Machapisho

TIBA KWA MATATIZO YA MACHO

Picha
MAUMIVU YA MACHO  Yako magonjwa ya aina nyingi ya matatizo ya macho kutegemeana na chanzo cha tatizo. japo ntagusia kuhusu matatizo mengine ya macho ila ntaongelea zaidi JICHO KUCHOMA CHOMA NA KUPELEKEA MAUMIVU SABABU YA TATIZO   Kuangalia sana tv,simu au kompyuta Kusoma kwa muda mrefu Ukosefu wa usingizi kutumia vikuza muonekano (lenses) TIBA YAKE  © tibazakissuna.blogspot.com > Tumia MAJI YA BARIDI kuoshea uso  > Tumia ROSE WATER kusafishia jicho kwa kuweka kwenye pamba ukikosa tumia matone ya SHUBIRI  > ASALI na MAJI changanya kwa ujazo sawa kisha pakaa kwenye jicho likiwa lime jifunga > Kata kipande kidogo cha TANGO kisha weka kwenye jichoukiwa umelifunga ukiwa umejilaza chali  kwa dakika 15 > Unaweza kukosa vyote sio mbaya pia kama utafunga jicho na kujiweka kijiko juu yake kwani ubaridi wake huleta nafuu MATATIZO MENGINE YA JICHO   > JICHO LILIL...

Shubiri mwitu tiba ya magonjwa ya kuku

Picha
Kuku ni moja ya miradi inayofanywa kwa wingi na watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wakulima na wafugaji, na wanaofanya shughuli nyinginezo.     Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili na kuzungumziwa mara kwa mara ni magonjwa yanayoshambulia kuku, bila wafugaji kufahamu ni nini cha kufanya.     Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku, zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya tiba rahisi ya asili kwa kuku ni kwa kutumia shubiri mwitu maarufu kama Aloe Vera. Mmea ambao umekuwa ukisifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu, wanyama na ndege. Shubiri mwitu mbali na kutibu kuku, hutumika pia kwa wanyama na binadamu   Shubiri mwitu ( Aloe ) imekuwa ikitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo ...

RAIS MAGUFULI ASEMA UTAWALA WANGU SITAKI KULIMBIKIZIA WATU VYEO ,MBUNGE HAWEZI KUWA RC AU DC

Picha
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa katika utawala wake hatateua mbunge kuwa mkuu wa Mkoa au Wilaya. Amesema lengo ni kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji, kwamba "Haiwezekani katika watanzania mil. 50 tukose watu hadi turundie watu vyeo. Tunataka tuchape kazi kwa ufanisi na ufanisi hauwezi kuja kwa kumrundikia mtu vyeo".

Vita kumrithi David Cameron yapamba moto

Picha
Anayetaka kugombea kupitia chama tawala cha Conservatives cha nchini Uingereza, Stephen Crabb. Na Leonard Msigwa VITA ya kuwania uongozi wa juu ndani ya chama tawala cha Conservatives cha nchini Uingereza, imeanza kushika kasi. Wanasiasa mbalimbali wenye nguvu na uwezo wameonyesha nia ya kutaka kumrithi waziri mkuu aliyejiuzulu, David Cameron. Steveb Crabb amekuwa mwanasiasa wa kwanza kujitokeza hadharani na kutamka nia yake ya kutaka kuirithi nafasi hiyo. Crab ameweka bayana kwa kusema kwamba: “Najitokeza kuwania nafasi ya kiongozi wa juu ndani ya chama na baadaye kuwa waziri mkuu. Naipenda nchi yangu, nakipenda chama changu”. Mwanasiasa huyo alijiunga na Conservative mara tu alipohitimu elimu yake ya chuo kikuu. Alianza siasa rasmi 1998 alipochaguliwa kama mwenyekiti wa chama cha Southwark North and Bermondsey Conservative Association, nafasi aliyodumu nayo hadi mwaka 2000. Mwaka 2001 aligombea ubunge jimbo la Preseli Pembrokeshire ambako alishika nafasi ya pili. A...

MAONI YA MDAU: BURE YA MANJI ILIVYOIATHIRI YANGA

Picha
Na Isack, Babati Manyara Kitengo walichofanya Yanga cha kuruhusu mashabiki kuingia bure uwanjani kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe kimeikosesha klabu fedha nyingi sana ambazo wanazihitaji kwa kuendekeza siasa ambazo hazina maana. Kulikuwa hakuna sababu ya kuacha mashabiki waingie uwanjani bure lakini kwa sababu ya siasa za soka la kibongo, waliona sawa kukubali kuingia hasara. Mechi kubwa dhidi ya TP Mazembe walitakiwa waitumie vizuri kupata pesa ambayo wangewalipa posho nzuri wachezaji wao na hata kufanya usajili wa wachezaji wapya. Katika hili TFF pia wameonesha udhaifu, wameshindwa kuwazuia Yanga kuruhusu mashabiki kuingia bure kitu ambacho ni hatari kiusalama hususan katika mechi ya kimataifa ambayo inasimamiwa na CAF. Vurugu zilitotokea uwanjani wakati watu wakijaribu kulazimisha kuingia uwanjani baada ya mageti kufungwa ni baadhi ya matukio ambayo yalihatarisha usalama, kuna mageti yalivunjwa, huku kukiwa na uharibifu mwingine kama mabomba ya gesi haikuwa ...

MJUE MITCHY BATSHUAYI, JEMBE LINALOSUBIRIWA KUTUA CHELSEA

Picha
Na Naseem Kajuna Kwa ripoti zilizojitokeza siku ya jana Chelsea wanakaribia kumsajili Mchezaji wa Marseille na timu ya Belgium Mitchy Batshuayi kwa kiasi cha Paundi million 33. Kama watu wengi, hakika ulibaki unatoa macho ulipopata habari hii na ukabaki ukijiuliza Batshuayi ni nani. Mitchy Batshuayi Tunga 22 ni mshambuliaji wa Belgium mwenye asilia ya kikongo anayechezea klabu ya Marseille nchini Ufaransa. Kwa sasahivi Mitchy Batshuayi yuko nchini Ufaransa akijaribu kuisaidia nchi yake Belgium kutwaa taji la michuano ya Euro 2016. Mitchy Batshuayi alifunga goli kwenye mechi ya mwisho ya Belgium walioshinda 4-0, lilikuwa goli lake la tatu kwenye mechi 6 tu kwa ajili ya nchi yake. Mitchy Batshuayi ni mmoja ya wachezaji wanaosakwa na klabu nyingi sana duniani hasa ukizingatia kwamba klabu yake ya Olympique Marseille imeshatangaza kwamba hawategemei mchezaji huyu kurudi kwenye klabu yao kwani wanahitaji kumuuza ili wapate fedha. Batshuayi alizaliwa Brussels Ubelgiji, na alijitambulis...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KWENYE UTEUZI WAKE WA WAKUU WA WILAYA SOMA HAPA LIVE!!

Picha
Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Ndg.Emile  Ntakamulenga , kwa kile kilichoelezwa kuwa aliteuliwa kimakosa. Rais amemteua Ndg.Nurdin Babu kujaza nafasi hiyo. Kabla ya kutengua uteuzi wa Ntakamulenga, Rais pia alishatengua uteuzi wa DC wa Ikungi Ndg.Fikiri Avias na kumteua Bw.Miraji Mtutura ambaye alikuwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza kujaza nafasi hiyo.