Machapisho

Sunderland yashuka daraja rasmi

Picha
Baada ya kuandamwa na matokeo mabovu kwa muda mrefu, hatimaye Sunderland wameshuka daraja kwa mara ya nne katika ligi kuu ya Uingereza Epl. Sunderland walikuwa uwanja wao wa nyumbani wa Stadium of Light wakati wakiikaribisha timu ya Fc Bournemouth na mashabiki wao waliamini wanaweza pata matokeo katika mchezo huo. Alikuwa Joshua King aliyeweka machozi kwenye mashavu ya mashabiki wa Sunderland kwani bao lake dakika ya 88 liliwaonesha Sunderland mlango wa kutokea Epl. Baada ya mchezo huo, kocha wa Sunderland David Moyes alisema hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo bali anataka kupambana ili kuirudisha tena ligi kuu. “Sunderland watapambana tena na nina uhakika katika hilo, kwa sasa inatupasa kuwa kitu kimoja kuanza kuweka mipango yetu pamoja ili turudi tena msimu ujao” alisema Moyes Katika michezo mingine goli la Jamie Vardy aliwapa ushindi Leicester dhidi ya Westbrom, Southampton na Hull City wakatoka suluhu ya bila kufungana kama ilivyo kwa Stoke City na West Ham....

Simba Yaingia Fainali, Yaiadhibu Azam 1 - 0 Kombe la Shirikisho

Picha
SIMBA SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linalojulikana kama Azam Sports federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 48, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu baadaye.  Kwa ushindi huo, Simba itasubiri kukutana na mshindi kati ya wenyeji Mbao FC na Yanga SC zinazomenyaa kesho Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, Azam FC ilipata pigo dakika ya 15 baada ya kiungo wake mchezeshaji, Salum Abunakar ‘Sure Boy’ kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib. Ilionekana kama wachezaji hao wamegongana kwa kawaida mno, lakini kwa namna Hajib alivyojirusha huku akipiga yowe la kuugulia maumivu Akrama aliingia kwenye mtego wa...

BUNDA: Orodha ya majina ya watumishi wa umma wenye vyeti feki (W) BUNDA

Picha

Rais Dkt Shein azindua Msikiti Masjidi Madinatul Munawara Kijiji cha Donge Kitaluni

Picha
Pichani jengo la Msikiti Masjidi Madinatul Munawara katika Kijiji cha Donge Kitaluni Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja uliojengwa kwa ufadhili wa Bibi Latifa Shehab Albreiki Nchini Dubai ambapo umezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,chini ya Usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi,[Picha na Ikulu.] 28/04/2017. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Donge,pia Waziri wa Fedha na Mipango Mhe,Dkt.Khalid Salum Mohamed wakati alipowasili katika viwanja vya Msikiti Masjidi Madinatul Munawara katika Kijiji cha Donge Kitaluni Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja leo alipofika kuuzindua msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa Bibi Latifa Shehab Albreiki Nchini Dubai,chini ya usimamizi wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi,[Picha na Ikulu.] 28/04/2017. ...

Shaffih Dauda: Kikosi changu bora cha Simba na Azam 

Picha
Kuelekea pambano la nusu fainali kati ya Simba na Azam, mchambuzi mkongwe wa masuala ya soka Tanzania Shaffih Dauda ametaja kikosi chake bora. Shaffih ametaja kikosi cha wachezaji anaowaona bora ambao walizichezea timu zote mbili kwa nyakati fulani na wengine wamestaafu soka huku wengine hawapo timu yoyote kati ta hizo mbili. Golini Shaffih ameamua kumuweka golikipa wa Yanga Deogratius Munishi “Dida” ambaye kabla ya kutua Yanga ameshawahi kuzitumikia Azam na baadae Simba. Beki wa kushoto ni Mohameid Hussein wa Simba ambaye alikulia wakati flani katika timu ya Azam, huku mlinzi wa kulia ni Shomari Kapombe ambaye sasa yuko Azam lakini hapo kabla alikuwa Simba. Walinzi wa katikati yupo mkenya Owino na beki wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania Boniface Pawasa ambaye kwa sasa amestaafu kucheza soka. Katika mfumo wa Shaffih ambao ni 4 – 3 – 3 katikati ameweka viungo watatu ambapo kiungo wa katikati ni marehemu Patrick Mafisango akizungukwa na Seleman M...

HUU ndio Mjengo Matata wa Bilioni 264 Alionunua Jay Z kwa Ajili ya Watoto Wake Mapacha ..!!

Picha
UPENDO wa familia ni watoto na wakati wote wanapopatikana, wazazi huwa na furaha kwa kuwaandalia sehemu nzuri, huku wakiwekewa mipango kadha wa kadha kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. Mkali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Shawn Carter ‘Jay-Z’ na mke wake, Beyonce, wameonyesha namna wanavyoandaa maisha bora ya watoto wao mapacha wanaowatarajia hivi karibuni. Wakali hao wa muziki duniani wametumia dola milioni 120, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 264 za Kitanzania kununua nyumba kwa ajili ya watoto hao mapacha wawili. Wapenzi hao, ambao ndoa yao ina mvuto mkubwa na mfano wa kuigwa na mastaa wengi duniani, wametumia kiasi hicho cha fedha kuwanunulia nyumba yao ili watoto hao wakizaliwa waikute. Eneo la nyumba hiyo lina ukubwa wa eka mbili na linalindwa na ulinzi mkali kwa ajili ya usalama wa mali zilizopo ndani ya eneo hilo. Inasemekana kuwa, madirisha ya nyumba hiyo yamefungwa vifaa maalumu kwa ajili ya kuzuia kushambuliwa na risasi. Nyumba hiyo ina jumla ya vyumb...

KUTANA na Familia Isiyozeeka..Baba na Mama Wanamiaka 47 lakini Wapo Kama Vijana wa Miaka 17..!!!

Picha
FAMILIA ya Kichina imebamba katika mitandao ya jamii baada ya kuonekana haina dalili za kuzeeka kwa mujibu wa picha zao. Msichana mmoja anayetumia jina la sysev7n  mtandaoni, alikuwa akisafisha picha za baba yake katika nyumba yao huko Chengdu. Akiwa katika harakati hizo za usafi aliona kitu cha kushangaza katika picha hizo zile za zamani na za sasa. Alilinganisha na picha zilizochukuliwa hivi karibuni na zile za zamani wakati wa utoto wake, akabaini kwamba wazazi wake wana mwonekano ule ule, yaani hawajazeeka. Kufuatia ugunduzi wake huo, akazirusha katika akaunti yake kwenye mtandao wa jamii wa Kichina ujulikanao kama Weibo. Picha hizo hazikuchukua muda kuwa gumzo kwa watumiaji wa mtandao kwamba familia hiyo imejaaliwa utajiri wa ujana, kwa mujibu wa mtandao wa People's Daily Online. Mama na baba wote wana umri wa miaka 47. Picha ya baba wa mwanamke huyo, akiwa amepozi naye alipokuwa mdogo, ambayo ilipigwa miaka 18 iliyopita, ilionesha baba yake hajazeeka hata kidogo na yu...