Machapisho

PolePole: Hakuna Kiongozi wa Dini ametishwa kwa kusema ukweli Tanzania

Picha
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amewazungumzia Askofu Zakaria Kakobe pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa dini na kusema kuwa hakuna mtu ambaye amezuiliwa kuongea Tanzania na kuwa wapo huru kutoa maoni yao. Polepole alisema hayo juzi wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Television na kusema hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania. "Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli ndani ya nchi ya Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anayesema mtu Tanzania kuna mtu kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani atakuwa na matatizo ila nachofahamu kwamba mtu kuzungumza lugha ya matusi kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zetu ni makosa" alisema Polepole Polepole aliendelea kusisitiza kuwa viongozi hao wa dini wapo wazi na huru kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya M...

USIA KWA WANANGU

Picha
‘Ewe wanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Allaah Atakileta. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye khabari za yote’.   ‘Ewe mwanangu! Shika Swalah, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa’ ‘Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Allaah Hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha ‘ [Luqmaan:16-18]

Lissu aunguruma kuhusu ukiukwaji wa Haki za Binadamu

Picha
Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kuuaga mwaka 2017, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoa waraka akilaani ukiukwaji wa haki za binadamu na kuminywa kwa uhuru wa kutoa mawazo. Waraka huo alioutoa jana Alhamisi Desemba 28,2017 akiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu tangu Septemba 7,2017 aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwenye makazi yake Area D mjini Dodoma. Lissu pia amezungumzia tukio la kutoweka mwandishi wa habari wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Azory Gwanda ambaye leo ni siku ya 39 tangu alipotoweka akiwa wilayani Kibiti mkoani Pwani anakofanyia kazi zake. “Watanzania ambao wamekuwa wakitumia uhuru wao wa maoni kutoa mawazo wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa mahakamani... mwanachama wa Chadema, Ben Saanane na mwandishi wa Mwananchi (Azory Gwanda) wametoweka na hawajulikani walipo. Hakuna uchunguzi au taarifa za kutoweka kwao,” amesema. Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chade...

Waziri Mkuu Awasilisha Tamko La Maadili Ya Viongozi Wa Umma

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekwishawasilisha tamko la maadili ya viongozi wa umma kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tangu  Alhamisi Desemba 28, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Namahema ‘A’ wilayani Ruangwa mkoani Lindi jana jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2017), Waziri Mkuu alisema fomu hizo zilipokelewa  na amekwishapatiwa barua ya kupokea tamko hilo. “Nimewaita hapa ili kuthibitisha kuwa nimetekeleza takwa hilo la kisheria na tayari Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi ya Umma imekiri kupokea tamko langu kwa barua hii hapa,”  alisema Waziri Mkuu huku akionyesha barua hiyo ambayo ilisainiwa na Jaji Harold Nsekela, Desemba 28, 2017. “Kwa kuzingatia mfano ulioonyesha na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ninawaagiza viongozi wote wanaotakiwa kujaza fomu hizo kwa mujibu wa sheria wafanye hivyo na kuziwasilisha ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017 saa 10 jioni...

Waziri Mkuu apokea wanachama 60 wa CUF

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 60 kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM). Wanachama hao wamepokelewa jana mchana (Ijumaa, Desemba 29, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nkowe kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Kabla ya kuwakabidhi kadi za CCM, Waziri Mkuu alipokea kadi za CUF kutoka kwa vijana saba kwa niaba ya wenzao 60. Vijana hao ni Hamisi Juma, Fatuma Abdallah, Mwajuma Mohammed, Thomas Moto, Zainab Nachiluku, Samia Said na Juma Said. Vijana hao saba waliokabidhiwa kadi mpya za CCM pamoja na wenzao 53, walikula kiapo cha uaminifu. Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama wote ni vijana ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali na wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano. Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka vijiji vya Kipindimbi, Nkowe na Mpumbe. Novemba 5, mwaka huu, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vy...

Serikali yawatoa hofu wananchi kuhusu deni la Taifa

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwamba deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa  hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti  ya Serikali kwa mwaka 2017/2018. Dkt. Mpango alisema kuwa katika tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56. “Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonesha kuwa deni hili ni himilivu  katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu,” alisema Dkt. Mpango. Akieleza takwimu hizo, Waziri Mpango amesema kuwa mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, deni la Taifa lilifikia shilingi bilioni 47,823.1 ikilinganishwa na bilioni 42,552.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2016 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi bil...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 30

Picha