani. Rais Magufuli alibaini ukwepo kwa magari zaidi ya 50 yakiwa...