Machapisho

KAMA USAJILI WA EURO MIL 90 WA HIGUAIN JUVE NI KWA AJILI YA UEFA, BASI WAMETUPA PESA ZAO

Picha
Na Mahmoud Rajab Pesa, pesa, pesa. Pesa ni kitu cha ajabu sana hapa ulimwenguni. Inaweza kufanya chochote kile kwa mantiki ya kutimizwa matakwa fulani. Katika soka ndiyo usiseme, imekuwa ni kama makaratasi tu, zinatolewa ovyo kwa nia ya kupata saini za wachezaji mbalimbali. Hivi inawezekanaje Juventus kutoa fedha nyingi kiasi hiki kumsajili Gonzalo Higuain, wakidhani kwamba ni mtu sahihi kuwapa taji la Uefa? Nini hasa kimewashawishi Juventus kuona kwamba Higuain ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo? Juve wametoa kiasi cha euro mil 90 kumsajili Higuain kutoka klabu ya Napoli. Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis alisema kwamba ni kichaa pekee ambaye anaweza kutoa kiasi hicho cha pesa kufanya usajili huo, Sasa yametimia. Je, Juventus wameamua kucheza ‘pata potea’ kwenye usajili huo wa Higuain? Higuain ameamaliza kiu ya muda mrefu ya Juventus kutafuta mtu mwenye makali mbele ya lango. Hilo ni sawa kabisa. Wamekosa mtu ambaye anaweza kuwa mfungaji bora kwenye ligi kwa takriba...

KUTANA NA MTAALAM WA I.T MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE DUNIANI

Picha
Ayan Qureshi. Wazazi wengi Afrika wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba na vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa. Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu. Katika mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibi...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 31

Picha

MBOWE AONGOZA WAOMBELEZAJI KATIKA MAZIKO YA BABA MZAZI WA DEVOTHA MINJA MBUNGE WA VITI MAALUM LEO

Picha
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa jimbo la Hai, Mhe. Freeman Mbowe leo Jumamosi 30/07/2016 ameongoza maelfu ya waombolezaji waliofika kumzika Baba wa Devotha Minja ambaye ni Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA, marehemu Mathew Minja amezikwa nyumbani kwake Rauya Koteno Marangu mkoani Kilimanjaro. Maziko hayo yamehudhuriwa pia na viongozi mbalimba. Kati ya viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Godbless Lema, Mbunge wa viti maalum Arusha mjini, Mhe. Joyce Mukya, Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini, Mbunge wa Karatu, Mhe. Cecilia Pareto na Mhe. Grace Kiwelo. Akiongea kwa niaba ya Chama cha Chadema, wabunge, wanachama na kutoa salamu za rambi rambi,Mhe. Mbowe ametoa pole nyingi kwa familia ya Mzee Mathew Minja kwa msiba huo mkubwa. "Kila mtu atakufa na kila siku kifo kikitokea tunajifunza jambo, tukikutana kwenye misiba tunakuwa wanyenyekevu, wapole, watulivu tuliojawa huzuni na h...

MUGABE AWATISHIA WAMAREKANI,AMTAJA TRUMP ..!!!

Picha
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba. Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba alikubali kuonana nao. Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa. Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''.

STAA ALI KIBA AANZA KUSHOOT REMIX"AJE"AKIWA NA M.I

Picha
Mkali wa wimbo ‘Aje’ AliKiba baada ya kufanya vizuri na original version ya wimbo huo, ameweka kambi nchini Afrika Kusini kuandaa remix ya wimbo huo akiwa amemshirikisha msanii wa Nigeria, M.I. Awali kolabo hiyo ya ‘Aje’ akiwa na M.I ilivuja katika mitandao ya kijamii wakati haijamalizika hali ambayo ilimfanya kuachia original version yake. Kwa mujibu wa video ya AliKiba iliyozagaa katika mitandao ya kijamii, inamuonyesha muimbaji huyo akiwa location Africa Kusini huku akizungumza project hiyo. “Tunashoot video, ‘Aje remix’ video nikuwa na M.I,” alisema AliKiba. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini, amedaiwa kushoot video mbili mpaka sasa, moja ya kolabo yake na Barakah The Prince na nyingine ya kolabo yake na M.I.

RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA WILAYA ZA IGUNGA NA NZEGA MKOANI TABORA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini ...