Machapisho

IJUE HISTORIA YA KABILA LA WAKURYA

Picha
Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya. Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria. Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji. Kilimo cha asili walikuwa wanalima ulezi mtama na viazi tu kwa ajili ya kutengeneza Togwa (obosara) na Pombe. Mazao mengine yalianza kulimwa miaka ya 1900  baada ya wajerumani kuhimiza kilimo. Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana. Ila kwa kupenda kwao vita walijiunga sana na jeshi K.A.R (King African Rifle) kupigana vita ya kwanza na ya pili n...

Rais Magufuli Abaini Tatizo Kubwa Wizara ya Maji na Wizara ya Ardhi.....Atoa Maagizo Mazito

Picha
Rais Dkt. John Magufuli ameagiza wataalamu wote wa idara za maji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hiyo na kuwawajibisha wahusika pale miradi isipotekelezwa. Rais Magufuli pia amewataka wataalamu wa ardhi na mipango miji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hiyo na kuwawajibisha wahusika pale mradi unapotekelezwa visivyo. Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo Mei 10, 2018 wakati alipokuwa anazungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kumuapisha Mhe. Alphayo Japani Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Bw. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora na kusema hajaridhishwa na utendaji katika sekta maji na ardhi kutokana na usimamizi mbaya wa miradi mingi ya maji na usimamizi mbaya wa masuala ya ardhi na mipango mi...

Rais Magufuli: Sasa hivi kila mahali watu wanalalamikia maji

Picha
Rais Dkt. John Magufuli ameagiza wataalamu wote wa idara za maji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hiyo na kuwawajibisha wahusika pale miradi isipotekelezwa. Rais Magufuli pia amewataka wataalamu wa ardhi na mipango miji katika halmashauri zote nchini kusimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hiyo na kuwawajibisha wahusika pale mradi unapotekelezwa visivyo. Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo Mei 10, 2018 wakati alipokuwa anazungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kumuapisha Mhe. Alphayo Japani Kidata kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada na Bw. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora na kusema hajaridhishwa na utendaji katika sekta maji na ardhi kutokana na usimamizi mbaya wa miradi mingi ya maji na usimamizi mbaya wa masuala ya ardhi na mipango mi...

Wadau wampongeza Spika Ndugai

Picha
Wadau wamempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kwa kuonesha nguvu ya Bunge katika kusimamia maslahi ya Taifa, nakubainisha hatua hiyo itaweza kujenga imani kwa wananchi juu ya Bunge lao. Akizungumza kwenye kipindi cha Easta afrika BreakFast kinachorushwa na East Afrika Radio, mtaalamu wa siasa za kikanda, Amini Mgeni amesema Spika wa bunge la Tanzania amesimamia haki na kuonesha wajibu wa wabunge katika kusimamia maslahi ya wananchi, jambo ambalo linapaswa kuigwa na wabunge wote. "Hivi ndivyo bunge linavyopaswa kuwa ni mhimili unaojitegemea na unapaswa kuikosoa serikali nakutetea wananchi maana wao ni wakilishi wa watanzania wengi waliowapa dhamana, Spika Ndugai ataheshimika daima kama ataendelea na msimamo wake huu bila kuangalia chama", amesema Amini. Mei 8, 2018 Spika Ndugai aliyakataa maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage nakumtaka atoe majibu yakueleweka kuhusu uhaba wa mafuta nchini, jambo ambalo Waziri M...

Mhandisi aliyetajwa na Rais Magufuli Chuo cha Mkwawa asomewa mashtaka na kunyimwa dhamana

Picha
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa, imemnyima dhamana Mkurugenzi wa Kampuni ya MNM, Engineering Service Ltd, Mhandisi Godwin Mshana, kwa tuhuma za kujenga ukumbi wa Chuo Kikuu Mkwawa, (MUCE) chini ya kiwango. Mshana alifikishwa leo Mei 10, Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, Iringa, David Ngunyale. Wakili wa Serikali, Blandina Mnyamba amemsomea mashtaka Mshana na kusema kuwa alitenda makosa hayo kati ya 2010 na 2012.  Amesomewa mashtaka ya kughushi nyaraka za serikali, kujipatia fedha Sh 3 bilioni kinyume na utaratibu na shtaka la tatu ni kuhujumu uchumi katika matumizi ya Sh 2bilioni. Dhamana ya Mshana imezuiwa na kesi hiyo itasikilizwa tena Mei 22 mwaka huu.  Mei 2 mwaka huu, akiwa katika ziara Chuo Kikuu cha Muce, Iringa, Rais Magufuli aliagiza uchunguzi ufanyike katika ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa chuo hicho, uliogharimu Sh 8 bilioni. Pia, Rais Magufuli  aliagiza, aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Philemon Mushi naye ...

Kauli ya kwanza ya Sugu baada ya kutoka gerezani leo

Saa chache baada ya kutoka jela, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema ni mfungwa wa kisiasa, “nilifungwa kiholela na nimetoka kiholela.” Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe leo Mei 10, 2018 walifika katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga lakini walipigwa chenga ya mwili baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka, hivyo kulazimika kuwafuata nyumbani. “Sikutaka kuhoji sababu za kutolewa, jana niliambiwa jiandae kesho (leo) tutatoka, basi nasi tukasema haina shida kwa sababu sikuwa na sababu ya kuwa ndani. Naamini sikutakiwa kuwa gerezani.” Sugu akiwa na Masonga alifika nyumbani kwake na kumkuta mlinzi pekee kutokana na mkewe Happiness Msonge kwenda Gereza la Ruanda kuwapokea. Dakika chache baadaye Happiness na mke wa Masonga, Grace Malya walifika nyumbani hapo na kuwalaki kwa furaha huku wakikumbatiana na ...

Maneno ya Nape baada ya Sugu kutoka gerezani

Picha
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemkaribisha uraini Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa akitumikia kifungo chake . Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa. “Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter. Sugu na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya