Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2018

DC ARUMERU AZUNGUMZA NA MADIWANI ARUSHA DC

Picha
Mkuu Wa wilaya ya Arumeru *Mh.Jerry Muro* amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji katika halmashauri hiyo. *Dc Muro* ameyasema hayo hii leo katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha ambapo amesema kuwa vipo vyanzo vingi vya mapato ambayo halmashauri hiyo inaweza kukusanya na kufika kiasi cha shilingi *billion kumi.* Licha ya kutoa agizo hilo akalazimik kutoa tahadhari ya kutolipwa posho pamoja na kuvunjwa kwa baraza la madiwani kutokana na wao kushindwa kukusanya mapato Mara baada ya kutoa agizo kwa baraza hilo La madiwani mwenyekiti wa halmashauri hiyo ndugu *Noah Lembris* amemsisitizia Mkuu wa Wilaya kuwa watazidi kufuata sheria zaidi ili kufikia maendeleo ya wananchi pamoja. Katika kikao hicho cha baraza la madiwani kimejadili pia changamoto mbalimbali ikiwemo miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo *Dr Wilson Charles Mahe...

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI AFRIKA(OATUU) LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA VITA DHIDI YA UFISADI NCHINI

Picha
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika**(OATUU**) lililokutana mjini Dar es Salaam,Tanzania kwa mkutano wa siku limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa mapambano ya dhati juu ya vitendo vya Rushwa na Ufisadi. Akisoma maazimio ya kikao hicho Katibu Mkuu wa *OATUU* *Cde Arzeki Mezhoud* amesema kwamba Tanzania ni kati ya nchi chache za mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya Rushwa Afrika na Rais Magufuli ni kielelezo wa Kiongozi anayechukia Rushwa kwa Vitendo na kwamba *OAATU* inamuunga mkono katika jitihada hizi na asijione yupo peke yake katika vita hii kubwa. Akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) *Mh Anthony Mavunde* kupokea maazimio hayo ya *OATUU* kwa niaba ya Serikali,Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania *(TUCTA)* Cde Tumaini Nyamuhokya amesema TUCTA inaunga mkono jitihada za serikali kupambana na Rushwa na muda wote itashirikiana na serikali katika mapambano hayo. Ai...

Makampuni yanayoajiri Vikongwe, kutoa mishahara midogo Kikaangoni

Picha
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa mwezi mmoja kwa Makapuni binafsi ya Ulinzi kuhakikisha yanarekebisha mfumo wao wa kuajiri pamoja na utoaji wa mishahara kabla ya Wizara yake haijaanza kuyahakiki makampuni hayo. Lugola amesema baadhi ya Makampuni hayo yameajiri wazee wasiojiweza ambao muda wote wanalala na wanasabaisha uhalifu kuendelea kwa kasi, wakati vijana wapo wengi wenye nguvu zao wanaweza wakazifanya kazi hizo kwa umakini zaidi, na pia tatizo lingine wanalipwa mishahara midogo hali hiyo inawafanya pia wajiingize katika uhalifu. Akizungumza na mamia ya wananchi mjini Bunda, mkoani Mara katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mjini hapo, Waziri Lugola alisema, Serikali ya awamu ya tano kamwe haitataka uzembe, hivyo makampuni hayo yanayovunja utaratibu huo siku zao zinahesabika. Lugola aliongeza kua, licha makampuni hayo yamekua yakiwekeza nchini na pia yanasaidia kufanya doria katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya miji, lakini yapo maen...

MKUU MPYA WA WILAYA YA HAI LENGAI OLE SABAYA AAPISHWA KILIMANJARO LEO

Picha
Na Dixon Busagaga wa Globu  ya Jamii, Kanda ya Kaskazini MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya katika hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai. Mkuu mpya wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (hayupo pichani) ,Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akitia saini katika karatasi ya Kiapo mara baada ya kuapa kushika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Hai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) akitia saini katika karatasi ya kiapo,mbele yake ni...

Umri sahihi wa kufunga ndoa ni huu hapa

Picha
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Utah kilichopo nchini Marekani imebainisha kwamba watu ambao wamefunga ndoa kati ya umri wa miaka 28 mpaka 32 wamekuwa na ndoa yenye mafanikio zaidi. Utafiti huo umebainisha kwamba ndoa ambazo zipo katika hatari ya kuvunjika ni zile ambazo mmoja wa wanandoa ana umri wa chini ya miaka 20 na wale waliofunga ndoa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 45 na kuongeza kuwa ndoa hizo hazijadumu zaidi ya miaka mitano. Taarifa za utafiti huo umeongeza kuwa kwa watu ambao wanasubiri kufika umri wa miaka 30 ili kufunga ndoa wanahatari ya kupata shida sana katika miaka mitano ya mwanzo ya ndoa yao Awali ilijulikana kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri mkubwa ndiyo wananafasi ndogo ya kuachana, lakini utafiti huu umeonesha kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri wa miaka 45 uwezekano wa kupeana taraka unaongezeka kwa asilimia 5 kila baada ya mwaka mmoja. Sababu kubwa inayosababisha watu walio katika umri mkubwa kupeana taraka ni historia za nyuma za kila m...

Dalili za awali za ugonjwa wa figo na jinsi ya kuweka figo zako katika afya bora

Picha
Figo zina majukumu muhimu sana katika mwili wa binadamu- kwanza inaondoa sumu kutoka mwili wa binadamu na kusafisha damu na kutoa sumu zote. Kama figo haifanyi kazi vizuri, basi hii inaweza kusababisha mkusanyiko wa sumu katika mwili na inaweza kusababisha baadhi ya matatizo makubwa ya afya. Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo na jinsi ya kuweka figo zako katika afya nzuri Figo inafanya kazi nyingi muhimu katika mwili wa binadamu 1. Kuweka katika uwiano mzuri kiwango cha maji Figo ina uwezo wa kusawazisha kiwango cha maji katika mwili wa binadamu,na pia inashiriki katika kutoa kemikali kwa njia ya mkojo 2. Kutoa taka mwilini Sisi sote tunajua moja ya kazi kuu za figo ni kusafisha mwili, kutoa sumu,chumvi na urea 3. Kusimamia kanuni za damu Kama kiwango cha oksijeni kitakuwa chini katika figo, itasababisha kuundwa kwa erythroprotein, homoni ambayo inachochea marrow katika mifupa(bone marrow) 4. Kusimamia Kanuni za asidi Hii ni muhimu sana katika kazi za figo, figo zinawajib...

Sugu Atinga Rasmi Bungeni....Wapinzani Walipuka kwa Furaha

Picha
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, ameingia bungeni kwa mara ya kwanza leo Mei 21, 2018 tangu aachiwe kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10 mwaka huu. Baada ya kuingia bungeni, wabunge wa upinzani walilipuka kwa furaha wakimshangilia huku wakigonga meza zao kwa takriban dakika mbili, hali iliyosimamisha shughuli za Bunge kwa muda. Sugu ameingia ukumbini saa 3:20 asubuhi akiwa ameambatana na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Kunti Yusuph ambaye alisikika akisema: "Leo bungeni ni Sugu tu." Wakati anaingia, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege alikuwa anajibu maswali ya wabunge, lakini akalazimika kunyamaza kwanza. Sugu alikwenda moja kwa moja kwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na kumpa mkono kisha  kwa  waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu,  Jenister Mhagama na kumpa mkono. Alielekea kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Ut...

Anachotarajia Shaffih Dauda baada ya mabadiliko Simba

Picha
Jumapili Mei 20, 2018 klabu ya Simba imefanya mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya mabailiko ya katiba yao ili kuendana na mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo. Wanachama wa Simba kwa pamoja wamepiga kura ya ndio kupitisha mabadiliko ya katiba yao ili kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu ambapo kuanzia sasa klabu hiyo itaendeshwa kwa mfumo wa hisa. Mwekezaji Mohammed Dewji amechukua hisa asilimia 49 na wanachama wengine wamebaki na hisa 51%. Baada ya mabadiliko hayo ya mfumo na katiba ndani ya Simba, Shaffih Dauda amesema tatizo la vilabu vya Simba na Yanga sio mfumo tatizo ni watekelezaji wa mfumo husika. “Tatizo la Simba na Yanga siamini kama ilikuwa ni mfumo uliokuwepo, mfumo si tatizo wanaoingia kwenye mfumo kwa ajili ya utekelezaji ni akina nani? “Mfumo unaweza ukabadilishwa lakini inapokuja suala la utekelezaji hapo ndio kwenye tatizo. Ukifuatilia vizuri sio tatizo kwenye mpira peke yake, ‘human capital’ ni tatizo kubwa la nchi.” “T...

Mambo 5 waliyoazimia Viongozi wastaafu Afrika

Picha
KONGAMANO la Kikanda la Viongozi Wastaaafu wa Afrika limeazimia mambo makuu matano ikiwamo la kuwataka viongozi walio madarakani kuimarisha mifumo yao ili kusaidia kulinda amani na kuzuia migogoro. Kongamano hilo lililoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, lilihudhuriwa  na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na washiriki wengine kutoka  taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa zinazojihusisha na masula ya usalama na kulinda amani.  Akisoma mazimio hayo jana jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa chuo cha Uongozi, Gerase Kamugisha, alitaja maazimio hayo kuwa ni kuimarisha taasisi za kanda na Umoja wa Afrika zenye jukumu la kujenga na kulinda amani. Alitaja aazimio lingine kuwa ni kuongeza uratibu, ushirikiano na mashauriano miongoni mwa taasisi za kitaifa, kikanda na bara zima zinazohusika na juhudi za kuzuia migogoro au kulinda amani ikiwamo kuimarisha mifumo ya ushirikiano baina ya Baraza la Amani...

Hizi ndio sababu za Dewji kupewa Simba

Picha
Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa Mwanasheria wake Evodius Mtawala, leo imeweka wazi sababu za mshindi wa zabuni ya kuwekeza kwenye klabu hiyo Mohamed Dewji, kupewa asilimia 49 ya hisa tofauti na 51 kama alivyotaka yeye. Mtawala ameyasema hayo ikiwa ni siku chache zimebaki kuelekea kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo Mei 20 ambapo wanachama wataamua iwapo wanapitisha katiba mpya yenye kuruhusu mfumo wa hisa au la. ''Kwanza wanachama wanatakiwa kufahamu kuwa tayari  Mohammed ‘Mo’ Dewji amekubali kununua asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba SC na sio 51 kama aliyoomba awali na hii ni kwasababu ya kanuni na maelekezo ya Serikali'', amesema. Mwanasheria huyo ambaye amewahi kuwa katibu wa Simba ameongeza kuwa wao kama klabu walikuwa tayari kuuza asilimia 50 mpaka 51 kwa bilioni 20 alizotoa Mo Dewji lakini baadae serikali iliagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja. Kwa upande wa wanachama, Mtawala amesema watamiliki hisa ndani ya kampuni ya 'Simba ...

"Hali ya Q Chief si Salama Anahitaji Msaada Mkubwa Sana"..Mke Afunguka

Picha
Mke wa msanii wa muziki wa bongo fleva Q Chief, anayejulikana kwa jina la Eliza, amesema kwamba mume wake anahitaji msaada zaidi, kwani hayuko sawa. Eliza ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, na kusema kwamba mume wake huyo ambaye kwa sasa wametangana, anaonekana hayuko sawa kwani amemfanyia vurugu na kumtolea maneno machafu, hivyo ni vyema iwapo atapatiwa msaada. “Katoka kunifanyia vurugu saa hivi, kanitukana sana, kuna makosa amefanya lakini siwezi kuongea, hata aibu kuongea, kuna vitu alikosea akaondoka mwenyewe, ameamua mwenyewe hakufukuzwa, sasa ndio maisha ambayo amepanga, kasema anaacha muziki amemrudia Mwenyezi Mungu ambapo ni suala jema, ila hayupo normal, anahitaji msaada”, amesema Eliza. Msanii huyo hivi karibuni ametangaza kuachana na muziki, huku akijilaumu kuwa amekosea sana familia yake na watoto wake na mke wake kumkimbia, hadi kufikia kutoa machozi mbele ya waandishi wa habari.

Mambo ambayo Lulu anaruhusiwa na asiyoruhusiwa kufanya akitumikia kifungo cha nje

Kwa mujibu wa kifungu na 3(2) (a) cha Sheria ya Huduma kwa Jamii ya mwaka 2002 kifungo cha nje ni utaratibu ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli/kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii. Utaratibu huu hutolewa kwa wafungwa ambao vifungo vyao havizidi miaka mitatu bila kujali wana faini au hawana. Masharti na utaratibu unaotumika kumpa mfungwa kifungo cha nje Baada ya Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu kupewa kifungo cha nje jana, watu wengi wamekuwa wakijiuliza imekuwaje akapewa kifungo hicho, lakini wapo pia waliokuwa wakijiuliza, baada ya kupewa kifungo cha nje, ni mambo gani mengi anaruhusiwa kufanya au harusiwi kufanya? Taarifa ya Magereza kuhusu sababu ya Mwigizaji Lulu kupewa kifungo cha nje Mfungwa anapopewa kifungo cha nje, hakuna masharti ya jumla yanayofanana kwa wafungwa wote kwamba watakapokuwa nje ya gereza watatakiwa kufanya hiki na hawatakiwa kufanya kile. Kifungu cha 4 cha Sheria za Huduma za Jamii kinaipa m...

Sethi avuliwa ukurugenzi wa IPTL akiwa mahabusu

Picha
Huku akikabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, Harbinder Sing Sethi ameondolewa katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL). Uamuzi wa kumuondoa Seth katika ukurugenzi umefikiwa na bodi ya wakurugenzi ambayo pia imemvua madaraka ya kuwa mwenyekiti mtendaji wa IPTL, baada ya kushindwa kushiriki na kuhudhuria mikutano ya bodi. Seth anadaiwa kushindwa kuhudhuria vikao vya bodi bila kuruhusiwa na wakurugenzi wenzake kwa miezi sita mfululizo tangu Juni 19, 2017 alipokamatwa na kushitakiwa. Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa IPTL, Ambroce Lugenge wakati akitoa muhtasari wa maazimio yao wakati wa mkutano mkuu wa tatu uliofanyika Aprili 10. Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili kampuni hiyo na uendeshaji wa mambo yanayohusu IPTL. Sethi anakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola22.198 milion...

Mzee Abdul Amwagia Sifa Tele Mama Diamond Platnumz

Picha
HAKUNA kitu kizuri duniani kama kujielewa kuwa umekosea na kurekebisha makosa. Pia katika maisha hakuna binadamu aliyekamilika pale linapokuja suala la kukosea. Inaeleweka kuwa, kwa muda mrefu wazazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mzee Abdul Jumaa ‘Baba Diamond’ na Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ walikuwa na tofauti za muda mrefu na hivi karibuni tofauti zao zinajionesha wazi kuisha licha ya kila mmoja kuwa katika uhusiano mwingine. DIAMOND NA MZEE ABDUL Mzee Abdul aliingia kwenye bifu zito na Diamond baada ya kumtuhumu kutomjali kwa sababu tu ana ugomvi na mama yake mzazi, (Bi Sandra) hali iliyosababisha staa huyo anayebamba na Ngoma ya African Beauty kumchunia kwa muda mrefu. Hayo yote yalijidhihirisha wazi pindi tu Diamond alipofanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza, Latiffah Nasibu ‘Tiffah’ aliyezaa na mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ siku aliyokuwa anamtoa nje kwa mara ya kwanza ...

Utata Kesi ya Ali Kiba ya Kutelekeza Mtoto

Picha
DAR ES SALAAM: Mambo ni moto! Baada ya hivi karibuni mzazi mwenzake na staa wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba ‘King Kiba’, Hadija Hassan kuuambia umma kwamba amemwaga ugali kwa kwenda mahakamani kudai malezi ya mtoto, utata mkubwa umeibuka katika kesi hiyo.  Kinachotatiza ni pale King Kiba naye alipoibuka ‘juzikati’ mbele ya ‘maiki’ ya redio maarufu jijini Dar na kumwaga mboga kuwa hajui chochote kuhusu kesi inayoelezwa na Hadija kwenye vyombo vya habari kuhusu yeye kumtelekeza mwanaye. “Yule mtoto kweli ni wa kwangu, ugomvi wetu unakuja pale familia yetu tunapotaka kumchukua na kukaa naye hata kwa siku chache hataki jambo ambalo linatupa wasiwasi kwa nini afanye hivyo na amekwenda mahakamani ili kuninyanyasa na familia yangu.  “Alikuwa hataki sisi tukae naye mpaka mtoto wakati fulani alikuwa anamtaja baba mwingine, kiukweli nilijisikia vibaya sana, nilitamani sana shauri lifike mahakamani ili ukweli ujulikane,” alisema ...

Rayvanny Ampigia Salute Ali Kiba, Amtaja Katika Wasanii Wanaofanya Vizuri

Picha
MSANII wa Bongo Fleva kutoka WCB Wasafi, Rayvanny bila kinyongo ameonyesha kupenda kazi anayoifanya Alikiba ambaye ni hasimu wa Diamond Platinumz kwa miaka mingi. Akifanya mahojiano na Global TV Online, rayvanny amewataja wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa nchini Tanzania hasa katika tasnia ya muziki ambapo mbali na Kiba alimtaja pia Diamond na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kwamba wanaipeperusha vyema bendera ya Tanzania Kimataifa.  VIDEO;

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo

Picha
Bonyeza links zifuatazo 20 Job Opportunities at Tanzania National Roads Agency (TANROADS) Njombe 5 Job Opportunities at The Ministry of Finance and Planning May 2018 Job Opportunity at NBC Bank Tanzania, Head of Credit Job Opportunity at Halotel Tanzania, Legal Advocate Job Opportunity at NBC Bank Tanzania, Operating Officer Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

Alikiba Apokea Tuzo ya Nyota wa Michezo.

Picha
Ikiwa ni siku tano zimepita tangu Alikiba aachie ngoma yake mpya ‘Mvumo wa Radi’ amepokea tuzo ya heshima ya Plaque inayoitwa Nyota wa Mchezo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM. Msanii huyo amepewa tuzo hiyo jana Jumatatu  kutokana na mchango wake kwenye muziki na jitihadi alizipiga kupeperusha bendera ya Tanzania na kuwa inspire wasanii wengine wachanga na kuendelea kuwepo mpaka leo kwenye muziki. Kiba amekuwa msanii wa tatu kupewa tuzo hiyo baada ya Vanessa Mdee aliyekabidhiwa mwezi January mwaka huu na Diamond aliyepewa mwezi wa tatu. Kwa sasa video ya ngoma yake mpya ya Mvumo wa Radi ina views milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Wema Augua Ghafla Mahakamani

Picha
JANA Mrembo Wema Sepetu ameshindwa kujitetea katika kesi yake ya kutumia dawa za kulevya baada ya kuugua ghafla akiwa mahakamani hapo. Wakili wa Serikali, Costanine Kalula alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo limeitishwa ili Wema na wenzake waanze kujitetea, lakini Wema anaumwa, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine. Baada ya kueleza hayo, Mama mzazi wa  Wema Sepetu, Miriam Sepetu aliieleza mahakama kuwa Wema alifika mahakamani hapo lakini wakati anasubiri  kuingia mahakamani alianza kuumwa ambapo alianza kutapika na hivyo kuondoka. Baada ya maelezo hayo , Hakimu, Thomas Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi May 29 na 30, 2018  washtakiwa watakapoanza kujitetea. Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia. Inadaiwa February 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na ms...

Mwandishi wa Habari asimulia alivyotekwa na wafanyakazi wa Ofisi ya RC Arusha

Picha
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha, limesema kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusiana na kuwepo kwa tukio la utekaji  wa mwandishi wa mitandao ya Kijamii, lililofanywa na watumishi wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha na kisha kushtakiwa kuwa alifumaniwa na mke wa mtu. Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema hayo ofisini kwake leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kuwepo kwa tukio hilo . Akisimulia tukio hilo Lucas Myovela, amesema  alipigiwa simu na Amina Msuya au Ravness anayefanya kazi ofisi RC Arusha upande wa kutunza kumbukumbu, akimuomba wakutane ili amuelezee tatizo kati yake na rafiki yake wa kiume aitwae Swalehe Mwindadi, ambae nae ni mtumishi ofisi ya mkuu wa mkoa, masijala ingawa kwa sasa anasaidia ofisi ya Itifaki. Anasema  Amina au Ravness, alimsimulia mkasa na kumwambia kuwa hawana maelewano na mwenzake hivyo anaomba suala hilo liandikwe kwenye vyombo vya habari kwa kuwa limeshafikishwa kwa Katibu tawala wa mk...

Jibu la Hamisa Mobetto kuhusu kufunga ndoa na Diamond

Picha
Mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu iwapo yupo tayari kufunga ndoa Diamond Platnumz mara baada ya muimbaji huyo kuweka wazi atafanya hivyo mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi wa Filamu ya Mama kutoka kwa Aunt Ezekiel, Hamisa alipoulizwa iwapo yupo tayari kuolewa na Diamond alijibu kwa sasa huwezi kuzungumzia hilo. “Siwezi kujibu hilo swali,” aliongea Hamisa kwa kifupi. Katika hatua nyingine Hamisa alidai kuwa yeye sio single mother kwani wazazi wenzie wanamsaidia katika malezi ya watoto. “You can’t call your self Single Mother kama unasaidiwa kulea mtoto na baba watoto wako, so facts is mababa watoto wangu wote wananisaidia kulea watoto vizuri, kwa hiyo siwezi nikasema single mother sababu nasaidiwa kulea watoto,” alisema Hamissa. Hamisa ni mama wa watoto wawili ambao wa kwanza alizaa na Majay na wapili alizaa na Diamod Platnumz.

Vodacom yatangaza faida ya shilingi 170 bilioni

Kuimarika kwa mapato ya kampuni ya Vodacom kumeiwezesha kupata ya faida ya Sh170.24 bilioni hivyo kuwa na uwezo wa kutoa gawiwo la Sh83.81 kwa kila mwanahisa. Faida hiyo imepatikana katika mwaka unaoishia Machi 31, 2018 huku maeneo matatu yakibainishwa kuchangia ufanisi huo. Mkurugenzi mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao amesema maeneo yaliyopata faida hiyo ni katika huduma ambako faida imeongezeka kwa asilimia 5.9 na kufika Sh966.3 bilioni wakati yale ya M-Pesa yakiimarika kwa asilimia 16.7 hadi Sh291.2 bilioni. Pia, mauzo ya data yakiongezeka kwa asilimia 34.7 na kufikisha Sh141.6 bilioni. “Mafanikio hayo yametokana na huduma bora tunazozitoa kwa wateja na kuimarika kwa matumizi ya data na mfumo unaoboreshwa kila siku wa fedha mtandaoni.” amesema Ferrao.

Kauli ya serikali kuhusu utaratibu utakaotumika kupima watu UKIMWI kwenye baa

Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema upimaji wa Kifua Kikuu (TB) na UKIMWI kwenye baa hautakuwa wa lazima. Waziri wa Afya ameyasema hayo baada ya kuzuka hofu miongoni mwa wananchi ambapo baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakipotosha kuwa, upaji huo utafanywa kwa lazima. Ameyasema hay wakati akizungumza katika maadhimisho wa miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), na kusema watatumia ushawishi kuhakikisha wananchi wanapimwa na kujua afya zao. “Tutatekeleza mpango wa kusogeza huduma za upimaji TB na ukimwi kwenye baa, ila hautakuwa wa lazima, tutachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo,” alisema. Alisema, wizara ipo katika mkakati wa kufanyia marekebisho ya Sheria ya UKIMWI kwa lengo la kuruhusu watu kujipima mwenyewe, kutoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kwenda kupima UKIMWI bila kupata ridhaa ya wazazi au walezi. “Haya ni maeneo ambayo kama tut...

Mchezaji Neymar Aweka Wazi 'Anacho-Miss' Barcelona

Picha
Nyota wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr amesema kama mtu akimuuliza anachokumbuka ndani ya Barcelona jibu ni wachezaji wenzake wa Lionel Messi na Luis Suarez ambao walitengeneza ushirikiano mkubwa. "Tulikuwa na urafiki mzuri sana kati yangu, Messi na Suarez kwahiyo kitu ambacho siwezi kusahahau ndani ya Barcelona ni kucheza na hao wachezaji wawili ambao daima tulifurahi na tulikuwa marafiki wakubwa," amesema. Neymar ameyasema hayo kwenye mahojiano na runinga moja ya Ufaransa alipokuwa akiongelea kupona kwake na kurejea rasmi kazini huku ligi ikiwa inaelekea ukingoni lakini yeye amesema yupo imara kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi. Neymar amekaa nje ya uwanja tangu mwezi Februari kutokana na kusumbuliwa na kifundo cha mguu wa kulia lakini sasa amepona baada ya kufanyiwa matibabu nyumbani kwao Brazil. Nyota huyo mwenye miaka 25 aliondoka Barcelona kwenye usajili wa majira ya kiangazi 2018 na kutua PSG kwa dau la rekodi ya dunia Euro 222 zaidi...

Pole Sana Aisee.... Aliyetaka Kumuhonga Zari Range Rova Apigwa Kibuti

Picha
Zari The Boss Lady amesema hamfahamu Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya aliyetangaza kumnunulia mrembo huyo gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017. Hapo jana Ringtone Apoko aliweka wazi kuwa amenunua gari hilo baada ya kusikia Zari atawasili nchini humo kwa ajili ya event yake, pia kipindi cha nyuma msanii huyo alipopata taarifa za Zari kuachana na Diamond alijitokeza na kueleza ana nia ya kumuoa.  Zari akiwa nchini Kenya amehojiwa na kituo cha Radio, Kiss FM na kueleza kuwa hamfahamu msanii huyo. “I don’t know ringtone and I have never met him. This is actually news to me. I have over 3.9 million followers on instagram and I wouldn’t know who follows me,” Zari  said. “Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi,” ...

Tuwapende Mama zetu na Wake zetu Wanapitia Magumu Sana Kipindi cha uja Uzito.

Picha
Nilikuwa nikisikia wanawake wakisema nimepata shida miez tisa kumbeba mwanangu tumboni nilikuwa sielewi vizuri taabu na shida hizo ni zipi mpk wajisifie kila dakika kila saa na kila siku. Sasa nahizi taabu na shida wanazozipata. Maana mke wangu ndo kwanza mja mzito miez tisa kasoro siku chache sasa naona shida na taabu anazopata. Kulala shida kusimama kwake shida kukaa shida hakuna jema hata moja. Akilala kila anavyojaribu mara aweke mgongo chini anateseka, alale kiupande upande shida mpk namhurumia. Najaribu kuwaza ndivyo nilivyomtesa mamayangu hivyo nikiwa Tumboni??? Kama ndivyo kweli mama anatakiwa aheshimiwa na kupongezwa kwa uvumilivu wanaopitia mpk kutuleta duniani. Lakini kinachonifanya niwaze zaid je baada ya kuzaliwa mimi mtoto wa kwanza kama nilimtesa mama hivi ikawaje akaniletea mdogo wangu, hakukumbuka shida na taabu nilizomletea?? Daaaaah wanawake mnastahili pongezi kubwa kwa ujasiri na uvumilivu mnaopitia kipindi cha ujauzito. Japo nasikia mkienda mbele zaid kutununua...

Zitto Kabwe Aivaa Serikali

Picha
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amesema kwamba haiingii akilini kwa serikali kuagiza malighafi za kujengea reli nchini, wakati tuna makaa ya mawe na chuma wilayani Ludewa, ambayo mpaka sasa hayajaanza kuchimbwa. Akizungumza Bungeni jana Zitto Kabwe alisema iwapo serikali ingechukua hatua katika kutengeneza kiwanda cha chuma kutokana na madini ya chuma yaliyopo Ludewa, serikali isingeingia gharama ya kuagiza malighafi za ujenzi wa reli nje, na pia ingeweza kupata kipato kwa kuuza kwa nchi jirani kama Kenya na Zambia, ambako nako kuna ujenzi wa reli unaendelea. “Niligusia ujenzi wa reli na jinsi ambayo tunaagiza malighafi za ujenzi kutoka nje, waziri anasema wameenda wamezindua kiwanda cha nondo sijui wapi na wapi, nondo zote hizi malighafi zake ni kutoka nje, na tuna chuma Mchuchuma na Liganga miaka yote hii.  "Kweli inaingia akilini tuna chuma na makaa ya mawe yamejaa pale Ludewa, tunampa mkandarasi kazi ya kujenga reli, vyuma vinatoka Uturuki, India, China kwel...

Maxence Melo: Utambulisho wa Majina Mitandaoni Utaua Habari za Kiuchunguzi

Picha
Wadau wa majukwaa ya habari za mitandaoni, nchini Tanzania wameitaka Serikali kutafakari juu ya kasoro zilizoko katika Kanuni za Maudhui ya kimtandao. Wakati wa mdahalo huo uliofanyika Jumamosi, Dar es Salaam, wadau hao walijadili mchango wa mitandao ya kijamii katika kuhamasisha utawala bora. Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo alisema kipengele kinachotaka utambulisho wa majina ya washiriki katika mitandao ya kijamii kinalenga kuuwa upatikanaji wa taarifa nyingi za kiuchunguzi. “Athari zake ni kwamba, utapata watu wachache watakaotoa taarifa za ufisadi ndani ya Serikali, hatuoni sababu za kutambua majina ya washiriki katika mitandao, itakuwa ni mwisho wa watu wengi kusema ukweli,” alisema Melo aliyesimulia harakati za kuanzisha jukwaa hilo takribani miaka 15 iliyopita. Washiriki wengine katika mdahalo huo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ni makundi ya vijana mbalimbali ya wafuasi wa vyama vya siasa, wanahabari na wa...

Profesa Mwandosya: "Hongera Sugu umehitimu chuo cha uanasiasa gerezani"

Picha
Waziri wa serikali ya awamu ya nne Prof. Mark Mwandosya ameingia katika Orodha  ya watu walioonesha furaha yao baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kuachiliwa jana  kutoka gerezani ambapo alihukumiwa kifungo cha miezi mitano. Prof. Mwandosya ameandika katika ukurasa wake wa twitter;  “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa, gereza la Ruanda, Mbeya. Kutofautiana vyama, itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui. Mungu Ibariki Tanzania.”

Zari , Mwanaume Haachwi , Ulicheza Faulo Kumwacha Diamond Kirahisi Rahisi

Picha
Tatizo wadada wa mjini mnapenda kuoelewa/ kudate mastaa Ila hamtaki kulipa gharama, ku date na staa sio mchezo, mamillion ya watu wanatamani kulala na mastaa, mastaa huwa wanasumbuliwa kila kukicha, ebu fikiria mtu kama Rihanna, unadhani hakuna mtu wa kumuoa? , tatizo watu wanajua ni stress kumdate rihanna , mtu kila siku anazunguka duniani kufanya shoo, unajua anakutana na watu wangapi? , Hana muda na mpenzi wala familia, uko tayar kuvumilia ku date mtu kama huyo , uko tayar ku cope? , mastaa hawana muda wa kutosha wa ku enjoy na familia zao. Sasa Dada yetu zari wakati unakutana na diamond ulimkuta akiwa staa tayar , alikua na msululu kibao wa wanawake aliodate nao au kulala nao , ulijua fika kuwa mtu wako anawindwa na wadada wa mujini, Ila wewe ukabahatika, na mkazaa , tena mtoto wa watu alikua anakuheshimu na kukupost instagram juu, Diamond ni malaya hilo liko Wazi, Ila kwa kuwa iliamua kumzalia tena watoto wawili, we ni bora tu ungemvumilia upuuzi wake mkalea watoto vizuri , maan...

Warembo Wazichapa Kavu Kavu Kumgombea Baba Diamond...

Picha
DARESSAL AA M: Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma. Tukio hilo lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja maarufu kwa jina la Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar ambayo baba wa msanii huyo anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata ‘kinywaji’.  Mtoa ubuyu wetu aliyelipigia simu Amani alisema kuwa, warembo hao walitangulia kufika katika baa hiyo na kupiga stori pamoja huku wakipata kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika nao, kila mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake. “Yani walianza kubishana. Ghafla wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua. Baba Diamond kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo chetu.  Baada ya kuunasa ubuyu huo, Amani lilimvutia waya baba Diamond ambaye alishtuka kusikia hab...

Tupo Tayari Kwa Fainali Za AFCON 2019

Picha
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo tayari kwa maandaalizi  ya fainali za michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019. Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Tanzania. Ameyasema hayo jana (Alhamisi, Mei  10, 2018) wakati akijibu swali la Mbungewa Sumve Bw. Richard Ndassa katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni Jijini Dodoma. Katika swali lake Bw. Ndassa alitaka kujua Serikali imejipangaje kufanikisha mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuipa Tanzania uenyeji wa fainali hizo. “Maandalizi ya fainali hizo yanaendelea vizuri, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuziunga mkono timu zote zinazofikia mashindano ya kimataifa ili ziweze kufanya vizuri”. Waziri Mkuu alisisitiza kwamba “ni jukumu letu kuziandaa timu zote ambazo zinashirik...

Rais Magufuli: Kuteuliwa sio tatizo, ukishindwa tunakurudisha

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amesikitishwa na vitendo vya Mabalozi kushindwa kutekeleza maagizo yake aliyowapa ya kumpa taarifa juu ya utendaji kazi wao na manufaa ambayo Tanzania imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi aliyopangiwa kila robo mwaka. Ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza kumuapisha, Alphayo Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa T abora. Amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa manufaa ya Taifa na sio kufanya mambo ndivyo sivyo. “Balozi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi fulani, nchi imenufaikaje na uwepo wake kwenye nchi ile?. Kuteuliwa sawa lakini sio lazima ukae katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa, ukishindwa kuleta manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atakayeleta manufaa kwa nchi,”amesema Rais Dkt. Magufuli Hata hivyo,Rais Dkt. Magufuli ...

Spika ataka Mawaziri wasafiri, awapa kazi wabunge

Picha
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuna haja ya wabunge kuwaombea mawaziri kwenye mamlaka husika ili wapate fursa kusafiri nje ya nchi. KauIi hiyo ya Spika imekuja kufuatia hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo alisema ni muhimu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage asafiri nje ya nchi, ili kujenga uhusiano ya kidiplomasia na kutafuta masoko ya bidhaa za mbaazi, choroko na giligilani. Spika Ndugai ambaye alikiri kukubaliana na mchango wa Zitto Kabwe amesema ni kweli mawaziri inabidi wasafiri na wabunge wanapaswa kuwaombea kutoka kwenye mamlaka. “Waziri wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazima aende, tumuombee popote pale kwenye mamlaka lazima asafiri, maana bidhaa zetu tutauza Kongwa, kuna soko huko? “Waziri wa utalii lazima asafiri ‘apige mawingu’ huko na wengine huko, ndiyo ukweli jamani, sisi wabunge lazima tuwasemee,” amesisitiza...

Rais Magufuli: Kuteuliwa sio tatizo, ukishindwa tunakurudisha

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amesikitishwa na vitendo vya Mabalozi kushindwa kutekeleza maagizo yake aliyowapa ya kumpa taarifa juu ya utendaji kazi wao na manufaa ambayo Tanzania imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi aliyopangiwa kila robo mwaka. Ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza kumuapisha, Alphayo Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa T abora. Amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa manufaa ya Taifa na sio kufanya mambo ndivyo sivyo. “Balozi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi fulani, nchi imenufaikaje na uwepo wake kwenye nchi ile?. Kuteuliwa sawa lakini sio lazima ukae katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa, ukishindwa kuleta manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atakayeleta manufaa kwa nchi,”amesema Rais Dkt. Magufuli Hata hivyo,Rais Dkt. Magufuli ...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 11

Picha
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 11