IJUE HISTORIA YA KABILA LA WAKURYA
Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya. Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria. Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji. Kilimo cha asili walikuwa wanalima ulezi mtama na viazi tu kwa ajili ya kutengeneza Togwa (obosara) na Pombe. Mazao mengine yalianza kulimwa miaka ya 1900 baada ya wajerumani kuhimiza kilimo. Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana. Ila kwa kupenda kwao vita walijiunga sana na jeshi K.A.R (King African Rifle) kupigana vita ya kwanza na ya pili n...