Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji vya hospitali ya rufaa ya Musoma na ya Murangi na vyumba hivyo kubadilishwa stoo na eneo la taka. Naibu Waziri ambaye yuko Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne alifanya ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini uchafu uliopo katika chumba cha upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa mashuka na mipira yake kuwekwa chini na huku kukiwa na vifaa vya kuwekea mashuka hayo. ‘’Hivi ndivyo mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani ya nyie kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu jamani, sisi sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa Mkoa au mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo hopspitali ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa? Alihoji Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa. Aidha aliagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda...