Machapisho

Kwa Mara ya Kwanza Dogo Janja Afunguka Kuhusu Ndoa Yake na Irene Uwoya

Picha
HABARI zilizoenea katika mitandao ya kijamii ni kwamba msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja, amefunga ndoa kimyakimya na mnyange wa filamu, Irene Uwoya. Baada kuenea kwa uvumi huo, mtandao wa Global Publishers ulifuatilia kujua ukweli juu ya ndoa hiyo iliyowashitua wengi. Hatua ya kwanza jana ni pale mwandishi wa mtandao alipowaendea wahariri wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers yanayohusiana na habari za wasanii wa Bongo Muvi, Bongo Fleva na wengineo ambapo walijibu kwamba walikuwa wamemtafuta msanii Hamad Aly ‘Madee’ aliyewajibu kwamba alikuwa hajui chochote kuhusu suala hilo. Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja. Mambo hayakuishia hapo kwani wahariri haohao walipowasiliana na Dogo Janja alijibu kwamba na yeye hakujua kinachoendelea. Mwishoni wahariri wakamalizia kwa kuongea kwenye simu na Irene Uwoya ambapo alipopokea aliulizwa kuhusu suala hilo la kufunga ndoa na Dogo Janja.  Jibu la kwanza la mrembo huyo lilikuwa ni: “Mimi ni wa k...

Hivi ndivyo Bondia Muingereza, Antony Joshua Alivyomgalagaza Mfaransa

Picha
Jana usiku kulikuwa na pambano kubwa la masumbwi kati ya Bondia Muingereza, Antony Joshua na bondia  Carlos Takam kutoka Cameroon. Ambapo Joshua alimaliza pambano kwa kumtwanga Takam kwa TKO iliyoleta utata kwa mashabiki. Joshua alipata ushindi wa TKO kunako raundi ya 10 kwa refa kusimamisha pambano hilo baada ya Takam kuvuja damu nyingi usoni. Watu wengi waliohudhuria kwenye pambano hilo walimzomea mwamuzi wa pambano hilo wakidai Takam alikuwa bado ana nguvu ya kupambana japokuwa alikuwa amepasuka usoni. Mashabiki wengi wa Takam wanasema refa angempa muda bondia huyo kufutwa damu ili aendelee na pambano kwani alikuwa bado na nguvu za kurusha ngumi hivyo wanaamini mwamuzi huyo alimaliza pambano kwa matakwa. Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mpambano huo, Anthony Joshua amesema kama pambano lingeendelea angemuumiza zaidi Takam hivyo maamuzi ya refa yalimuokoa . Huu unakuwa ni ushindi wa 20 mfululizo kwa Antony Joshua (28) baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa ...

Aliyekuwa Kiongozi wa Catalonia Anaweza Kugombea Tena

Picha
Serikali ya Uhispania inasema kuwa inakaribisha kushiriki kwa kiongozi aliyefuwa wa Catalonia Carles Puigdemont kwenye uchaguzi mpya. Serikali ya Madrid imeamrisha kuwa uchaguzi mpya kwa bunge la eneo la Catlonia utafanyika mwezi Disemba. Madrid ililivua eneo la Catalonia utawala wake baada ya bunge la Catalonia kupiga kura ya kujitangazia uhuru, Bwana Puigdemont amewashauri watu kukataa udhibiti kamili kutoka Madrid. Waziri mkuu wa Uhispania avunja bunge la Catalonia Barcelona watakuwa wapi Catalonia ikiwa huru? Alilaani kufutwa kwa utawala wa Catalonia na kuahidi kuendelea kufanya kazi ya kujenga nchi ili huru. Wakati huo huo mamia ya raia wa Uhispania wamekusanyika katika mji mkuu Barcerlona kuunga mkono umoja wa Uhispania. Aidha Uhispania inaendelea kushinikiza kuchukua udhibiti wa nguvu dhidi ya serikali ya jimbo la Catalonia, iliyofutiliwa mbali.

Yaya Toure Adai Furaha Yake ni Kushinda Taji la Ligi Kuu ya Mabingwa Barani Ulaya

Picha
Nyota wa Manchester City Yaya Toure amesema anatamani kutwaa ubingwa wa UEFA akiwa na timu hiyo ili kukamilisha ndoto yake. Toure amedai furaha pekee anayoitamani ndani ya kikosi cha Manchester City ni kushinda taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya kwani  ndio kombe pekee ambalo hajafanikiwa kutwaa akiwa Etihad. Yaya Toure hadi sasa ametwaa makombe mawili ya EPL, mawili ya EFL pamoja na moja la FA hivyo anaona kama hadaiwi chochote kutoka nchini England zaidi ya ubingwa wa Ulaya. Raia huyo wa Ivory Coast ameshawahi kutwaa ubingwa wa UEFA akiwa na FC Barcelona mwaka 2009, hivyo anahitaji taji lake la pili la Ulaya.

Fahamu namna ya kufuta meseji ya WhatsApp uliyomtumia mtu kimakosa

Picha
Je umewahi kutuma ujumbe, picha au video kimakosa katika mtandao wa whatsapp? Fikiria umetuma ujumbe kimakosa kwa baba yako wakati ulilenga kumtumia mpenzi wako, utajisikiaje? huwa unakuwa na hali gani? je utamuelezaje kuwa hukulenga kumtumia yeye? Kumekuwa na kesi kadha wa kadha ambazo watu wanaoheshimika kukosea kutuma jumbe kimakosa jambo ambalo linawafanya wapoteze heshima mbele ya jamii inayowazunguka. Mwaka mmoja uliopita mchungaji wa kanisa moja huko Afrika Kusini alijinyonga baada ya kutuma kimakosa picha za utupu katika kundi la WhatsApp (WhatsApp group) la waumini wake, aliyolenga kumtumia mpenzi wake (mchepuko) kumtaarifu kuwa mke wake hayupo. Mtandao wa WhatsApp umeleta chaguo ambalo sasa watumiaji wanaweza kufuta ujumbe walioutuma kimakosa ambao mpokeaji hatauona, ila atapata taarifa kuwa ujumbe huo umefutwa. Utaweza kuufuta ujumbe ulioutuma kimakosa kabla ya dakika saba kuisha tokea ujumbe ulipotumwa. Baada ya dakika saba kuisha haitowezekana tena kuufuta. Ili kuwez...

Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Picha
Siku kama ya leo, Oktoba 29, 1959, Rais John Pombe Magufuli alizaliwa.  Mpekuzi Blog inakutakia  heri ya siku ya kuzaliwa. Tunakuombea Mungu akulinde, akupe afya njema na kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha uongozi wako.

Kidato Cha NNE Kesho Wataanza Mitihani Ya Mwisho ya Taifa.....Katibu Mkuu NECTA Awaasa Kutojihusisha na Udanganyifu

Picha
Watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kutafanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne nchini. Akizungumza leo Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa hao, 323,513 ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea. Dk Msonde amesema mtihani huo utaanza kesho Oktoba 30,2017 hadi Novemba 17,2017. Dk Msonde amesema maandalizi ya mitihani yameshakamilika."Hivi ninavyozungumza mitihani imeshafika kwenye vituo.” Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unafuatwa. Katibu mtendaji huyo amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo. "Mliyojifunza yanatosha fanyeni mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa," amesema. Dk Msonde amesema baraza hilo halitasita kuwafutia mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu.