Machapisho

Mapya Yaibuka Sakata la Kusajiliwa kwa Buswita

Picha
Sakata la kiungo wa Yanga SC aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbao FC Pius Buswita kufungiwa mwaka mmoja kucheza mpira lapata sura mpya baada ya katibu mkuu wa Yanga ndugu Charles Boniface Mkwasa kulitolea ufafanuzi. Buswita amekumbana na rungu la TFF la kutojihusisha na soka kwa mwaka mmoja baada ya kile kinachodaiwa kusajili vilabu viwili kwa wakati mmoja yaani Yanga SC na Simba SC . Simba ndio waliomwekea pingamizi TFF ikidaiwa kawatapeli hivyo kufungiwa mwaka mmoja. Mkwasa asubuhi ya leo akiongea na kituo cha redio ya EFM amekiri kupokea barua ya hukumu hiyo ikiwaeleza hawataweza kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja kama adhabu yake . Mkwasa amesema kama klabu pia wameiandikia TFF barua kupinga uamuzi huo na kulieleza jambo hilo kwa kina sambamba na maelezo ya mchezaji husika . ” Simba SC wanasema Pius wamemsajili tarehe 2 juni 2017 ilihali kipindi hicho alikuwa ndani ya mkataba na Mbao FC kitu ambacho ni makosa kwa sababu hawakuwafuata Mbao . Sisi tumewafuata Mbao na mche...

Magazeti ya Mwananchi na Nipashe yageuzwa mfano wa kuonya mengine

Picha

Majambazi Yateka Basi na Kupora Abiria

Picha
Majambazi  sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana. Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana. Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge. Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo. Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwac...

Inasikitisha.. Muuguzi Awaua Wagonjwa 90 Ili Awafufue Tena

Picha
Muuguzi nchini Ujerumani anayetumikia kifungo cha maisha kwa kuwaua wagonjwa sita, imebainika aliwaua wengine 84. Idadi ya watu aliowaua imemwingiza katika rekodi ya mwanamke aliyefanya mauaji mengi kuliko wote nchini humo. Mwanamke huyo, Niels Hoegel (40), alifungwa mwaka 2015 baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wagonjwa sita kwa kuwachoma sindano inayosababisha moyo kusimama ghafla. Mamlaka za nchi hiyo zimekuwa zikifanya uchunguzi wa maelfu ya vifo, ikiwamo kufukua maiti za wagonjwa waliokufa chini ya uangalizi wake katika hospitali binafsi za Delmenhorst na Oldenburg ambazo amewahi kufanya kazi. Polisi nchini humo wameliambia Shirika la CNN kuwa, wanaamini Hoegel aliua wagonjwa 36 katika Hospitali ya Oldenburg kati ya mwaka 1999 na 2001, na wengine 48 katika Hospitali ya  Delmenhorst. Pia, wanasema idadi ya watu aliowaua inaweza kuwa kubwa zaidi lakini ushahidi hautapatikana kwa kuwa miili mingi ilichomwa moto, hivyo si rahisi kugundua sababu ya kifo kwa kupima majivu....

Ajari Yaua Sita na Kujeruhi 42 Mkoani Singida

Picha
Watu sita wamefariki dunia na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa mfanyabiashara wa Mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Mkoani Singida. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba, amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27  katika kijiji cha Kijota wakati lori hilo likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini ambapo amebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva. Kamanda Magiligimba amesema dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka hakuwa makini na barabara wakati anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi. Aidha waliofariki wametajwa katika ajali hiyo ni pamoja na Haji Jumanne, Mikidadi Mohammed wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama, Musa Salimu mkazi wa kijiji cha Mwakiti, wengine ni Allen Mwangu mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari mkaz...

Wabunge Wakerwa na Uwanja wa Ndege Dar Wasema Unatia Aibu

Picha
Hali ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam imewaibua baadhi ya wabunge ambao wamesema ni mbaya, jambo linalotia aibu. Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), Ali Salim Khamis amesema katika jengo la abiria paa linavuja na kuna joto kali. “Naweza nikapata shaka iwapo Terminal III nayo kwa miaka saba inaweza ikaanza kuvuja, Uwanja wa Julius Nyerere kwa kweli unatuaibisha,” amesema. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana Agosti 29, wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Pac) ilipokutana na Mamlaka vya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa). Amesema Taa ina viwanja vingi vya ndege lakini vinavyochangia mapato ni vichache, huku vingine vikiwa havifanyi kazi. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe amewataka wabunge waisaidie mamlaka hiyo ipate fedha za kutosha ili kuboresha viwanja vya ndege nchini. “Kwa kweli ni aibu uwanja wa ndege Dar es Salaam. Tuwasaidie ili waweze kuongezewa fedha,” amesema. Katika hatua nyingine, Mwenyekit...

Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya mikopo sasa ni Septemba 11 badala ya Septemba 4

Picha
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. "Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo," amesema. Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.