Wakimbiaji wa Kike Wenye Homoni za Kiume Kama Caster Semenya Wabanwa na Kanuni Mpya za Riadha Duniani
Baadhi ya wakimbiaji wa kike wenye homoni nyingi za kiume watatakiwa kukimbia dhidi ya wanaume au kubadili mashindano mpaka pale watakapopata matibabu, hizi ni sheria mpya zilizotolewa na chombo cha riadha duniani. Sheria, ambazo zitaanza kutumika tarehe 1 mwezi Novemba,zitawahusu wanawake wanaokimbia kuanzia mita 400 mpaka maili moja Mshindi wa mbiao za mita 800 kwenye michuano ya Olimpiki, Caster Semenya ni miongoni mwa watakaoathirika Mkimbiaji wa Afrika Kusini awali alitakiwa kufanyiwa kipimo cha kubaini jinsia na wakuu wa shirika hilo laini majibu hayakuwekwa hadharani. ''Sheria hizo si kuhusu udanganyifu, ni kuhakikisha kunakuwa na michuano ynayofanyika kwa haki na umaana''Rais wa IAAF Lord Coe alieleza akizungumza baada ya kushinda mbio za mita 800 na mita 1500 kwenye michuano ya jumuia ya madola mwezi Aprili,Semenya alisema atakimbia umbali mrefu zaidi Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya ku...