SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 11 Agosti 2018

T media news

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI AFRIKA(OATUU) LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA VITA DHIDI YA UFISADI NCHINI


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika**(OATUU**) lililokutana mjini Dar es Salaam,Tanzania kwa mkutano wa siku limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa mapambano ya dhati juu ya vitendo vya Rushwa na Ufisadi.

Akisoma maazimio ya kikao hicho Katibu Mkuu wa *OATUU* *Cde Arzeki Mezhoud* amesema kwamba Tanzania ni kati ya nchi chache za mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya Rushwa Afrika na Rais Magufuli ni kielelezo wa Kiongozi anayechukia Rushwa kwa Vitendo na kwamba *OAATU* inamuunga mkono katika jitihada hizi na asijione yupo peke yake katika vita hii kubwa.

Akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) *Mh Anthony Mavunde* kupokea maazimio hayo ya *OATUU* kwa niaba ya Serikali,Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania *(TUCTA)* Cde Tumaini Nyamuhokya amesema TUCTA inaunga mkono jitihada za serikali kupambana na Rushwa na muda wote itashirikiana na serikali katika mapambano hayo.

Aidha Naibu Waziri Mavunde amewashukuru *OATUU* kwa kutambua jitihada za Rais Magufuli na serikali yake ya awamu na kuwataka wananchi wote kuunga mkono hatua zinazochukuliwa ma serikali kupambana na Rushwa.