Machapisho

TAWFIQ MONEY SERVICI

Picha

Wanaume Tuache Ubahili Tuwatunze Wapenzi Wetu

Picha
Kwanza nianze kwa kukili kua maisha ni magumu sana nadhani kila mtu anajua. Na katika mahusiano ya mapenzi kati ya me na ke lazima kunakua na tofauti ya kipato, yaani Mara nyingi wanaume wanakua na hali mzur kimapato kuliko mwanamke. Nieleweke vizur kua si maanishi kua wanawake wote wanakipato duni LA hasha. Ningependa kuwashauri wale wenye wapenzi WA kike mambo haya yafuatayo:- 1.  Ujue tofauti ya kuchunwa na kuhudumia unapokua na mpenzi ujue ni jukumu lako kumpendezesha anapopendeza watu watajua we ndio kidume uliemwezesha. 2  .Sio mpaka akuombe ndio umpe. jaribu kumfaam hali ya maisha na kipato chake ujue kukisia cha kumpa kwa matumizi yake. 3 .Usiulize ya nini,ikitokea mpz amekuomba HELA usiulize ya nn ye ni MTU mzima awezi kukuomba HELA akaenda kuchambia. 4 . Kutumia pesa nyingi sehemu ya starehe. Kuna watu wanaenda mpaka hotel ya nyota 5 kustarehe akitumia zaidi ya laki tano.cha ajabu baada ya kutoka hotel anamwacha mpz wake 10000 ya nauli. Huu ni ujinga bora u...

Bunge laeleza kiundani taarifa ya Freeman Mbowe kunyang’anywa gari

Picha

MUSOMA: Aliyoyabaini Naibu Waziri wa Afya baada ya kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini

Picha
Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji vya hospitali ya rufaa ya Musoma na  ya Murangi na vyumba hivyo kubadilishwa stoo na eneo la taka. Naibu Waziri ambaye yuko Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne alifanya ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini uchafu uliopo katika chumba cha upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa mashuka na mipira yake kuwekwa chini na huku kukiwa na vifaa vya kuwekea mashuka hayo. ‘’Hivi ndivyo mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani ya nyie kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu jamani, sisi sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa Mkoa au mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo hopspitali ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa? Alihoji Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa. Aidha aliagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda...

Mchungaji Msigwa afikishwa mahakamani kwa Matusi na Kutishia Kuua

Picha
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amepandishwa kizimbani leo Alhamisi katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata. Mbali na Msigwa pia Diwani wa Viti Maalum, Selestina Johanes na dereva wa mbunge huyo, Godi Mwaluka wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo. Akisoma shtaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Rehema Mayagilo amesema kuwa mbunge huyo na washtakiwa hao wawili wanashtakiwa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua diwani huyo. Hakimu Mayagilo amesema kuwa Msigwa na wenzake walitenda kosa hilo jana saa nane mchana katika viunga vya Ofisi za Halimashauri ya Manispaa ya Iringa. Baada ya kusomewa shtaka hilo Msigwa na wenzake wamepata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka huu itakapotajwa tena.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

Picha
Job Opportunity at Mobisol, Head of Human Resources Job at Shinyanga Urban Water Supply and Sanitation Authority (SHUWASA) Job Opportunity at Save The Children Tanzania Job Opportunity at VSO, Programme Manager Youth Job Opportunity at KP Recruiters, Sales Coordinator Job Opportunity at KP Recruiters, Sales Manager Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

Hatimaye Mchezaji Hasheem Thabit Apata Timu ya Kuchezea Kikapu nje ya Marekani

Picha
Mtanzania Hasheem Thabeet ambaye alikuwa anacheza mchezo wa mpira wa kikapu katika Ligi Kuu ya kikapu ya Marekani NBA, leo September 27 2017 ameripotiwa kujiunga na timu ya kikapu ya Yokohama B-Corsairs inayoshiriki Ligi Kuu ya kikapu nchini Japan. Hasheem Thabeet ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wa mpira wa kikakupu waliyofanikiwa Tanzania, amewahi kucheza vilabu kadhaa vya kikakupi nchini Marekani amapo ndio nchi inayofanya vizuri kwa upande wa Basketball duniani, Hasheem amepewa jezi namba 34. Ligi Kuu ya kikapu nchini Japan inatarajiwa kuanza Ijuma hii ya September 29 2017, kama utakuwa unakumbuka vizuri Hasheem Thabeet amewahi kuzichezea timu za Memphis Grizzlies, Portland Trail Blazers na Oklahoma City Thunder, Ligi Kuu ya kikapu ya Japan itaanza Ijumaa ya September 29