SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 27 Februari 2018

T media news

Jerry Muro Akoshwa na Kasi ya Okwi "Kwangu Mimi Okwi Ndiye Mchezaji Bora Chirwa Hawezi Mfikia Okwi"

Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameeleza mtazamo wake wa kuwa nani anaweza kuwa mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Muro amesema anampa nafasi kubwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kutokana na kiwango kizuri ambacho amekuwa akikionesha akiwa na Simba.

Mbali na hilo, Muro pia amemtaja mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa kuwa hawezi kumfikia Okwi, kwani kiwango chake si kama cha mwenzake.

Muro amesema Chirwa amekuwa akigoma kila wakati kuichezea hata timu yake, hivyo hampi na nafasi ya kuchuana na Okwi na akaenda mbali kwa kusema hastahili kulinganishwa naye.

"Kwangu mimi Okwi ndiye mchezaji bora kwa sasa, hauwezi ukamlinganisha na Chirwa ambaye amekuwa akigoma hata kuichezea Yanga, Okwi ni ''Real Proffesional" hivyo hawezi kufikiwa na Chirwa katika mbio za ufungaji bora" alisema Muro.

Okwi mpaka sasa amefikisha mabao 16 katika mechi 19 alizocheza msimu huu, wakati Chirwa ana mabao 11.