Machapisho

Kudadeki..Kumbe Daraja la Kigamboni Linaingiza Pesa Ndefu Kiasi Hiki..!!?

Picha
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, katika daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Makusanyo hayo, imeelezwa, ni kuanzia katikati ya Mei, mwaka jana hadi mwezi huu na ni juu ya lengo kwa asilimia 20. NSSF inakuwa taasisi ya pili ndani ya wiki moja kutangaza mapato ya mradi, baada ya Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kufanya hivyo Alhamisi. Akizungumza na Nipashe jana juu ya maendeleo ya mradi wa daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema limeingiza jumla ya Sh. bilioni sita. Aidha, Prof. Kahyarara alisema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu. Prof. Kahyarara alisema NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya wakala. Alisema awali makaridio yalikuwa ni kukusanya Sh. bilioni tano katika kipindi hicho. “Sera yetu ni kwamba hizi fedha hat...

Daktari Aandika Barua ya Kuacha Kazi Baada ya Mkuu wa Mkoa Kumuweka Rumande Kwa Kosa la Kipindupindu

Picha
Mganga  Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, Dk. Erick Bakuza ameandika barua ya kuacha kazi Dk. Bakuza amechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache tangu alipopewa adhabu ya kuwekwa mahabusu na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi. Dk. Nchimbi alitoa amri ya kukamatwa kwa daktari huyo kutokana na kuzuka ugonjwa wa kipindupindu ambao ulisababisha vifo vya watu wawili mwishoni mwa mwaka jana. Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rashid Mandoa jana alithibitisha kuacha kazi kwa Dk. Bakuza. “Ni kweli amewasilisha barua ya kuacha kazi lakini ninavyojua mimi si kweli kwamba ameacha kazi kutokana na adhabu aliyopewa na Mkuu wa Mkoa ya kuwekwa ndani. “Kwanza ujue hakuwekwa ndani, na ameamua kuacha kazi kwa sababu amepata sehemu nyingine ambayo anaona ina maslahi anayohitaji yeye,” alisema. Juhudi za kumpata Dk. Bakuza kuzungumzia hatua yake hiyo hazikuzaa matunda. Kauli ya Mkuu wa Mkoa Wakati Mkurugenzi huyo akisema kwamba Dk. Bakuza hakuwekwa ndani, Mkuu wa Mkoa huyo, Dk. ...

Golikipa David Burhan wa Kagera Sugar, afariki dunia

Picha
Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za bongo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo. "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani" Marehemu David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es Salaam, Abdallah Buruhan.

Ubuyu wa Moto Moto.. Penzi la Tunda Ladaiwa kumkosesha Dogo Janja Usingizi..!!!

Picha
Kwa wapenzi wote wa ubuyu, tena ubuyu mtamu, basi hapa ndipo penyewe! Ubuyu uliotufi kia mubashara unatonya kuwa video queen aliyeuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian anadaiwa kumkosesha usingizi staa wa Manzese Music, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni mapenzi aliyonayo kwake. KUMBE NDIYO CHANZO CHA BIFU! Chanzo makini kilitoa ubuyu wa motomoto kuwa, Dogo Janja au Janjaro anayekimbiza na Ngoma ya Kidebe, amekuwa akiteseka kutokana na mapenzi aliyonayo kwa Tunda japokuwa waliwahi kuwa wapenzi zamani. Inadaiwa kuwa, haijulikani Tunda alimpa nini Dogo Janja lakini ukweli ni kwamba anatamani kuwa naye tena na ndiyo chanzo cha bifu lake la mara kwa mara na mwandani wa Tunda ambaye naye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’. “Unaambiwa Dogo Janja hapati usingizi kwa sababu ya penzi alilonalo kwa Tunda. “Kama utakuwa unamfuatilia, amekuwa akiandika kwenye ukuras...

ANGALIA PICHA MADHARA YA KUJICHUBUA

Picha
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao. Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge. Madhara ya kujichubua ni yapi? Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi,  chunusi,  uvimbe katika ngozi,  ngozi kuwa nyembamba, Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito, kutokwa na mabaka,  pumu,  kupata watot...

ALI KIBA YAZINGATIE MALALAMIKO YA MASHABIKI WAKO

Picha
Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act. Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda. Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria. Ushindi wa MTV EMA pia am...

Maalim Seif Ajipa Matumaini ya Kuwa Rais wa Zanzibar Siku Moja.Haya Ndiyo Aliyoenda Kuwaambia Marais wa Dunia Kuhusu Zanzibar..!!!

Picha
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad bado anaamini atakuwa Rais wa Zanzibar akidai kwamba nchi alizopeleka malalamiko yake zimefikia katika hatua nzuri. Tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2015, Maalim Seif amekuwa akitoa kauli za matumaini akisema: “Mambo yaelekea kuwa mazuri.” Hata hivyo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyeshinda katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016 ambao Maalim Seif aligoma kushiriki, amekuwa akisema kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumwondoa madarakani, awe wa ndani au nje ya nchi. Akizungumza katika kipindi cha Funguka kinachoendeshwa na Tido Mhando kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema wananchi wasifikiri kuwa mataifa hayo yamenyamaza, bali suala hilo litapatiwa ufumbuzi na atapata haki yake hivi karibuni.