Taarifa iliyotolewa Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano na UMMA wa Chama Cha Waigizaji Kinondoni, Masoud Kaftany imewaomba wasanii na Watanzania kwa ujumla wao wajitokeze kumpokea Wastara kesho Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.
TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa
Tar : 26 /February/2018
YAH : MAPOKEZI
Chama Cha Waigizaji Kinondoni ( Tdfaa Kinondoni ) Kinapenda Kuwajulisha Wana-Filamu na Watanzania kuwa kutakuwa na mapokezi ya ndugu yetu na mwanatasnia mwenzetu, Bi Wastara Juma yatakayofanyika siku ya Alhamis ya tarehe 1 March, 2018 saa saba kamili mchana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Chama kinawajulisha na kuwaomba waigizaji na wadau wote wa tasnia ya filamu tujitokeze kwa wingi kumlaki muigizaji mwenzetu na mpendwa wetu Wastara Juma kwa furaha baada ya kufanikiwa katika matibabu yake nchini India katika Hospitali ya Saifee iliyoko Mjini Mumbai.
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU – PAMOJA TUNAJENGA TASNIA YETU..
Mungu amtie nguvu na amzidishie afya njema, Amin.
Masoud Kaftany
Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano na UMMA.
Chama Cha Waigizaji Kinondoni.