KAMA USAJILI WA EURO MIL 90 WA HIGUAIN JUVE NI KWA AJILI YA UEFA, BASI WAMETUPA PESA ZAO
Na Mahmoud Rajab Pesa, pesa, pesa. Pesa ni kitu cha ajabu sana hapa ulimwenguni. Inaweza kufanya chochote kile kwa mantiki ya kutimizwa matakwa fulani. Katika soka ndiyo usiseme, imekuwa ni kama makaratasi tu, zinatolewa ovyo kwa nia ya kupata saini za wachezaji mbalimbali. Hivi inawezekanaje Juventus kutoa fedha nyingi kiasi hiki kumsajili Gonzalo Higuain, wakidhani kwamba ni mtu sahihi kuwapa taji la Uefa? Nini hasa kimewashawishi Juventus kuona kwamba Higuain ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo? Juve wametoa kiasi cha euro mil 90 kumsajili Higuain kutoka klabu ya Napoli. Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis alisema kwamba ni kichaa pekee ambaye anaweza kutoa kiasi hicho cha pesa kufanya usajili huo, Sasa yametimia. Je, Juventus wameamua kucheza ‘pata potea’ kwenye usajili huo wa Higuain? Higuain ameamaliza kiu ya muda mrefu ya Juventus kutafuta mtu mwenye makali mbele ya lango. Hilo ni sawa kabisa. Wamekosa mtu ambaye anaweza kuwa mfungaji bora kwenye ligi kwa takriba...