Maandamano ya Ukuta ni ndoto ya mchana’
MSOMI maarufu nchini, Profesa Benson Bana na mwanasiasa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Leticia Mosore wamesema maandamano yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), hayawezekani kwani ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa Taifa. Aidha, maandamano hayo ya nchi nzima imeelezwa kuwa ndio kifo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwani kila chama kimekuwa kikihangaika kivyake. “Wanaotaka kuandamana wanajidanganya na kuwalaghai wenzao kwani kufanya operesheni ni suala la dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo hayawezekani kabisa,” alisema Profesa Bana katika mahojiano maalumu na Idara ya Habari (MAELEZO). Mhadhiri huyo Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliongeza kuwa wanaojiita Ukuta ni kwamba Rais John Magufuli amewanyima ajenda, kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze kutapatapa wasijue nini cha kufanya. Alisema kama viongozi wa Ukuta ni w...