Machapisho

Kairuki: Serikali Haitaajiri Walimu wa Masomo ya Sanaa

Picha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari. Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao "Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa ...

TANZIA: Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa AFARIKI Dunia

Picha

Mfahamu zaidi Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro

Rais Dkt Magufuli juzi Mei 28, 2017 alimteua na jana, Mei 29, 2017 alimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro ambapo amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu atapangiwa kazi nyingine. Simon Sirro ambaye awali alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwisho wa makala hii tutawaorodhesha wengine waliomtangulia kushika wadhifa huo. Simon Nyakoro Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963. Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria. Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi. Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi w...

TANGAZO:TAWFIQ MONEY SERVICE WAKALA WA KIBANK BUNDA

Picha
ANAPATIKANA BARABARA YA BOMANI MKABALA NA STENDI YA ZAMANI TUNATOA HUDUMA ZIFATAZO KWAJIA YA BANK: -KUFUNGUA AKAUNTI ZA CRDB,EQUITY ,POST  BANK. -KUWEKA PESA -KUTOA     PESA -KUTUMA  PESA -KULIPIA ADA ZA SHULE -KULIPIA MALIPO MBALIBALI YA SEREKALI. KUWEKA PESA NA KUTUMA NI BURE KABISA.  PIA TUNATOA HUDUMA ZA :- - BIMA ZA MAGARI - MOTOR VAHICLE PIA TUMEFUNGUA OFISI  NYINGINE NYASURA STENDI UPANDE WA GARI ZINAZO KWENDA MWANZA KARIBUNI KUPATA HUDUMA LUKU VING'AMUZI VYA TV SIMU NAMBA 0784699901,0756141420

Upepo Mkali Kuvuma Dar, Wananchi Watakiwa Kuchukua Tahadhari..!!!

Picha
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya ukanda wa pwani. Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imesema upepo huo unatarajiwa kuendelea hadi kesho. Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Mamlaka imesema hali hiyo inatokana na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania. TMA imetoa angalizo kwa watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki

CUF ya Maalim Seif Wakataa Maamuzi ya Mahakama Kuhusu CUF ya Lipumba..!!!

Picha
Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) kupitia wakili wake, Hashimu Mziray imewasilisha kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kupinga uamuzi uliotolewa Mei 21, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa kuyatupilia mbali maombi yao waliyoyafungua mahakamani hapo dhidi ya wabunge wawili, Magdalena Sakaya(Kaliua),  Maftah Nachuma(Mtwara Mjini) na wenzao sita. Walikuwa wakiomba mahakama hiyo iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama. Akiwasilisha kusudia la kukata rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mziray alisema hawakuridhika na uamuzi huo kwa sababu si kweli kuwa  CUF haina bodi ya wadhamini. Wakili Mziray alisema CUF ni chama ambacho kipo hai, kina wabunge, madiwani, majengo, wanachama na hata Msajili wa Vyama vya Siasa hajakifuta. Alibainisha kuwa Hakimu Mashauri akulielewa tangazo la Wakala wa Vizazi na Vifo(RITA) hivyo wanaiomba Mahakama Kuu kutengua uamuzi wake kwa madai kuwa ni...

Serikali Yatenga Bilioni 1.5 Kupambana na Ugonjwa wa Ebola Nchini..!!!

Picha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa zimetumika kuukabili ugonjwa huo. Ummy amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda  katika nchi ya DRC na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini. "Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania, tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC. Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kama hana virusi nyemelezi. Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yet...