Mapya Yaibuka Sakata la Kusajiliwa kwa Buswita
Sakata la kiungo wa Yanga SC aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbao FC Pius Buswita kufungiwa mwaka mmoja kucheza mpira lapata sura mpya baada ya katibu mkuu wa Yanga ndugu Charles Boniface Mkwasa kulitolea ufafanuzi. Buswita amekumbana na rungu la TFF la kutojihusisha na soka kwa mwaka mmoja baada ya kile kinachodaiwa kusajili vilabu viwili kwa wakati mmoja yaani Yanga SC na Simba SC . Simba ndio waliomwekea pingamizi TFF ikidaiwa kawatapeli hivyo kufungiwa mwaka mmoja. Mkwasa asubuhi ya leo akiongea na kituo cha redio ya EFM amekiri kupokea barua ya hukumu hiyo ikiwaeleza hawataweza kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja kama adhabu yake . Mkwasa amesema kama klabu pia wameiandikia TFF barua kupinga uamuzi huo na kulieleza jambo hilo kwa kina sambamba na maelezo ya mchezaji husika . ” Simba SC wanasema Pius wamemsajili tarehe 2 juni 2017 ilihali kipindi hicho alikuwa ndani ya mkataba na Mbao FC kitu ambacho ni makosa kwa sababu hawakuwafuata Mbao . Sisi tumewafuata Mbao na mche...