Punguza Uzito Bila Gharama Kubwa: Jinsi ya Kutengeneza Juice ya Ukwaju Nyumbani | T MEDIA NEWS
Kupunguza uzito si lazima kutumia pesa nyingi au dawa ghali. Kwa kutumia vyakula vya asili vinavyopatikana kirahisi, unaweza kusaidia mwili wako kujisafisha na kupunguza uzito kwa njia salama. Moja ya njia rahisi ni kutumia juice ya ukwaju , ambayo inajulikana kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kuondoa uchafu mwilini. Faida za Juice ya Ukwaju Husaidia kusafisha tumbo Huboresha mmeng’enyo wa chakula Huchangia kupunguza uzito Husaidia kuondoa sumu mwilini Mahitaji Ukwaju robo kilo (uliomenywa) Limao 1 la wastani Maji lita 1 Asali vijiko 3 au rojo ya tende nusu kikombe Jinsi ya Kuandaa Weka ukwaju kwenye sufuria kisha ongeza maji lita 1. Chemsha kwa dakika 15–20 ili ulainike vizuri. Koroga mara kwa mara wakati una chemka ili uchanganyike vizuri. Baada ya hapo, ipua na uache ipoe. Ondoa mbegu za ukwaju kisha chuja maji yake. Kamulia limao ndani ya mchanganyiko. Ongeza asali au rojo ya tende kulingana na chaguo lako. Koroga vizuri – juice yako itakuwa tayari kwa ...