Machapisho

HESLB Yafafanua vigezo Utoaji mikopo, Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa

Picha
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017. Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu. Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza. Katika mkutano na waandishi wa habari jana (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupokea maombi mwezi ...

Ufafanuzi Kuhusiana na Umri wa Miss Tanzania 2016 Diana Edward Loy Watolewa

Picha
Usiku wa Jumamosi, mrembo wa Kinondoni, Diana Edward Loy alitwaa taji la Miss Tanzania 2016 katika fainali zilizofanyika jijini Mwanza. Hata hivyo pamoja na ushindi huo, haikuchukua muda akaanza kuubeba mzigo wa umaarufu kwa kusambaa taarifa zinazohusiana na umri wake. Taarifa iliyosambaa ilisema: MISS TANZANIA 2016 🙊🙊🙊🙊🙊🙊 JINA:Diana Edward Lukumai UMRI:Miaka 18 ELIMU:Shahada(degree) Hii ina maana; Alianza Chuo akiwa na miaka 15 Alianza Form one akiwa na miaka 9 😂😂😂😂😂😂 Ingawa sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili. Kaimu afisa habari wa mrembo huyo, Charles William amelazimika kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya habari za mshindi huyo: Napenda kuujulisha Umma yafuatayo; 1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshind...

Tazama Video Fupi Aliyofanya Miss Tanzania Huko Umasaini Kuhusu Ukeketaji wa Wasichana wa Kike

Picha
Kwa wasichana wengi wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania, ushindi huja kwa surprise na muda mfupi kugubikwa na matarajio makubwa kutoka kwenye jamii. Lakini si kwa Miss Tanzania 2016, Diana Edward aliyevishwa taji Jumamosi hii, jijini Mwanza. Tangu ameanza kushiriki shindano hilo katika hatua za vitongoji, mrembo huyo alikuwa amejianda kuwa Miss Tanzania. Diana mwenye asili ya kimasai, kwa muda wote wa ushiriki wa shindano hilo, aliuweka mbele utamaduni wake, kitu ambacho ni nadra kwa Mamiss wengine ambao wengi wao wamekulia mjini. Amekuwa akijihusisha na shughuli za utetezi wa masuala ya kijamii, hasa watu wanaoishi mazingira magumu, pamoja na kampeni za kutokemeza ukeketaji. Wiki moja iliyopita alitoa documentary fupi kuhusu ukeketaji unaofanyika katika jamii yake ya kimasai. Yeye mwenyewe ni mhusika. Video: 

Unaamini Kuna Uchawi Katika Mapenzi? Soma Hii Inakuhusu

Picha
BILA shaka msomaji wangu uko poa, kwa wewe ambaye unasumbuliwa na shida mbalimbali za kidunia, nakuombea kwa Mungu upate ahueni. Wiki iliyopita tulianza kujadiliana kuhusu mada hii kama inavyojieleza. Je, wewe unaamini kwamba kwenye mapenzi kuna uchawi? Unaamini kwamba kuna kitu kinaitwa limbwata? Je, ni kweli mtu anaweza kwenda kwa mganga na akafanikiwa kumpumbaza mwenzi wake akili? Nakushukuru wewe uliyetumia muda wako kunipa majibu ya jinsi unavyoyaelewa mambo haya.  Majibu niliyoyapata yalikuwa katika makundi mawili; wapo waliosema wanaamini ni kweli kuna uchawi katika mapenzi, wakaenda mbali na kutoa mifano iliyowatokea au waliyoishuhudia na kuwafanya waamini kwamba kweli kuna uchawi katika mapenzi. Msomaji wangu mmoja kutoka Unguja, Zanzibar, alisema anao ushahidi wa jinsi mume wa rafiki yake alivyoendewa kwa mganga na kimada wake hadi akafikia hatua ya kutelekeza familia ya mke na watoto watatu, akahamia kwa kimada. Unaambiwa mpaka leo hasikii haambiwi, ameikana familia ya...

Miss Tanzania 2016 ameona kilichosambazwa kuhusu elimu yake, kayasema haya

Picha
Baada tu ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2016, Mrembo  Diana Lukumay  alianza kupokea msg za taarifa zilizosambazwa mitandaoni kuonyesha kwamba alifeli kidato cha nne lakini pia pamoja na hayo bado CV yake ilionyesha anayo degree. Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema ‘Jina langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na umri wangu ni miaka 18, nilizaliwa Arusha Mount Meru Hospital na ni mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto wanne’ ‘Nilisoma shule ya msingi ya serikali Levolosi 2005-2011, sekondari ya kutwa ya serikali Arusha 2012 -2015,  matokeo ya kidato cha nne nilipata darala la pili… nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa kwenda shule ya Wasichana Bwiru Mwanza’ ‘Kwakuwa nilikua tayari nipo kwenye tasnia ya urembo niliamua kutojiunga na masomo hayo kwakuwa yalishaingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya kitongoji ambapo nilijiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016/2017)...

YEMI ALADE, TEKNO NA JOSE CHAMELEONE KUTUA ‘FIESTA’ DAR, ORODHA YA WASANII WA TANZANIA IPO HAPA

Picha
Tamasha kubwa la muziki la Fiesta linaelekea ukingoni, kwenye show ya mwisho ambayo huwa kubwa zaidi ikiwakutanisha wasanii mbalimbali kwenye steji moja. Wakali wa muziki wa Afrika, Yemi Alade, Tekno na Jose chameleone ni baadhi ya wasanii wa nje watakao shambulia jukwaa la tamasha hilo, huku tukiendelea kusubiri msanii wa Marekani kutangazwa kama ilivyo desturi ya tamasha hilo. Pia Tamasha la burudani la Fiesta 2016 limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba watamleta msanii wa Marekani Jay Z katika show ya Fiesta Dar es salaam. Mapema Jumamosi hii zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam. Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii: Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; pich...

BREAKING NEWZZZ…BONDIA THOMAS MASHALI AUWAWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Picha
Bondia Thomas Mashari ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo. BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali ‘Simba asiyefugika’ ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na mwili wake umeokotwa maeneo ya Kimara kabla ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Rais wa Oganizesheni ya Ngumi za kulipwa (TPBO) Yassini Abdallah ‘Ustadh’ alisema mauti yalimkuta bondia huyo baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na wasamalia wema maeneo ya Kimara. “Ni kweli Mashali amefariki dunia nimepokea Habari hiyo muda mfupi uliopita sasa nipo njiani naelekea Muhimbili” alisema Ustadhi. Taarifa za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadae na ndugu wa marehemu.