Machapisho

Bunge kuanza Vikao Leo, laweka wazi ratiba zake

Picha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma leo (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbara kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 yakiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu zitawasilisha taarifa zake Bungeni hapo.

TLP yaivaa UKAWA uchaguzi wa marudio Kinondoni

Picha
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimevishukia vyama vinavyounda Ukawa kufuatia uamuzi wake wa kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha, baada ya kuususia uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi hautokuwa wa haki. Akizungumza na wanahabari jana  Januari 29, 2018 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lymo amedai kuwa, uamuzi huo wa UKAWA ambao umemsimamisha mgombea wa Chadema, Salum Mwalim kugombea jimbo la Kinondoni umewadanganya wananchi. “Uamuzi huo umeonyesha kwamba Chadema haiheshimu wananchi, umedanganya wananchi na umeathiri upinzani. Walitangaza kujitoa halafu wamebadili gia angani kitendo hiki hakikubaliki,” alisema. Lymo amedai kuwa, Chadema imesimamisha mgombea pasipo kufuata taratibu kutokana kwamba hakuna kikao kilichokaliwa wala maamuzi yaliyotolewa na vyama vinavyounda UKAWA katika kupendekeza mgombea wake. “Katika uchaguzi huu hakuna UKAWA sababu iko vipande vipande, hakuna kikao au maamuzi ya UK...

Serikali Yauza Meno Ya Viboko Kwa Sh.30,900,000/= Katika Mnada Wa Hadhara Jijini Dar Es Salaam

Picha
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa  Wanyamapori Tanzania (TAWA)  imefanya mnada wa hadhara wa kuuza meno ya viboko vipande  12,467 yenye uzito wa kilo 3,580.29   katika   ofisi  zake ndogo katika  Jengo la Mpingo,  jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya makampuni  19 yenye leseni daraja la kwanza yameshiriki  katika mnada huo. Mnada huo umefanyika  chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambapo  kampuni ya  On Tours Tanzania Limited  imeibuka mshindi kwa kwa kununua meno hayo kwa jumla ya shilingi  30,900,000/= Awali akizungumza katika mnada huo, Mwenyekiti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Karerema Kwaleh aliwataka wafanyabiashara kuzingatia masharti mnada huo. Ambapo Karerema alimtaka mfanyabiashara yeyote  atakeibuka mshindi  kulipia asilimia ishirini na tano (25%) ya bei papo hapo na asilimia sabini na tano (75%) italipwa yote katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya...

Mawaziri Wa Fedha Na Mipango Wa Tanzania Na Rwanda Wakutana Kujadili Mradi Wa Ujenzi Wa Reli Ya Isaka- Kigali

Picha
Benny Mwaipaja, WFM Mawaziri wa Fedha na Mipango wa  Tanzania na Rwanda wamekutana  Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018. Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili  na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha. Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balo...

Yasome hapa magazeti ya leo Jumanne Januari 30, 2018

Picha

Mmh! Zari Kiboko Ampa Ujumbe Huu Mama Diamond “Fanya Tuhame Guest House Tumuachie Mwanao”

Picha
Bado inaonekana ishu ya Diamond Platnumz kudaiwa kulala na wasichana wengine nyumbani kwake Madale, mama watoto wake Zari The Boss Lady hajaichukulia poa na inadaiwa kuwa amekasirishwa na tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii. Diamond siku kadhaa zilizopita alidaiwa kupeleka msichana mwingine na kulala nae nyumbani kwake Madale, ila baada ya kuenea kwa video clip ikimuonesha msichana huyo akiwa Madale, Zari alionesha kukasirishwa na kuandika snapchat “Ati Madale State lodge au Madale Guest house?” Baada ya siku kadhaa kupita baadhi ya mashabiki waliamini inawezekana ishu hiyo imepita ila comment ya Zari katika post ya instagram ya mama Diamond inaonesha amekasirika bado, hiyo ni baada ya ku-coment katika picha ya Mama Diamond aliyopost na kuandika “Kubwa la maadui” ikimuonesha Mama Diamond akiwa Madale lakini Zari akacomment “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”

Walichozungumza Rais Dkt Magufuli na Balozi Dkt Slaa Ikulu leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya Mazungumzo hayo Balozi Mteule Mhe. Dkt. Slaa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Balozi na ameahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Mhe. Dkt. Slaa amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora wenye maono na uthubutu wa kutekeleza mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa ( Standard Gauge ), ujenzi wa daraja la juu ( Flyover ) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela ( Tazara ), mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ( Stieglers’ Gorge ) na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. “Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekelez...