Machapisho

Wafanyabiashara Wachina Kortini Kwa Kutorosha Noti za 500

Picha
Wafanyabiashara wawili raia wa China, Su Ning (39) na Feng Guang Quan (51) wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kusafirisha Sh30 milioni kwenda nchini China, bila kibali cha Gavana wa Tanzania. Washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha noti za shilingi miatanomiatano 60,000 kinyume na sheria ya ubadilishaji fedha na kwamba, kiwango hicho kilikuwa kimefungwa kwenye mabunda 40. Kila bunda moja lilikuwa na Sh500,000. Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, walikiri kutenda makosa hayo na Mahakama iliwasomea maelezo ya awali ambayo pia walikiri maelezo hayo, ikiwamo begi lililokuwa na mabunda 40 ya noti yenye thamani ya Sh20 milioni. Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, Wakili wa Serikali, Shadrak Kimaro akisaidiana na Estazia William walidai katika shtaka la kwanza, washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Agosti 15 na Agosti 31, mwaka jana. Ilidaiwa kuwa washtakiwa walikama...

Boss wa Clouds FM Ruge Akanusha Gerald Hando na PJ Kuacha Kazi...

Picha
MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,  leo kupitia kipindi cha Power Breakfast‬ amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ,  kuacha kazi. “Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi,  taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31.  Sehemu kubwa ya wafanyakazi  wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo  katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba.

Serikali ya Tanzania Kuingiza Nchini Ndege 2 za Kisasa Kutoka Canada Ndani ya Siku 60

Picha
Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano wa anga na Serikali ya Quwait.  Makubaliano hayo yatawezesha mashirika ya ndege ya nchi zote mbili kufanya safari za moja kwa moja na kukuza sekta ya utalii. Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi imethibitisha kwamba imeagiza ndege za kisasa kutoka nchini Canada ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini ndani ya siku 60 (miezi miwili ijayo). Kwa kuanzia, awamu ya kwanza ya ndege hizo zitafanya safari za ndani bara na visiwani kabla ya kujitanua ndani na nje ya Afrika. Shime watanzania, tusimame kidete na serikali yetu kuhakikisha kwamba tunaachana na unyonge wa kutumia ndege za mashirika ya nchi jirani. Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji katika sekta ya chakula, nishati, vinywaji n.k.

TRA Yakamata Magari Matano ya TFF Kutokana na Malimbikizo ya Kodi ya Bilioni 1.118

Picha
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi. TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao. Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo. “Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa. “Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari ...

EMMANUEL EBOU AFUNGIWA SOKA MWAKA 1 UINGEREZA

Picha
Na Amin Nyaungo Mlinzi wa Zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory coast Emanuel Eboue amefungiwa kwa miezi 12 kucheza mpira baada ya kugundulika kutomlipa pesa aliye kuwa Wakala wake alizokuwa anamdai. Eboue alikuwa Galatasalay ya uturuki kwa mara ya kwanza anarejea England tangu aondoke Arsenal, mlinzi huyo mpole mwenye miaka 32 alisajiliwa na Sunderland mwezi mmoja ulio pita na ilitakiwa aanze kuonekana wiki hii dhidi ya Westbromwich Albion Fifa wamesema wanaweza kutengua adhabu hiyo endapo Eboue atalipa deni lake analo daiwa

SIKU 7 ZA DKT SHEIN ZANZIBAR ZIMEKATIKA, ATAFUATA KAULI AU KATIBA?

Picha
Dkt. Shein aliapishwa kuwa Rais wa Zanzibar Alhamishi ya March 24, 2016 ambapo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar inamtaka awe amemtangaza Makamu wa Kwanza wa Rais katika kipindi cha siku saba tangu kuapishwa. Ingawa mpaka sasa ameshampata makamu wa pili wa Rais visiwani humo. Hali imekua Tofauti sana kwa Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Marudio Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein,  kwakuwa aliahidi anataka kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka miongoni mwa vyama 13 vilivyoshiriki katika uchaguzi huo uliosusiwa na chama cha wananchi CUF, pamoja na vyama vingine Saba. Dr Shein alitangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC,Jecha Salimu Jecha kuwa mshindi katika Uchaguzi huo kwa kupata asilimia 91.4 % ya Kura Zote zilizopigwa. Chama kilichofuatia kwa matokeo hayo ni Alliance for Democratic Change ADC, ambacho Mgombea wake Hamad Rashid Mohamed, alipata asilimia 3.0% ya kura zote. Kutokana na matokeo hayo, inaonesha kuwa hakuna chama cha Upinzani kilichofikisha aslimia 10% ya k...

Askari Polisi Anatafutwa Na Jeshi La Polisi Baada Ya Kugundulika Alijipatia Ajira Kwa Vyeti Vya Kugushi.

Picha
Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi aliamua kutoroka na hajulikani aliko. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol amefanya kazi ndani ya jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila kujulikana kuwa ana vyeti vya kugushi, Vielelezo vya kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo ni wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la polisi lina  taka kumfungulia mashitaka Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawaomba wanchi ambao watakuwa na tarifa za Emanuel Nyangoli watoe tarifa kwa kituo chochote cha polisi au apige kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Nomber 0715 009 956. ...