Machapisho

Dalili za Ugonjwa wa zinaa - kisonono

Picha
Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao. Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani. Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu. DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO. Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - mau...

AJALI YAUWA WAWILI NA 26 KUJERUHIWA MKOANI SINGIDA

Picha
Watu wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 26 wamejeruhiwa na kulazwa katika hosipitali ya mkoa wa Singida baada ya basi la kampuni ya National Express lililokuwa likitokea Iramba kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika wilaya ya Mkalama. Mganga mkuu wa hosipitali hiyo daktari John Mwombeki amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na amesema amepokea majeruhi 26 na maiti 2 moja ni ya dereva wa basi hilo bwana Athuman Said na nyingine ni ya mama aliyetambulika kwa jina la Janeth ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Maluga wilayani Iramba. Kamanda polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa polisi ACP Debora Daudi Magiligimba amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva na kutokufuata sheria za barabarani na kusisitiza madereva kuwa makini ili kuepukana na ajali za kizembe kama hizi.

Mourinho: Haondoki mchezaji yoyote zaidi ya Johnstone ikifika January.

Picha
Kwenye habari ambayo imewashangaza wengi sana manager Jose Mourinho ametoa taatifa kwamba ukifka mwezi January hatamruhusu mchezaji yoyote kusepa kwenye club hiyo zaidi ya Sam Johnstone tena kwa mkopo. Kwa muda mrefu kumekua na tetesi za wachezaji kadhaa wa Manchester united kwama watasepa kwa mkopo na wengine wataondoka moja kwa moja ukifika mwezi January. Lakini Jose ametoa kauli iliyomaliza tetesi hizo. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jose alisema, “Sam Johnstone ndio mchezaji pekee ambaye nitamruhusu aende kwa mkopo kwasababu hajapata kabisa nafasi ya kucheza, anahitaji kucheza. Sitaki kuuza wachezaji na bodi ya timu inaniunga mkono kabisa.” “Lakini kama nilivyosema kama mchezaji anataka kuondoka ikiwa anadhani hapati nafasi ya kutosha ya kucheza basi anaweza kwenda kama condition zetu zitatimizwa. Lakini kama timu hatuna mpango wa kumuuza mchezaji yoyote” Mourinho alimaliza kabisa kwa kusema kwamba hawajapokea ofa yoyote ambayo imewashawishi kumru...

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI RUANGWA

Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016. Baadhi ya wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UCHUMI WA NCHI WAZIDI KUIMARIKA - DKT PHILIP MPANGO

Picha
Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango akizungumza na waandishi wa habari juu ya ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana kuongezeak kwa uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbaliu ya kilimo, biashara, viwanda na migodi. Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii. Takwimu za ukuaji wa uchumi nchini unaonyesha unaendelea kukua kwa kiasi kubwa zaidi kulinganisha na mataifa mengine na kuwa miongoni mwa Nchi za bara la Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakuwa ikifuatiwa na Congo DRC na Rwanda,Kenya, Uganda, Burundi, Afrika ya Kusini, Zambia na Malawi. Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango amesema kuwa kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi, uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali za kwa jamii ikiwemo afya, elimu na maji. "Kasi ya kuongezeka au ...

HALMASHAURI YA KINONDONI YASAINI MKATABA WA BILIONI 22 ZA MRADI WA UBORESHAJI WA JIJI LA DAR

Picha
Halmashauri ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22 na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara. Akizungumza na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango wa mradi huu unalenga  kuboresha miundombinu ya barabara ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini. "Katika uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla." Aidha meya ametaja  barabara ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.2...

Serena Williams hatimaye avishwa pete na mmiliki wa Social network.

Picha
Star wa tennis Serena Williams amefanikiwa mengi sana kwenye maisha yake na kutengeneza pesa nyingi sana. Lakini kwa sasa kama mtoto wa kike lazima atakua anataka kukamilisha maisha yake kwa kuolewa na mtu amendae. Kuna kipindi zilitoka taarifa kwamba Serena anatoka na rapper Drake lakini haikuthibitishwa na kuishia kama tetesi licha ya picha zenye utata kusambaa kwenye internet. Sasa hivi inajulikana kwamba Serena yupo kwenye uhusiani na mmiliki wa social networt maarufu “Reddit”. Alexis Ohanian ni co found wa mtandao huo maarufu sana kwa nchi za Ulaya na Marekani. Sasa hivi taarifa ni kwamba jamaa huyo amemvalisha pete Serena na labda wanaweza kufunga ndoa mwakani. Wawili hawa wameshaonekana pamoja wakifurahia maisha kwa muda mrefu sana na sasa hivi wameweka rasmi uhusiano wao.