Kudadeki..Kumbe Daraja la Kigamboni Linaingiza Pesa Ndefu Kiasi Hiki..!!?
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, katika daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Makusanyo hayo, imeelezwa, ni kuanzia katikati ya Mei, mwaka jana hadi mwezi huu na ni juu ya lengo kwa asilimia 20. NSSF inakuwa taasisi ya pili ndani ya wiki moja kutangaza mapato ya mradi, baada ya Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kufanya hivyo Alhamisi. Akizungumza na Nipashe jana juu ya maendeleo ya mradi wa daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema limeingiza jumla ya Sh. bilioni sita. Aidha, Prof. Kahyarara alisema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu. Prof. Kahyarara alisema NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya wakala. Alisema awali makaridio yalikuwa ni kukusanya Sh. bilioni tano katika kipindi hicho. “Sera yetu ni kwamba hizi fedha hat...